Mabasi Dar yaruhusiwa kushusha vituo binafsi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, ameondoa katazo lililokuwa likizuia mabasi yaendayo mikoani kutoruhusiwa kupakia abiria au kushusha katika vituo binafsi na badala yake ameruhusu utaratibu huo kuendelea kwa sharti la kila basi kuingia ndani ya kituo kikuu cha Magufuli.

RC Makalla ametoa maamuzi hayo wakati wa kikao cha pamoja baina ya LATRA, wamiliki wa stendi binafsi na Halmashauri ya Ubungo na kubaini pasipokuwa na shaka kuwa waliotengeneza vituo binafsi walifuata taratibu na kupatiwa vibali na LATRA baada ya kukidhi vigezo.

Miongoni mwa vigezo vilivyotolewa na LATRA ili kuruhusiwa kuanzisha stendi binafsi ni pamoja na uwepo wa vyoo, sehemu ya mapumzimo kwa abiria, viburudisho na sehemu ya maegesho.

Kutokana na hilo RC Makalla ameridhia vituo binafsi vitano vilivyohakikiwa kuendelea kutoa huduma na kufungua milango kwa wamiliki wengine wanaohitaji kuwa na vituo binafsi kushirikiana na LATRA ili wapatiwe vigezo vinavyohitajika ambapo wamepewa mamlaka ya kufuta au kutoa leseni.

Aidha RC Makalla ameagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kukaa kikao mara moja na wamiliki wa stendi binafsi ili kuona njia bora ya ukusanyaji wa mapato.
 
Sasa tuache kutumia pesa nyingi kujenga stendi za mabasi,
 
Inchi inawndeshwa na kelele za mitandaoni,wanafanya madudu kisha wanasikikizia wananchi wanasemaje,wakikaa kimya basi ndy imeisha hiyo,wakilalamika ''nendeni mkaliangalie hili linalolalamikiwa na wananchi"

Hii taarifa Yule kiongozi mwenye mashavu makubwa km ameficha nyama hawezi kuifurahia kabisa

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mbona makasiriko? Una biashara ya hotel hapo mbezi, pole sana Mkuu
 
Yes my RC always shirikisha ubongo kwenye maamuzi yako, huu ni uamuzi wa busara na ningekua mimi ndio RC kituo cha mabasi cha Magufuri ningekifunga na ningerudisha kituo cha ubungo kwa wanaosafiri kutumia T1,wale wanaosafiri kwenda mikoa ya kusini mabasi yangeondokea pale mnazi mmoja
 
Machinga wameteswa sana nchi hii,hawathaminiwi,Mali zao zimeharibiwa,wameitwa kila aina ya majina mabaya.
Wamenyanganywa Mali zao mwisho wa siku wametengewa maeneo yao.....lakini wamerudi na wanauzia maeneo yao ya zamani.
swali: Je serikali huwa inakurupuka katika maamuzi ya baadhi ya mambo yenye kuhitaji umakini?

Mfano: stendi zimejengwa nchi nzima isipokuwa bukoba....ila utaratibu wa uendeshaji wa hizo stendi ni wizi,unyanganyi,vitisho na kubebeshana misalaba....why?
Hili suala Hata mjinga atalipatia...iko hivi, abiria washukie kwenye vituo vyovyote vile kulingana na eneo analoona ni sahihi then bus Hata likiwa tupu liingie stendi kuu. Just simple as that.
 
Nadhani bado wanahitaji kuumiza vichwa zaidi,kuwa na stand ya Magufuli ni moja ya njia ya kupunguza foleni zisizo za lazima katikati ya mji,kwahiyo waendelee kukuna vichwa ili kuliweka hili vizuri,maana nawaza tu kama kila kampuni ya mabasi itafanikiwa kukidhi hivyo vigezo itakuwa ni vurugu kwakweli...
 
[siyo kweli mkuu]
 
Uamuzi mzuri, ila hapo kwenye ukusanyaji mapato ndio hofu yangu ilipo, serikali/LATRA wasije kuwawekea hao jamaa kiasi kikubwa ili kuwakomoa ili waanze kurudi Stand ya Magufuli wenyewe bila kupenda.
 
Unaweza ku
Machinga wameteswa sana nchi hii,hawathaminiwi,Mali zao zimeharibiwa,wameitwa kila aina ya majina mabaya.
Wamenyanganywa Mali zao mwisho wa siku wametengewa maeneo yao.....lakini wamerudi na wanauzia maeneo yao ya zamani.
swali: Je serikali huwa inakurupuka katika maamuzi ya baadhi ya mambo yenye kuhitaji umakini?

Mfano: stendi zimejengwa nchi nzima isipokuwa bukoba....ila utaratibu wa uendeshaji wa hizo stendi ni wizi,unyanganyi,vitisho na kubebeshana misalaba....why?
Hili suala Hata mjinga atalipatia...iko hivi, abiria washukie kwenye vituo vyovyote vile kulingana na eneo analoona ni sahihi then bus Hata likiwa tupu liingie stendi kuu. Just simple as that.
Niambie Faida ya Darajs la juu Ubungo stand Sasa hivi? Walijua watahamia Mbezi wakaruhusu Ujenzi Daraj la milions Ubungo stand ya zamani
 
Mkuu mbona makasiriko? Una biashara ya hotel hapo mbezi, pole sana Mkuu
Mkuu kwani hatupaswi Kusema ukweli? Ni lazima tuonekane tumetumwa,tunatumika au tuna maslahi Fulani Lindi tukisema ukweli? Huoni Kama kuna tatizo la kiongozi mahali mkuu?
 
Sasa tuache kutumia pesa nyingi kujenga stendi za mabasi,
Usumbufu na wizi uliopo stand ya Magufuli vingefanyiwa kazi na kupunguza adha zilizopo ili kufanya watu waridhike na huduma!! Kwa Sasa stand ipo kama kusanyiko la watu wasio na busara
 
Hii ni sawa kabisa maana mtu huwezi fika dar saa 7 usiku unakaa magomeni ukashukia mbezi wakati gari inafika hadi shekilango.
 
Back
Top Bottom