Mabasi ya Usiku: Visa nilivyo kutana navyo!

Mabasi ya Usiku: Visa nilivyo kutana navyo!

Siku nyingine panda zile luxury....konda hawezi kukuuliza majina mwanzo wa safari adi unafika
 
KERO JUU YA WATU WANAOTOA MAHUBIRI AU KUTANGAZA BIDHAA ZAO KWENYE MABASI YA MIKOANI, KIUKWELI WANAKWAZA SANA, USAFIRI NI STAREHE YA MTU.

KUNA WATU WANAENDA MISIBANI, KUNA MWINGINE KAFUKUZWA CHUO HANA ADA, KUNA MWINGINE KATOKA KUACHWA NA MUME AU MKE.

KIUKWELI MAMLAKA HUSIKA WALIANGALIE HILO, MAANA LIMEKUWA KERO KWA ABIRIA, AU WENZANGU HUWA MNAONA KAWAIDA?
 
Sawa sio lazima ule ila unaweza kutoa polite excuse e.g. ninatumia dawa ambazo haziniruhusu chakula sasa hivi au namna nyingine utakavyoana inafaa. Sio kukataa kavu-kavu bro. Iko siku itakukosti.
Sukukataa kwa ubaya. Nilimueleza kuwa siwez kula nikiwa nasafiri tumbo alikostable..
Yeye alikua anasisitizia kuwa amepika yeye na zimekauka vzuri azitaleta shida.

Itani cost nini? Mbona akuna ubaya wowote hata ukikataa kwa kavu kavu
 
Sukukataa kwa ubaya. Nilimueleza kuwa siwez kula nikiwa nasafiri tumbo alikostable..
Yeye alikua anasisitizia kuwa amepika yeye na zimekauka vzuri azitaleta shida
Ok; Hilo ni jawabu zuri sana na kama alitamka naomba ukanywe maji, manake aliridhika.
 
No 1, inatia shaka mtoto miaka 4 anabadilishwaje nepi kwenye gari

No 6 ,madereva wanaboa sana kwenda kwenye hoteli hizo nagharama juu wao na makonda wao wanakula bure na dereva kwamwezi anapewa poshoyake kwakupeleka abiria wale pale

Kunasiku ilibidi niingie gharama kumnunulia bibi mmoja msosi ananjaa pesakidogo , liangaliwe nahilo
Ulichokiandika hakihusiani na mabasi ya usiku, hebu fafanua hili la kubadilisha nepi, inamaana kila basi la usiku ulilopanda ulimkuta huyo mtoto akibadilishwa nulifanikiwa! basi ulilopanda ulitapikiwa! Jambo moja ninalokubaliana na wewe ni hauna mazoea ya kusafiri kwa basi, yaani ni mtu wa ndege tu.
 
Baada ya mabasi kuanza safari za Usiku, nimekuwa nikisafiri sana hasa kama nikikosa ndege. Mabasi hayo yana raha na karaha, hizi ni baada ya karaha;

  1. Jirani yangu anabdili nepi ya mtoto wa miaka 4 , kitu kinanuka balaa, safari nzima kuziba mdomo.​
  2. Jirani ile tumefika tu Kabuku kabla ya Segera pale michungwani tukitoka dar kuelekea Arusha, akanitapikia, alikuwa amekula makande, aloo si poa.​
  3. Konda kila saa ananiuliza kwanguvu jina langu na kituo ninachoshukia.​
  4. Gari ina AC, watu wanaziba zile buttons, joto kali unasinzia kwa kukosa oxygen.​
  5. Gari inasimama hotelini, chips kavu elfu 5 na mshikika mmoja elfu 2.​
  6. Wakati tukifika hotelini, dereva anashuka fasta, wao wanatwambia kula dakika 10, wameandaliwa na wanakula kwa muda ila abiria wa mwisho kushuka hata hajafika msalani anaambiwa muda umeisha gari inaondoka.​
  7. Kukaa siti moja na mkaka, tangu amepanda ameweka tunini twake masikioni, hata salamu hamna , masaa 8 hatujaongea eti tunafika Tengeru ananiuliza hapa ni wapi nikamwambia sijui labda ni Morogoro.​
  8. Huyo mkaka nimekaa naye kwenye TAHMEED ya Nairobi, akapiga simu kwa mpenzi wake wanaongea zaidi ya dakika 60 kimapenzi, kuna vitu walikuwa wanaongea mpaka ninasisimka mwili .​
  9. Konda kuuliza kituo ninachishukia kwa sauti kubwa kila mtu ajue kwetu ni Kishumundu.​
Sasa unasisimka kwenye maongezi ya watu jamani🤣🤣🤣🤣ehh
 
KERO JUU YA WATU WANAOTOA MAHUBIRI AU KUTANGAZA BIDHAA ZAO KWENYE MABASI YA MIKOANI, KIUKWELI WANAKWAZA SANA, USAFIRI NI STAREHE YA MTU.

KUNA WATU WANAENDA MISIBANI, KUNA MWINGINE KAFUKUZWA CHUO HANA ADA, KUNA MWINGINE KATOKA KUACHWA NA MUME AU MKE.

KIUKWELI MAMLAKA HUSIKA WALIANGALIE HILO, MAANA LIMEKUWA KERO KWA ABIRIA, AU WENZANGU HUWA MNAONA KAWAIDA?
Sio kawaida kabisa. Leo hapa nimegundua kumbe siko peke yangu ninayelichukia jambo hili. Inaelekea hilo ni dili kati ya Konda/dereva na huyo hustler kwani baada ya vituo vichache hushuka.
Ni kweli hio ni kero kubwa kwa abiria i.e. Mtu unknown anawasikilizisha kwa nguvu wasafiri matangazo yake ya biashara. Sio haki. Mtu akitaka bidhaa asubiri akifika aendeko anaweza kuitafuta mahali stahili. Bidhaa za kwenye mabasi ni HATARI e.g. zikimdhuru mtumiaji nani atawajibishwa/atatolea maelezo?
 
Ulichokiandika hakihusiani na mabasi ya usiku, hebu fafanua hili la kubadilisha nepi, inamaana kila basi la usiku ulilopanda ulimkuta huyo mtoto akibadilishwa nulifanikiwa! basi ulilopanda ulitapikiwa! Jambo moja ninalokubaliana na wewe ni hauna mazoea ya kusafiri kwa basi, yaani ni mtu wa ndege tu.
Lakini walau kwa hiyo siku moja alotumia basi ameweza kuona baadhi ya viashiria vya uhalisia wa usafiri kwa njia ya Basi. Cku nyingne ajaribu na Treni ajiongezee uzoefu zaidi. Hizo ndege iko siku anga litafungwa na hakuna ndege kuruka. Je, atafanyaje?
 
Sukukataa kwa ubaya. Nilimueleza kuwa siwez kula nikiwa nasafiri tumbo alikostable..
Yeye alikua anasisitizia kuwa amepika yeye na zimekauka vzuri azitaleta shida.

Itani cost nini? Mbona akuna ubaya wowote hata ukikataa kwa kavu kavu
Kwa jamii za huku Field a.k.a. mashambani itaweza kutokea siku umekwama kwenye maeneo yao na hawatahangaika kukupa chochote kwani watasema "Huyu halagi kwa watu", "huyu anaona eti vyakula vya kwetu ni
vichafu", "huyu anadharau eti hatujui kupika", "huyu anaringa na kujiona yeye ni mstaarabu hawezi kula vyakula vyetu vya kishenzi" n.k. n.k. Njaa itabana mno.
Nitakupa mfano Hai: Huku Umasaini ndani ndani huku tunapoenda field wao hutukaribisha maziwa ya mgando ambayo kwa macho tu utaona sio salama.
Ukizingatia Kazi ya cattle vaccination inachukua muda mrefu, lazima njaa iwe imekaza, kali. Tunachofanya ni kusingizia tuko kwenye dozi na sharti la dawa ni hairuhusu kutumia maziwa. Basi kwa ukarimu huo huo watawachinjia kuku na kuchoma ili iwe ni mboga ya Ugali. Tukishakula tunashukuru na wao wanafurahia kazi tuliowafanyia. Hakuna aliyekereka.
 
Kero nyingine ni hii
 

Attachments

  • Screenshot_20261112-210535_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20261112-210535_WhatsApp.jpg
    90.2 KB · Views: 1
Namba 7 wewe ni mwanamke au mchicha mwiba?
Huyu jamaa namimi nina wasiwasi nae, kuna muda anakuwa na uhusika wa kike huwa nahisi ni mpakuliwa na kuna mmoja alikuwa wa kujifanya kujipikilisha misosi misosi full kupost makaangizi yake nae ukim-scan kiintelijensia unabaini ni "wali"
 
Unashindwa kukaza masaa 12 mwanetu, kula njiani safari ya usiku halafu masaa hayazidi 12 naonag udwanzi tu.
 
Back
Top Bottom