Mabinamu ya kweli haya jamani....

Xpin ni jina la babu yangu mzaa baba. Hahaha kule kwetu wazee wenzie walikuwa wanashindwa kulitamka wakawa wanamwita Iribini. Alikuwa kidume. Alikuwa na wake wanne na watoto 38. Nahitaji kufuata nyayo zake ili kudumisha mila.

Wewe una hatari kubwa na jina hilo la urithi wa babu.Tutaongea faragha nikufafanulie
 
maeneo yangu ya kujidai MAKAMBAKO,mwanzoni mwa miaka ya tisini kulikuwa na mtindo wa wakinga kununua FUSO!kuna watoto wengi sana waliitwa majina yafuatayo kwa vibongo tofauti:
FUSO SANGA
FUSO MAHENGE
FUSO MBILINYI
FUSO TUMTEMEKE
FUSO MGAYA
BEDFORD SANGA
SCANIA MAHENGE
STAUT MSIGWA

yani ni vurugu tu!..............

Na wale jamaa zet wengine wale;

Anapenda Mjusi
Kuleni Fisi
Ibrahim Mbuzi
Achanana Simba
Hashim Komba
Michael kaTembo
Juma Komba
Anakula Kinyoga

Hahaha! Vululu vululu!
 
yah vyema!,huyu bint nimempa jina la bibi yake mzaa mama yake,yaani jina la mama mkwe wangu,hii ni kuepusha utata kama huu aliouleta FL1
Na wewe ndo hilo jina la urithi pia hatari kubwa.siku hiz haturithishi majina,utarithi na tabia au destiny.
 
Je kuna uhusiano wowote kati ya jina na tabia ya mtu?
Sana tu,nina mifano kadhaa ya katika bible inayohusianisha tabia na jina.
lakini ngoja nikupe mmoja,wazaramo wanapenda kuwapa watoto wao majina ya shida,majuto,siyawezi,mtakuja,sikujua.Si unaona maisha yao jinsi ynavoelezea aina ya majina yao?
 
Na wale jamaa zet wengine wale;

Anapenda Mjusi
Kuleni Fisi
Ibrahim Mbuzi
Achanana Simba
Hashim Komba
Michael kaTembo
Juma Komba
Anakula Kinyoga

Hahaha! Vululu vululu!

hahahaha watu wana hatari kuleni Fisi :)
 
Sana tu,nina mifano kadhaa ya katika bible inayohusianisha tabia na jina.
lakini ngoja nikupe mmoja,wazaramo wanapenda kuwapa watoto wao majina ya shida,majuto,siyawezi,mtakuja,sikujua.Si unaona maisha yao jinsi ynavoelezea aina ya majina yao?

Hivi Kikwete si Mzaramo yule au?
 
Sana tu,nina mifano kadhaa ya katika bible inayohusianisha tabia na jina.
lakini ngoja nikupe mmoja,wazaramo wanapenda kuwapa watoto wao majina ya shida,majuto,siyawezi,mtakuja,sikujua.Si unaona maisha yao jinsi ynavoelezea aina ya majina yao?

na kweli ZD mtoto ukimpa shida ,mala Tabu ni kweli hayo yote yatamwandama

ukimpa mtoto jina la amani Precious mambo yanakuwa tambalale kabisa

Sasa umpe mtoto jina la kimada wako au serengeti boys mambo yatakuwa yale yale maji hufata mkondo
 
Ukiona mke/mme anatoa jina la ex wake kwa mtoto, lazima utie shaka kubwa sana. Kwanza lazima huyo ex awe hafahamiki kwa mwenzi wake. Wengi wanapoanza mahusiano huwa wanapenda sana kujua habari za mahusiano ya wenzi wao kabla hawajaingia kwenye hayo mahusiano mapya. Most of them huwa wako interested kujua ma-ex wao wako wapi, kwanini waliachana na mengineyo.

Iwapo discussion kama hizo zilifanyika na jina hilo halikusikika, na ikaja kugundulika kwamba ni jina la ex wa mwenzi, hapo naona ni sawa na kuiweka ndoa rehani/poni. Kupona kwa ndoa hiyo kunategemea uwezo wa kuigomboa (maelezo fasaha ya kushawishi kwamba hakuna kitu kinachoendelea kati ya wahusika). Vinginevyo mwenzi anaweza kupigia mstari jibu sahihi. Hata kama hakuna kinachoendelea kati yenu, lakini kunaweza kuwa na maswali mengi ya ziada. Kwanini hakutaja hilo jina wakati wengine wote walitajwa? Je, inaweza kuwa inaashiria kwamba kuna mambo yanaendelea underground?

Kitu kama hicho kikigundulika ni balaa kubwa sana, ndoa inaweza kusambaratika!
 
na kweli ZD mtoto ukimpa shida ,mala Tabu ni kweli hayo yote yatamwandama

ukimpa mtoto jina la amani Precious mambo yanakuwa tambalale kabisa

Sasa umpe mtoto jina la kimada wako au serengeti boys mambo yatakuwa yale yale maji hufata mkondo

Jirani yangu mmoja anaitwa Richman. Ni maskini wa kutupwa mtaani. Nyie jidanganyeni na majina tu. Mafanikio ya mtu hayaletwi na majina bana. Kwa hiyo wanaoitwa Muhammad, Suleiman, Jacob, Ibrahimu, Isaka, Isaya, Maria wote wataenda peponi siyo?
 
ha ha ha Mpwa you made may day!!
 
ha ha ha Mpwa you made may day!!

Mpwa kuna watu wanajidanganya na majina hapa. Majina kama kina kinjekitile, mirambo, mkwawa nk sijui itakuwaje tukiwapa watoto wet? Nadhani wakoloni warudi tena ili vita zipigwe. LOL!
 
Sasa umpe mtoto jina la kimada wako au serengeti boys mambo yatakuwa yale yale maji hufata mkondo

Kwa hiyo na mwanao ataishia kuwa kimada/serengeti boy? Hiyo ni imani tu na inaweza kuwa imani potofu.

Kuna watu wana majina yaliyojaa kila aina ya utukufu lakini ukiangalia maisha yao hata ya kwangu yana nafuu mara 100.

Binafsi siamini kwamba jina has something to do with tabia ya mtu, ingawa majina mabaya yanaweza kumjengea mazingira mabaya mtoto. Waswahili huwa wana amini kwamba maneno huumba matukio/vitu. Kama mtu anaitwa Majuto ama Masumbuko, basi siku zote akiitwa hilo jina wanakuwa kama vile wanamuombea apate majuto ama asumbuke katika maisha yake.
 
Mpwa kuna watu wanajidanganya na majina hapa. Majina kama kina kinjekitile, mirambo, mkwawa nk sijui itakuwaje tukiwapa watoto wet? Nadhani wakoloni warudi tena ili vita zipigwe. LOL!
Tatizo ni huu uzungu uliotuingia maana mtu kumpa jina la Kimarekani mtoto wake ndo ishakua fashion!!
 
Kwa hiyo na mwanao ataishia kuwa kimada/serengeti boy? Hiyo ni imani tu na inaweza kuwa imani potofu.

Kuna watu wana majina yaliyojaa kila aina ya utukufu lakini ukiangalia maisha yao hata ya kwangu yana nafuu mara 100.

Binafsi siamini kwamba jina has something to do with tabia ya mtu, ingawa majina mabaya yanaweza kumjengea mazingira mabaya mtoto. Waswahili huwa wana amini kwamba maneno huumba matukio/vitu. Kama mtu anaitwa Majuto ama Masumbuko, basi siku zote akiitwa hilo jina wanakuwa kama vile wanamuombea apate majuto ama asumbuke katika maisha yake.
Kina Masumboko Lamwai wanapeta tuu!!
 
Jirani yangu mmoja anaitwa Richman. Ni maskini wa kutupwa mtaani. Nyie jidanganyeni na majina tu. Mafanikio ya mtu hayaletwi na majina bana. Kwa hiyo wanaoitwa Muhammad, Suleiman, Jacob, Ibrahimu, Isaka, Isaya, Maria wote wataenda peponi siyo?

Nakwambia watu tungekaa tu kungoja kwenda peponi....kisa na sababu majina!!
 
Ngoja nikakabatize upya kabinti kangu; Nakapa jina la Elizabeth, huwezi jua kakichukua uraia wa Uingereza mambo yanaweza kuninyookea.
 
Back
Top Bottom