Mabadiliko makubwa yaja ...... Gazeti la RAI

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
803
Nimeona kwenye habari za magazetini kupitia Channel 10 ... Gazeti la RAI linadai kwamba mabadiliko makubwa ya uongozi serikalini yanakuja na yatafanyika mara baada ya Uchaguzi wa CCM ambao utafanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.

Kwa kuzingatia kwamba gazeti hili linamilikiwa na mdau wa wana mtandao, kunaweza kuwa na ukweli wowote kwenye hii habari? Kwa wale walio na uwezo wa kunusa tupasheni basi undani wa hayo mabadiliko, ili mradi isije ikawa ni udaku!
 
Udaku tupu na kutaka kutoa giriba kwa waTZ, hawa jamaa wameweka kichwa cha habari kwa ajili ya kuuzia gazeti lao, wanajua ni kitu gani waTZ wanakiangalia sasa hivi. Huyu RA unategemea atamshauri JK kisha akaandike au SR anaweza kufanya hicho.
 
Nimeona kwenye habari za magazetini kupitia Channel 10 ... Gazeti la RAI linadai kwamba mabadiliko makubwa ya uongozi serikalini yanakuja na yatafanyika mara baada ya Uchaguzi wa CCM ambao utafanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.

Kwa kuzingatia kwamba gazeti hili linamilikiwa na mdau wa wana mtandao, kunaweza kuwa na ukweli wowote kwenye hii habari? Kwa wale walio na uwezo wa kunusa tupasheni basi undani wa hayo mabadiliko, ili mradi isije ikawa ni udaku!!!!

Ukweli hupo, kama mwanamageuzi amesema kwamba tutegemea kuanguka kwa Lowassa, nadahni hii itakuwa ni stage kubwa katika kupunguza mafisadi,

Mie nadhani ungeanzisha thread tumsaidie Rais kupanga safu
 
Haya mabadiliko makubwa ni rumors na waliandika kwanza katika Mwanahalisi! Ni gazeti moja nzuri sana kwa wale ambao hawaifahamu! Lakini bahati mbaya it is speculation, not reality!

Also, I think that unless Bwana Mkubwa ataamua kuangalia nje ya 'mtandao' wake, hatapata maendeleo. Akitaka kukomboa uhai wa CCM na kuzuia kumeguka kwa chama na also kwa ajili ya kuinusuru nchi, ni lazima aachane na wale ambao wamemshauri mpaka sasa. Walichomsaidia ni kupata kura kwa njia chafu na kuutwa urais bila mkakati.

But I think the best solution ni kusubiri 2010 na kuiweka madarakani upinzani ili tupate a breath of fresh air! Then CCM inaweza ikajaribu kujisafisha. Until then tunadanganywa na tunapata firefighting tu, bila strategy!
 
Hata kama hayo mabadiliko yanakuja sioni kama kutakuwa na tofauti yoyote, they are all cut from the same cloth sana sana JK atawabadilisha na kuwasogeza sogeza hao maswahiba wake ili waendelee kujimwaga na kutafuna hii nchi kwa style nyingine.

We need fresh blood watu ambao wapo kufanya kazi sio ambao wamepewa zawadi ya madaraka na wanajua kabisa they can do anything they want and no one can ever touch them.
 
mabadiliko ya uongozi kwenye gazeti lenyewe la rai au nchi? maana nnaona kwenye gazeti ndio nimesikia wengine wameanzisha gazeti la raia mwema.

pengine walimaanisha hilo
 
Hawa wanamaanisha ama ni zile zile story za kutuhadaa kama kawaida yao?

Nimeacha kulisoma rai muda sasa kwani hawaandiki kwa nia njema.
 
Kama alivyosema mtu wa pwani kama ni mabadiliko basi yafanyike huko kwenye uongozi wa gazeti la Rai kwanza....
 
ukweli hupo,kama mwanamageuzi amesema kwamba tutegemea kuanguka kwa Lowassa,nadahni hii itakuwa ni stage kubwa katika kupunguza mafisadi,

mie nadhani ungeanzisha thread tumsaidie Rais kupanga safu

hilo litawezekana iwapo watu wnataka maendeleo kwa taifa na sio vyama vya siasa, na dua za wengi ni kuona rais anafail, sasa sijui itakuwaje !

Lakini unachosema ni kweli kabisa, kwamba rais anahitaji ushauri juu ya upangaji upya wa safu za viongozi na watendaji wakuu wa serikali maana sasa hivi kweli mabadiriko yanahitajika kwani its not too late !
 
Nimeona kwenye habari za magazetini kupitia Channel 10 ... Gazeti la RAI linadai kwamba mabadiliko makubwa ya uongozi serikalini yanakuja na yatafanyika mara baada ya Uchaguzi wa CCM ambao utafanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.

Kwa kuzingatia kwamba gazeti hili linamilikiwa na mdau wa wana mtandao, kunaweza kuwa na ukweli wowote kwenye hii habari? Kwa wale walio na uwezo wa kunusa tupasheni basi undani wa hayo mabadiliko, ili mradi isije ikawa ni udaku!!!!

Hili la mabadiliko lilishaonekana siku nyingi na limesababishwa na wananchi kukosa imani na timu nzima ya Muungwana. Hivyo kurudisha imani hiyo inabidi aipange timu yake upya na wale wote ambao si watendaji wazuri au wana sifa za ufisadi, ula rushwa, kusaini mikataba mibovu na kujilimbikizia mali inabidi wawekwe pembeni na kuingia na watu wapya kabisa.

Kwa maoni yangu hii ni karata ya mwisho ya Kikwete kurudisha imani ya uongozi wake kwa Watanzania akiicheza vibaya basi atakuwa ni Rais wa kwanza Tanzania kuongoza kwa awamu moja na pia kuchangia kwa kiasi kikubwa kwa ushindi wa kishindo wa wapinzani katika uchaguzi mkuu wa 2010, kama CCM haitamua kufanya wizi wa hali ya juu katika uchaguzi huo.
 
Well said Bubu.

Ni njia pekee iliyobaki kama bado anataka kuendelea na 2010.
Na hao wapya watakaoingia wawe na maagizo maalum. Kazi yao ni moja tu, kumrudishia heshima na serikali yake kwa wananchi; lengo likiwa ni kupata ushindi wa aina yoyote hapo 2010, hata kama utakuwa ni wa kuiba kura. Baada ya hapo hao viongozi wapya wanao uhuru wa kufisadi watakavyo, maadam hapatakuwa na kwenda kuwapigia tena wananchi magoti akiomba kura zao. Sidhani kuwa bado anayo malengo na matumaini ya kuweka 'legacy' ya uongozi.

Assuming, amepata fundisho mhimu katika hii miaka miwili ya uongozi wake, na yeye mwenyewe ajitahidi kujirekebisha.

Ikitegemea pia subira walizonazo wananchi; na sana sana ushawishi utakaotolewa na waShindani. Huko kwenye uShindani wakipatikana viongozi wenye msimamo utakaoweza kueleweka na wananchi vizuri, hiyo 2010 inaweza kuwa ndoto nzito kutokana na historia mbaya wananchi waliyoishuhudia kiutawala sio katika serikali tu, bali hata katika chama cha CCM katika miaka hii miwili.

Pengine wananchi wataanza kujiuliza: mbona wenzetu wakenya wanabadilisha serikali na chama? Kwa nini sisi tusiweze. Hapo patakuwa na somo zito ODM wakishachukua madaraka kenya.
 
Asubuhi nili-post habari nusu, na sasa nimeipata habari hiyo. Maybe watu wenye uwezo wa kusoma between lines wanaweza kuambua kitu kwenye hiyo habari iliyoandikwa na gazeti la Rai. Ama inawezekana ikawa ni speculation tu za waandishi wa habari. Swali la msingi ni kwamba je hao waliotuhumiwa ufisadi na rushwa wamechunguzwa na vyombo vya dola na JK akaridhika na report kwamba kweli hao watuhumiwa ni mafisadi? Bado ninaona kuna ombwe kubwa kwenye hizi habari na JK yuko kwenye mtego mbaya sana ambao ninamuonea huruma. Maana kama kuna watakaoonewa au watakaoondolewa na huku wakijua kuna wengine wameachwa kwenye cabinet na ni wachafu basi tutaendelea kushuhudia kuvuja kwa documents za serikali na kujionea mengi ya ajabu ambayo huko nyuma ilikuwa ni nadra kuyaona.

Just in case baadhi ya watuhumiwa wataachwa na wengine kutolewa kafara, basi nadharia ya vijana wa kijiweni kwamba "ukimwaga ugali basi mimi nitamwaga mboga ili wote tusile halafu tuone nani mjanja". Huu ni mtihani mkubwa, na hapa ndipo JK anatakiwa kuonyesha umakini wake na ukomavu wake. Ni ukweli usiopingika kwamba wengi wetu ni ma-opportunist, tunapiga kelele za ufisadi kwa kuwa hatujapewa opportunity ya kula, lakini siku tukipewa ulaji tutajitahidi kwa kadri tunavyoweza ili kujilimbikizia as much as possible, na baada ya hapo, na wale tuliokuwa tukionekana ni wasafi, tutakuwa wachafu!
 
Mabadiliko makubwa ya uongozi yaja

na mwandishi wetu


Mabadiliko makubwa ya kiuongozi yanatarajiwa ndani ya Serikali mara baada ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi kukamilika ngazi ya taifa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa Novemba hii.

Vyanzo vyetu ndani ya serikali na ndani ya chama chenyewe, zinaonyesha kwamba Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajia kufanya mabadiliko makubwa kwenye safu za uongozi akianzia kwenye sekretarieti ya chama na kuishia serikalini.

Habari kutoka kwa watu walio karibu na uongozi, zinaonyesha kwamba hadi sasa, Rais Kikwete hajaridhishwa na hali halisi ya kiuongozi.

“Kuna pengo kubwa kati ya mawazo na matarajio ya mwenyekiti na hali halisi ya kiuongozi ilivyo. Kwa hiyo kuna uwezekano wa mabadiliko tangu kwenye sekretarieti ambayo ndiyo humuwezesha mwenyekiti kufanya kazi zake kwa ufanisi na kisha mabadiliko hayo kusambaa hadi serikalini,”chanzo chetu cha habari kilieleza.

Kwa upande wa serikali hasa katika Baraza la Mawaziri, habari hizo zinaeleza kuwa baada ya mambo mengi kutokea na baada ya kujipa muda wa miaka miwili ya kuwapima watendaji wake, Rais Kikwete anatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa siyo katika sura tu bali na mwelekeo halisi wa serikali yake.

Kumekuwapo malalamiko ya hapa na pale kuhusu utendaji wa baadhi ya mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya. Hata hivyo, Rais Kikwete amekuwa mkimya kuhusu malalamiko hayo.

Chanzo chetu cha habari kimeliambia Rai kwamba Rais alisubiri kujiimarisha kwenye chama ndipo aweze kuwa na timu ambayo itafanya kazi kwa mujibu wa matarajio yake.

Kwa upande wa chama, kwa sasa mazungumzo yanayotawala kwenye chama hicho ni uteuzi wa Makamu Mwenyekiti; nafasi ambayo kwa sasa inashikiriwa na John Samwel Malecela. Kiongozi huyo hajasema kama angependelea kuendelea na nafasi hiyo au la. Kwa mujibu wa utaratibu wa CCM, baada ya kukamilisha safu za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwenyekiti hutangaza jina la mtu ambaye angependelea awe makamu wake.

Desturi hizo za uchaguzi zinaonyesha kwamba haijawahi kutokea wajumbe wakalikataa jina la mtu aliyependekezwa na mwenyekiti kuwa makamu wake.

CCM ina makamu wawili. Mwingine ni lazima atoke upande wa Zanzibar ambaye kwa sasa ni Amani Abeid Karume.

Wachunguzi wa mambo ya kisiasa, wanaeleza kwamba kuna uwezekano mkubwa Rais Kikwete akafanya kama alivyofanya mwenzake wa China Hu Jintao ambaye baada ya kuchoshwa na tuhuma za rushwa, aliamua kufanya mabadiliko makubwa ambayo yamesababisha kuondolewa madarakani kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama cha Kikomunisti cha nchi hiyo, Chen Liangyu ambaye anatuhumiwa kwa ubadhilifu katika mpango wa pensheni.

Wachambuzi wa mambo wanasema Kikwete anaweza kabisa kuchukua mfano wa kiongozi wa China ambaye baada ya kuchoshwa na rushwa ndani ya chama, ameamua kufanya kile kilichowashinda waliomtangulia. Katika uchaguzi wa ngazi za wilaya na mikoa, Kikwete aliagiza vyombo vya usalama vya dola kuingia katika kumbi za mikutano za CCM na kuwashughulikia watoa na wapokea rushwa.

Hata hivyo, hatua hiyo ilisababisha malalamiko makubwa kutoka kwa baadhi ya wahafidhina ndani ya chama hicho jambo lililomfanya Kikwete kuitisha mkutano wa dharura wa Kamati Kuu na kusisitiza nia yake ya kupambana na ufisadi kuanzia kwenye chama.

Kikwete aliwahi kukaririwa akisema kuwa huwezi kuwa na chama kinachokumbatia rushwa, ukapambana na rushwa ndani ya serikali. Ni kutokana na mkakati huo wa Kikwete, uchaguzi wa CCM ya mikoa umetoa sura mpya za uongozi.

Pamoja na matarajio ya mabadiliko hasa ndani ya chama, baadhi ya wanachama wa CCM waliozungumza na Rai lakini kwa masharti ya kutotajwa majina, wameeleza kwamba wangehitaji mabadiliko siyo ya sura bali ya kiitikadi.

Mmoja wa waasisi wa chama hicho, Peter Kisumo, alisema matarajio yake kuona siyo mabadiliko ya sura bali mabadiliko katika itikadi. “Ni lazima chama kijifikishe mahali ambapo kitakuwa na sauti ya kuzungumza na watu wakakisikiliza,” alisema mzee Kisumo. Uchaguzi wa wajumbe 85 wa kukamilisha nafasi za Halmashauri Kuu ya CCM ndiyo utatoa mwanga na mwelekeo wa nani atakuwa nani katika chama hicho.

Kwa sasa kinyang’anyiro kinachotupiwa macho mawili ni cha wajumbe 20 kupitia kundi la Bara.

Kundi hilo lenye jumla ya wagombea 59 lina majina mazito katika chama hicho na serikalini na mchuano wao unatarajiwa kuwa mkali.

Kundi hilo lina majina kama vile Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu wa sasa, Edward Lowassa, Naibu Katibu Mkuu, Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, Katibu Mkuu wa sasa, Yusuph Makamba, Naibu Katibu Mkuu, Jaka Mwambi, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Emmanuel Mwambulukutu pamoja na orodha ndefu ya mawaziri, naibu mawaziri pamoja na wabunge mashuhuri. Wagombea wanaopitia kundi hilo ni pamoja na Tarimba Abbas, Filbert Bayi, Shy-Rose Bhanji, Enock Chambiri, John Chiligati, Siwajibu Clavery, Dk. David Mathayo, Said Masoud Fundikira, Christopher Ghachuma, Arbogast Godogodo, David Holela, Jared Kadunga, Charles Kagonji, Dk. Deodorus Kamala, Constantine Kanyasu, Prof. Juma Kapuya na Alhaji Said Kilahama.

Wengine katika kundi hilo ni pamoja na Haidah Kilua, Abdulrahman Kinana, Lukas Kisasa, John Komba, Edward Lowassa, William Lukuvi, Pascal Mabiti, Dk. Milton Makongoro Mahanga, Amos Makala, Yusuf Makamba, Novatus Makunga, na Mohamed Yakub Mamoon.

Katika kundi hilo pia wamo Wilson Masilingi, Bernard Membe, Maurus Mhimbira, Mohamed Mkumbwa, Dk. James Msekela, Dk. Ibarhim Msengi, Jackson Msome, Prof. Idrisa Mtulia, Prof David Mwakyusa, Captain Jaka Mwambi, Emmanuel Mwambulukutu, Aggrey Mwanri, Abeid Mwinyimusa, na Job Ndugai.

Wengine ni William Ngereja, Kingunge Ngombale-Mwiru, Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, Dk. Baanda Salim, Salim Khamis Salim, Abdul Adam Sapi, Isidore Shirima, George Simbachamwene, Amos Siyantemi, Fredrick Sumaye, Dk. Hashim Twaakyondo, Frank Uhaula, Prof. Samwel Wangwe, Stephen Wasira, na Nicholaus Mateso Zacharia.

Source: RAI
 
... Ni ukweli usiopingika kwamba wengi wetu ni ma-opportunist, tunapiga kelele za ufisadi kwa kuwa hatujapewa opportunity ya kula, lakini siku tukipewa ulaji tutajitahidi kwa kadri tunavyoweza ili kujilimbikizia as much as possible na baada ya hapo na wale tuliokuwa tukionekana ni wasafi tutakuwa wachafu!!!

Keil,

Unatumia heading ambayo inaonyesha vingine lakini kilichomo ndani ni kingine mkuu. Mimi nilisoma hii nikadhani gazeti la rai linafanyiwa marekebisho? Nilisoma zile positive heading za JK na EL kuja kusoma ndani kumbe negatives kibao.

Naona hapa unatoa hukumu kubwa sana, yani watu wengi ni wafisadi ila wanapiga kelele kukemea ufisadi ili wapewe kula na wao wawe mafisadi? au kila mtu duniani ni opportunistic hivyo hakuna mwema hata mmoja!

Basi dunia hii imekwisha kama ndio hivyo.
 
Back
Top Bottom