Mabinti Mnaotuuzia Condoms Pharmacy muwe mnatupa maelekezo zaidi kuhusu Matumizi ya Condoms sio Mnatuonea Aibu Wateja Wenu

Bueno

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
34,610
Reaction score
59,577
Wakuu, ngoja leo niseme jambo moja ambalo nimepatwa nalo hapa katikati nilipokua kwenye mihangaiko yangu ya kutaka kukipata kilinda afya yangu ili nisipatwe na STI bila kutarajia sababu sikujikinga.

Nilitoka zangu nikaelekea Pharmacy moja kubwa tu na kwenye hii Pharmacy hua kuna shift ya wafanyakazi ambao wana jinsia ya kike. Age yao inaweza kua katika ya miaka 20-25 yaan ni mabinti tu.

Sasa hio siku nimeenda kuhitaji huduma nikamuuliza kuhusu Condoms nikashangaa ghafla binti kabadirika sura. Nikaanza kutaka maelekezo zaidi na maelezo zaidi kuhusu hizo Condoms nikashangaa binti hataki kabisa kunipa ushirikiano. Yaan binti akagoma kabisa kunipa maelekezo kuhusu hio Condom ubora wake upoje na inawezaje kunisaidia nisiweze kupata maambukizi. Bei ya Condom 1 alikua anauza 1000 yaan Buku tu.

Basi nikajaribu kuhitaji maelekezo zaidi kuhusu hizo Condoms binti akagoma kabisa hataki kunipa ushirikiano kabisa tena alikua km ananiharakisha niondoke bila hata kununua hio Condom. Wakuu nilishangaa sana.

Nataka niwaambie nyinyi Wahudumu wa Pharmacy hususani nyinyi mabinti tunapokuja Pharmacy kuhitaji huduma km tunavyouliza kuhusu dawa ya kikohozi au mafua inavyofanya kazi na tukiuliza kuhusu Condoms mtuelezee inavyofanya kazi na jinsi gani ya kuitumia vizuri ili mtu asipate maambukizi au kumtia mtu mimba.

Ninapokuja kununua Condoms usianze kua wet tena unaanza kuona aibu aibu na wewe unaanza kushikwa na hamu sijaja kununua hio Condom kwa ajili yako kumbuka wewe upo kazini hapo fanya kazi yako kwa weledi pasina kuonea wateja aibu.

Ndio hivyo tu wakuu nyie mabinti Wahudumu wa Pharmacy muwe na nidhamu na wateja tunaokuja kununua Mipira msituangalie usoni mkatuona km Wazinzi sana. Msilete ibada kwenye Pharmacy unataka kunihubiria kwamba nisivunje amri ya sita "Usizini" kwani nimekutuma?
 
Kuna binti wa famasi hapa ngoja nimpe asome
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…