Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,558
- 27,524
Baada ya mabasi kuanza safari za Usiku, nimekuwa nikisafiri sana hasa kama nikikosa ndege. Mabasi hayo yana raha na karaha, hizi ni baada ya karaha;
- Jirani yangu anabdili nepi ya mtoto wa miaka 4 , kitu kinanuka balaa, safari nzima kuziba mdomo.
- Jirani ile tumefika tu Kabuku kabla ya Segera pale michungwani tukitoka dar kuelekea Arusha, akanitapikia, alikuwa amekula makande, aloo si poa.
- Konda kila saa ananiuliza kwanguvu jina langu na kituo ninachoshukia.
- Gari ina AC, watu wanaziba zile buttons, joto kali unasinzia kwa kukosa oxygen.
- Gari inasimama hotelini, chips kavu elfu 5 na mshikika mmoja elfu 2.
- Wakati tukifika hotelini, dereva anashuka fasta, wao wanatwambia kula dakika 10, wameandaliwa na wanakula kwa muda ila abiria wa mwisho kushuka hata hajafika msalani anaambiwa muda umeisha gari inaondoka.
- Kukaa siti moja na mkaka, tangu amepanda ameweka tunini twake masikioni, hata salamu hamna , masaa 8 hatujaongea eti tunafika Tengeru ananiuliza hapa ni wapi nikamwambia sijui labda ni Morogoro.
- Huyo mkaka nimekaa naye kwenye TAHMEED ya Nairobi, akapiga simu kwa mpenzi wake wanaongea zaidi ya dakika 60 kimapenzi, kuna vitu walikuwa wanaongea mpaka ninasisimka mwili .
- Konda kuuliza kituo ninachishukia kwa sauti kubwa kila mtu ajue kwetu ni Kishumundu.