Mabadiliko makubwa yanakuja duniani

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
805
810
MABADILIKO MAKUBWA YANAKUJA DUNIANI:
Hivi sasa ukiwa makini na mfuatiliaji wa habari za kitaifa na kimataifa,utagundua haraka sana kwamba dunia inabadilika, na unabii unatimia, kwa haraka sana!

Nchi ambazo ni maarufu na zenye nguvu za kiuchumi hivi sasa,yaani wale G7,watapotea na kufifia muda siyo mrefu.Sababu kubwa ni kwamba unabii unatimia.Biblia imetaja kabisa nchi za mashariki zitakuwa na nguvu kubwa nyakati za mwisho

Afrika na watu wake wameamka, wanaanza kujitambua na kuelewa umuhimu wa kujitegemea.Marais wa nchi nyingi sana hivi sasa wameamua kupaza sauti na kutetea nchi zao.Muda siyo mrefu,nchi za G7 zinaangukia pua.

BRICS ni kifupisho cha Brazil, Russia,India, China na South Africa.Hizi ni nchi ambazo zinainuka kiuchumi duniani,zina nguvu kubwa na zimetambua zinaweza kufanya biashara kati yao bila kutegemea US$.Hizi ni habari njema.

Mwanauchumi maarufu Jim O'Neill wa shirika la Goldman Sachs alitabiri mnamo mwaka 2001,kwamba hizi nchi zitakuwa na nguvu kubwa na kuuteka dunia kiuchumi itakapotimia mwaka 2050.Lakini naona huu ukweli ukitimia kabla ya mwaka 2050!

Tayari kuna nchi takriban 30 zinaonyesha nia ya kujiunga na umoja huo,hii ikiwa ni ishara kwamba nchi nyingi zimechoka kuonewa na kunyanyaswa na G7.Yaani BRICS itabadilika kabisa na kuwa muungano mkubwa sana wa nchi nyingi sana. Naona hata jina litabadilishwa(angalia picha).

Tayari,hizi nchi za BRICS zimeamua kuanzisha benki yao,kufanya biashara kati yao,kuanzisha sarafi yao na kuhakikisha wananchi wao wanaweza kutembelea nchi zao bila masharti magumu. Hii itadhoofisha kabisa dola ya kimarekani pamoja na Euro kwenye soko la kimataifa.

Nahisi hili shirika la BRICS litakuwa na nguvu kubwa pia za kijeshi,hii itakuwa tishio kubwa sana kwa nchi nyingi za kimagharibi.Watakuwa na uwezo wa kusaidiana kijeshi, kijamii, kiuchumi na hata kielimu.

Naomba tusubirie kikao cha mwezi wa nane 2024,huko SA,nahisi mabadiliko makubwa yanakuja duniani....itakapotokea mtakumbuka haya.

Tatizo kubwa ni kwamba BRICS inakuja wakati ambapo nchi za Afrika baado hazijaungana....itakuwa pigo kwa upande mwingine,na hivyo kudhoofisha Afrika!

Ni maoni yangu.

Watch this space.
#BRICS is powerful.
 
Jambo hilo sio jipya wala hakuna unabii apo ni jambo la kawaida ,rejea nchi kama iran( uajemi) , Italy, England, uturuki, misri , ujeruman , Spain ureno , zote hizo zilishawah kuwa super power zikadondoka.
 
Hawajabuni Jin azuri.mfano nchi zikionhozeka na kufikia 50 je na jina litabaldlika liongeseke hizo herufi za jinanla nchi?
 
Pamenoga brics.dollar kulee.
Screenshot_20240302-131402.png
Screenshot_20231209-232805.png
 
Back
Top Bottom