umeongea mambo mengi ya msingi.
hivi wakati Nchimbi akiwa anagombea kwenye ugombea mwenza hakuwa anajua shida ya ule uchafuzi? Ona sasa kimemlamba
Hapa kuna mambo mawili ambayo yanatatanisha sana, na tusipokuwa makini yanaweza kutuvuruga sana kwa kuanguka kwenye mtego wa false dichotomy logical fallacy.
False dichotomy logical fallacy, kwa wale wasioijua vizuri pengine kwa jina hilo, hutokea pale unapopewa uchaguzi wa kuchagua kitu A au B, wakati hakuna ulazima wa kuchagua, unaweza kuchukua vyote viwili bila kutengeneza contradiction yoyote.
Kwa hiyo, ni muhimu kuanza kwa kuweka vitu clear.
1. Kwanza, Nchimbi si shujaa wa mageuzi Tanzania kama ambavyo baadhi ya watu wanataka kumfanya. Ana mapungugu yake mengi, ni m CCM wa siku nyingi, kama angetaka kuwa a radical revolutionary angeweza kuanika mengi ya CCM. Kwa hiyo, angalau kwangu mimi, jitihada zozote za kumtafuta Nchimbi ( na hata Humphrey Polepole) ni jitihada za kutafuta ukweli, na si za kumtafuta shujaa wetu wa mageuzi.
Katika mapambano ya kutaguta haki, kuna mtego wa kuingia kwenye vita za kuwakuza watu, team Magufuli vs team Samia, team Nchimbi vs team Samia, na ujinga mwingi kama huo. Ni muhimu kukumbuka kuwa hawa wote ni CCM na hata Nchimbi angekuwa rais pengine angejua kuuma na kupuliza zaidi, lakini bado angekuwa na mizengwe ya CCM.
Tena inawezekana mtu anayejua kuuma na kupuliza ndiye mbaya zaidi ya anayeuma tu, kwa sababu anayeuma tu (Samia) utastuka, huyu anayejua kuuma na kupuliza (Nchimbi) unaweza kujidanganya kwamba ni mwenzako anakujali, kumbe anakuchota tu.
2. Pili, baada ya kusema yote hayo ya juu, watu wanaojali haki, wanaojali kuujua ukweli, wanaojali logical consistency, kwa sasa, ni muhimu wadai kujua Nchimbi yuko wapi. Ndiyo maana unaona hata wakili Msomi Lissu kataja hili.Kwanza kwa sababu watu wote wanastahili haki. Yani hata jambazi likitekwa na kupotea bado linastahili kutafutwa, lipatikane, ijulikane halijauawa bila kushitakiwa, na hata kama lina mashitaka, lishitakiwe na kuhukumiwa mahakamani.
Kwa hiyo bila kujali u CCM wake na matatizo yake yote, Nchimbi bado ni raia wa Tanzania na anastahili haki za kiraia, ikiwapo haki ya kuishi, na kwa sasa hatuna hakika kama anaitumia hii haki ya kuishi au kashatangulizwa kuuawa.
Lakini pia, Nchimbi anatakiwa aonekane si tu kwa kulindwa yeye haki zake za kiraia, bali pia kutumiza haki nyingine za wananchi, wananchi ambao kwa mujibu wa tume ya uchaguzi wamemchagua Nchimbi kuwa Makamu wa Rais kwa asilimia takriban 98. In theory at least.
Wananchi hawa wana haki ya kikatiba kujua kwa undani kwa nini Nchimbi kajiuzulu, na kama kajiuzulu kweli. Wana haki ya kuhoji kama barua iliyosambaa kaandika Nchimbi kweli, na kama kaandika Nchimbi kweli, wana haki ya kuhoji, kwa nini Nchimbi aliona sawa kujiuzulu kwa sababu mtu mmoja tu hakumtaka kuwa Makamu wa Rais, wakati mamilioni ya watu wamempigia kura yeye kuwa Makamu wa Rais.
Hapa kuna swali la muhimu ambalo halijachambuliwa.
Kwa sababu Makamu wa Rais na Rais wote wanachaguliwa kwa kura moja ile ile kwenye tiketi moja, Makamu wa Rais anawajibika kwa nani? Kwa mamilioni ya Watanzania waliomchagua, au kwa Rais anayemsaidia?
Na hata tukisema kuwa Makamu wa Rais anawajibika kwa Rais, Watanzania walimpitisha tu kuwa Makamu wa Rais, msaidizi wa Rais, je, Watanzania hao, kwa sababu in principle ndio waliomchagua Makamu wa Rais, hawana haki ya angalau kupata maelezo ya kina kuhusu sababu za Makamu wa Rais kujiuzulu, zaidi ya kusema Rais hakumtaka tu? Watanzania hawa hawapewi hata heshima ya kuagwa na mtu waliyemchagua kuwa Makamu wa Rais, anaondolewa kwa kificho hivi kwa nini?
Kujibu swali lako, Nchimbi ni m CCM, alikuwa anajua uchafuzi wote, na pengine alikuwa na ndoto za kuubadilisha mfumo kutoka ndani akazidiwa nguvu, hatujui. Pengine hii ilikuwa ni power struggle yao tu ndani ya CCM, hakujali sana mambo makubwa mengi, hatujui.
Lakini, yote hayo hayaondoi ukweli kuwa tunahitaji kujua ukweli kamili, tunahitaji kuhakikisha Nchimbi yuko salama kama raia yeyote mwenye haki ya kuishi, tunahitaji Nchimbi ajitokeze hata tuweze kumuhoji na kuujua ukweli zaidi na hata yeye mwenyewe kumuwekea uwajibikaji zaidi.
Zaidi ya yote, tunahitaji kuhakikisha kuwa serikali inaposema Makamu wa Rais kajiuzulu, basi kajiuzulu kweli na hajauawa.
Hapa hakuna ucjaguzi wa kusema A Nchimbi ni m CCM jambazi tumpotezee au B Nchimbi ni Mtanzania anayestahili haki ya kuishi na ana wajibu wa kujielezea na jivyo tumtagute apatikane.
Kwa sababu, hata m CCM jambazi bado ni raia mwenye haki ya kuishi hatakiwi kupotezwa tu na zaidi tunataka kujua kama yu hai, kama yu hai tunamtaka ajitokeze ana maswali ya kujibu.