Maaskofu, Nchimbi yuko wapi?

Maaskofu, Nchimbi yuko wapi?

Nchimbi amekuwa Muumini wenu miaka yote na kutokana na Vyeo alivyokuwa kuwa navyo akifika Kanisani mlikuwa mntambua kipekee hivyo mlikuwa mnampa viti maalumu vya kukaa pengine pale mbele kabisa.

Kama mlimtambua kwa cheo chake, kwa nini sasa haji Kanisani kwenu na nyie mmenyamaza kimya?
Tukiachana na Nchimbi, Kanisa linatakiwa kuwapigania wanaodhulumiwa kila siku na kila mahali. Kwa upande wa TEC kumekuwa na kawaida ya kutoa matamko kupinga udhalimu. Ni jambo jema lakini matamko yamekuwa yakitolewa mara moja tu, baada ya hapo ni kimya kikuu. Je, ni sahihi kutoa tamko mara moja tu wakati dhuluma bado zinaendelea? Mimi nadhani matamko yatolewe kwa wingi na kwa uzito tofauti tofauti kulingana na hali ilivyo.

Huwezi kula chakula mara moja tu wakati njaa bado inaendelea. Matamko ya kupinga dhuluma yanatakiwa kutolewa kila siku na kila Kanisa kuanzia kwenye Jumuiya ndogo ndogo, vigangoni, parokiani na Jimboni.

Maaskofu mkikaa kimya huku dhuluma zikiendelea hamvitendei haki vyeo vyenu. Ipo siku waamini wataona hakuna sababu ya kutoa ZAKA, SADAKA na michango mingine huko Makanisani.
Mbona kwa Mzee Kibao hatukusikia mkimuulizia BAKWATA? Chadema mnacheza mchezo wa kijinga na wa kipumbavu halafu mnafikiri mnafanya siasa.

Dawa yenu ipo jikoni. Mtainywa muda si mrefu!
 
Unamkusudia nani hapa mkuu?
Samahani Mkuu nimechanganya mafaili hapa nilidhani wewe ni mleta mada !
Uliyoyaeleza kuhusu intellectual offloading ni kweli kabisa kila mtu analalamika kwamba wengine hawajafanya hiki ama kile ilihali mlalamikaji yeye mwenyewe anakuwa bado hajachukua hatua yeyote zaidi ya kulalamika tu !
 
Samahani Mkuu nimechanganya mafaili hapa nilidhani wewe ni mleta mada !
Uliyoyaeleza kuhusu intellectual offloading ni kweli kabisa kila mtu analalamika kwamba wengine hawajafanya hiki ama kile ilihali mlalamikaji yeye mwenyewe anakuwa bado hajachukua hatua yeyote zaidi ya kulalamika tu !
Kitu cha msingi hapa ilikuwa ni kuanzisha hata kesi tu ya kumtoa nyoka pangoni.

Ila wengine hatuna hata standing ya kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom