LATRA: Stendi binafsi za mabasi ya mkoani siyo halali lakini zina vibali

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,119
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Amos Makalla, ameitaka LATRA imthibitishie ndani ya siku 14 kama stendi binafsi za mabasi ya mikoani ni halali. Makalla ametoa agizo hilo kufuatia malalamiko ya wafanyabiashara ndani ya Stendi Kuu ya Magufuli kulalamika kuwa stendi hiyo haina abiria.

Hata hivyo msemaji wa LATRA amesema stendi binafsi siyo halali lakini zina vibali RC Makalla alichachamaa na kumwambia asimchonganishe na waziri!

Chanzo: ITV habari
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amekitaka LATRA imthibitishie ndani ya Siku 14 kama Stendi binafsi za Mabasi ya mikoani ni halali.

Makalla ametoa agizo hilo kufuatia malalamiko yA wafanyabiashara ndani ya Stendi Kuu ya Magufuli kulalamika kuwa Stendi hiyo haina abiria

Hata hivyo msemaji wa LATRA amesema Stendi binafsi siyo halali lakini zina Vibali

RC Makalla akachachamaa na kumwambia asimchonga ishe na waziri

Source ITV habari
Kwa hiyo walisubiria RC ndio awaulize?

Wao Kazi Yao huko ofisini ni nini hasa?
 
Magari yote yakihamia kwa Magufuli inaleta kero, wafanyabiashara hawakulazimishwa kuwekeza huko.

Stendi binafsi zitaendelea kuwepo maana zinasaidia ushindani wa biashara.

Hili swala waziri alishaongea sana na likabaki kama ilivyo
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amekitaka LATRA imthibitishie ndani ya Siku 14 kama Stendi binafsi za Mabasi ya mikoani ni halali.

Makalla ametoa agizo hilo kufuatia malalamiko yA wafanyabiashara ndani ya Stendi Kuu ya Magufuli kulalamika kuwa Stendi hiyo haina abiria

Hata hivyo msemaji wa LATRA amesema Stendi binafsi siyo halali lakini zina Vibali

RC Makalla akachachamaa na kumwambia asimchonga ishe na waziri

Source ITV habari
Wasituletee ujinga wao, stand binafsi zinawapunguzia wananchi adha ambazo serikali imeshindwa kuziondoa
  1. Akili za huyu RC ni ....... kabisa
  2. Usafiri wa ndani ya jiji ni mateso makali kwa wananchi
  3. Gharama za usafiri ndani ya jiji ni mateso kwa walala hoi na hasa kipato cha chini
  4. Miundo mbinu ya usafiri wa jiji haiwasaidii watu wa kipato duni
  5. Wasihamishie lawama kwa stand binafsi, lawama ziiendee saerikali kwa kutoshirikisha mawazo ya wananchi
  6. RC afanye utafiti binafsi ni namna gani wananchi wanateseka na hali ilivyo asifanye maamuzi toka mezani
 
Viongozi wa Tanzania wanapenda sans Publicity.
Sishangai kw haya matamko kwani hawazijui adha tunazozipata abiria tutumiao mabasi.
Kuna siku (desemba) nilitafuta basi last FRESTER la Bukoba kwa dkk 30 pale Magufuli Terminal. Hii ilitokana na kiburi changu, niliombwa nikapandie Shekilango, nikasema nitapandia Mbezi. Ilikuwa balaa.
Kituo kimekuwa kero, kero, kero kero kweli kweli. Stendi binafsi ndio suluhu. Tupite pale kama ROYAL TOUR inatosha. Vyoo tulipie! Kusindikiza mgeni tulipie! Abiria wa Dodoma, Moro, Kilosa, Tanga mchana lazima ulipie kuingia ndani. Stendi imejaa dhuluma, wizi na ubadhirifu.
Abiria anatoka Nduli (Iringa) eti akapandie gari Igumbilo wakti anaweza akapanda gari Gangilonga(ALSAEDY) au TFA (ABC) si ukichaa huo. Yaani nitoke Kigamboni/Tabata Kisukuru niende Mbezi wakati gari inawezekana kupandia Shekilango/Manzese.
Leo nimepanda BM wanatangaza route ya Dodoma-Kigamboni. Nimecheka sana, wakati jamaa wanapita na nguo zao za kijani pale Magufuli kukagua sijui nini?
 
Stebd ya magufuli haitoshelezi mabasi yote ya mkoani.
Ikiwa lengi ni kukusanya kodi bora hivyo vituo binafsi virsmishwe na ile kodi waliyopaswa kulipa magufuli stand wailipe.
Huko stand binafsi kuna wafanyabiashara pia.

Asubuhi kuna usumbufu mkubwa sana magufuli stand.
Basi za saa12 zinachelewa hadi 12.30 mnarudisha nyuma maendeleo
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amekitaka LATRA imthibitishie ndani ya Siku 14 kama Stendi binafsi za Mabasi ya mikoani ni halali.

Makalla ametoa agizo hilo kufuatia malalamiko yA wafanyabiashara ndani ya Stendi Kuu ya Magufuli kulalamika kuwa Stendi hiyo haina abiria

Hata hivyo msemaji wa LATRA amesema Stendi binafsi siyo halali lakini zina Vibali

RC Makalla akachachamaa na kumwambia asimchonga ishe na waziri

Source ITV habari
Hivi Mkuu wa Mkoa wa Dar na Wakuu wengine wa Mikoa wanataka wananchi wapate taabu kwenda kwenye vituo hivyo nje ya miji ili tu wafanyabiashara wa Stand hizo wapate faida kutokana na hasara wanayosababisha kwa kuweka vituo hivyo nje ya miji!? Ina maana hii hekima ya CCM haijabaini kuwa gharama ya usafiri kutoka Stendi ya Magufuli mpaka Kariakoo kama una mzigo inaweza kuzidi nauli ya bus kutoka Stendi hiyo mpaka Arusha, Dodoma au Iringa, licha ya usumbufu wa kuteremsha na kupakia mizigo upya pale Stendi! Hao abiria ambao wanaishi karibu na Stendi ambao huteremkia kwenye hizo Stendi hawatoshi kuwajaza mapesa wafanya biashara pendwa mpaka Wakuu wa Mikoa hiyo wanataka kuwafurahisha zaidi hao pendwa na wasafiri watakaoathirika kurundwa hapo Stendi na kuanza upya safari ya mjini hawawahusu Wakuu wa Mikoa!!Kwani LATRA hawahusiki na staha ya mlaji/msafiri!! au Wakuu wa Mikoa hawajasoma sheria zinazounda hizo mamlaka za udhibiti kwamba zina Charter ya kumtetea mlaji!? Huu ni uongozi gani? Poleni Watanzania.

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
 
Huu ni unafiki wa kiwango cha sgr,
Milori imejazana kariakoo anashindwa kuiondoa sasa anataka kuondoa mabasi yaliyopo inje ya mji?
Hapa tumepigwa na kitu kizito hakuna mkuu wa mkoa wala wilaya wote mabomu tu

Daslamu ni kama haina Serikali
Kila mwizi anaiba tu
 
Back
Top Bottom