Maandamano ya wananchi kumuunga mkono Spika Ndugai

Maandamano ya wananchi kumuunga mkono Spika Ndugai

Shida kubwa ilianzia kwenu kweny ushabiki wa kila alichofanya Magufuli. Amekopa trilion 29 ndani ya miezi 64, hakuna alienyanyua mdomo, miradi iliyojengwa inaendana na hyo fedha? Kuna uchumi gani Tanzania wa kusema mtamalizia miradi, mlipe mishahara na gharama zote za utawala kwa kutegemea fedha za ndani? Kwanini mkopo ule uliopangiwa allocations ndani ya Bunge chini ya Ndugai tena mkopo wa Mashart nafuu uwe ni shida hata mtu aufanyie siasa na dhihaka?

Job hakuna alipokosea kutoa maoni kwa mtazamo wake. Alikuwa akifanya Siasa huku amejisahaulisha kuwa CCM haipingani na Mwenyekiti. Makandkando yake yote ya kumnanga Mwenyekiti na kujidai hawako tayar kuongizwa na mwanamke yalikuwa yakufahamika. Amefanya Siasa na amefanyiwa siasa.

Yapo ya kuandamana na mlishindwa kuandamana. Mtakuja kuandama kweny hili ambalo wananchi wanaimbishwa kuwa mkopo umewajengeeni kadha wa kadha?
Magufuli hajakopa tsh tr 29 ni uongo leta source ya hiyo fact. Kaacha deni la taifa ni tsh tr 56. Leo ni tsh tr 70 miezi nane. Samia kakopa tr 14 miezi nane na tr 7 zinakuja. Kufika Mwezi march amalize mwaka atakua kakopa tr 21 kwa mwaka.

Chanzo changu ni press ya Mh Gwajima
 
Ok . Nimemjibu jibu hilo sababu siwezi kuji risk kisa kuandamana kwaajili ya Ndugai kwa hoja zake zisizo na mashiko tena alifanya makusudi akijua nn anamaanisha imeshakula kwake.
Sasa mm nikavunjwe miguu wakati huo yeye katulia anakula pesa zake alizochuma kwa raha zake.
Ngoja tukuelimishe inshu sio Ndugai bali inshu nini maana ya alichofanyiwa Ndugai ? kinachopingwa ni ile hali rais kuwa kiziwi hataki ashauliwe yaani anatuingiza kwenye mfumo wa ufalme akiamka anajiamulia ajisikiavyo hilo ndo kosa kubwa , amini nina kuambia leo kafanyiwa Ndugai ila tabia inakomaa hapa tunapinga huu ukandamizaji wa uhuru wa maoni , sijaona kosa la Ndugai maana yy ni mbunge na pia ni raia km ww so ana haki ya kutoa mitizamo yake mahala popote pale
 
Kwa ufupi ccm mpaka ije itoke madarakani ndipo tunaweza kusema tupo huru kwa ukamilifu.
 
Kwahiyo Mama samia ndio rais wa kwanza kukopa ? Wanafakii nyie
Kosa lake Ni kuweka wazi kuwa amekopa pesa na zitafanyiwa nini ? Tena mkopo hauna riba na ndio mkopo mzuri kuliko yote iliyowahi kukopwa.
Nyie wanyonge Mshazoea uongo mtamu eeh

Yes trillion 70 ,ila deni Ni stahimilivu na tunasifa za kukopesheka kwahiyo hapa Ni mwendo wa kukopa tu Kila inapobidi ili mradi tuna mikakati

Kuhusu kutembeza bakuli ,Ni bora mtembeza bakuli yuko real, Sasa mtangulizi wake anatuambia tunajenga kwa pesa zetu kumbe anachukua mikopo ya kibiashara kimya kimya tena taarifa zinasema yeye ndio kavunja records kwa mikopo.
Kipindi cha magu mkaufyata sijui mlikua mmefunikwa Kwenye chungu wanafiki nyie mnakuja kumtolea povuu mama ,mshindwe na mlegee
Akili yako ni fupi so kama yy sio wakwanza , anavyoongezea hayo madeni atakuja kulipa nan ? Ndo maana ya Ndugai , tunadaiwa deni kubwa na limetuelemea ila bado tunaenda kukopa , unahis nini hatima yakee?
 
Ngoja tukuelimishe inshu sio Ndugai bali inshu nini maana ya alichofanyiwa Ndugai ? kinachopingwa ni ile hali rais kuwa kiziwi hataki ashauliwe yaani anatuingiza kwenye mfumo wa ufalme akiamka anajiamulia ajisikiavyo hilo ndo kosa kubwa , amini nina kuambia leo kafanyiwa Ndugai ila tabia inakomaa hapa tunapinga huu ukandamizaji wa uhuru wa maoni , sijaona kosa la Ndugai maana yy ni mbunge na pia ni raia km ww so ana haki ya kutoa mitizamo yake mahala popote pale
Muulizeni mhe Kikwete ni kwanini pesa zilitumika kwa ule mchakato wa katiba na kisha ule mchakato haukukamilika ilhali Rais ndio mwenye mamlaka makubwa kwenye nchi ?
 
Wewe mi sio chadema lakini nikuhakikishie kuwa wapinzani wote wamefurahi ndugai kukutana na unyama alio uasisi, wote Wanakubaliana kuwa alikuwa na hoja ila kwa kuwa hoja imebebwa na aliyeshiriki kuumiza watetezi wa haki hiyohiyo basi bora aondoke kwanza hoja itabebwa na wengine bila kujali chama.


Huyu alikuwa bedui hasa wa demokrasia. Kwani tumesahau alichowafanya juzi tu akina J Slaa, Gwajima, Lissu ndo kabisa hadi alitamani afe kabisa.
soma nlichoandika na uelewe
 
Mkopo upi usio na kichwa Wala miguu kwa Awamu hii ? Maana hapa tunamzungumzia Ndugai akimshambulia mama

Mwenye miradi yake alieanzisha alikopa mapesa ndio akajenga, alafu mnataka mama asikope kwa pesa gani tulizokuwa nazo ?

Hivi aliezuiwa kutoa maoni Ni nani ? Hakuna aliezuiwa kutoa maoni. Ndugai kilichomponza akajikuta karopoka yasioeleweka Ni homa ya 2025
Ndugai kamshambulia lin mama ako?
 
Kwani hayo ya ukandamizaji wa uhuru wa maoni imeanza leo? Tena saizi si ni afadhali kuliko awamu iliyopita, na kuhusu tozo si waliiundia hukohuko bungeni na wakaipitisha yeye akiwa kiongozi au napo alisinzia kama alivyosemaga wakati ule? Haandamani mtu hapa hakuna cha kusema chadema wenye utimamu wala nini. Kila mtu apambane na hali yake tuu.
kaangalie clip ya Ndugai urudi tena kutujibu
 
Huyu Mama mwanzoni alinipa matumaini kidogo ila kuna mambo yameanza kunipa wasiwasi.Mfumuko wa bei uko juu, gharama za umeme ndio kama tulivyosikia. Kuhusu demokrasia bado anga halijatulia.
Doa jingine ni kwa ishu ya Ndugai, Ndugai anaongoza bunge ambalo kazi yake kubwa ni kuisimamia Serikali. Kwa kawaida mchakato wa kukupa huwa haupiti bungeni, hivyo Spika na wabunge kwa ujumla wanapaswa kuhoji na kudadisi mikopo serikali inayokopa nje au ndani ya nchi.
Pamoja na kwamba Ndugai alikuwa ni Spika wa hovyo nadhani hakupaswa kulazimishwa kujiuzulu kwa kuhoji tu namna Serikali inavyokopa, labda kama kuna sababu ya zaidi ya hiyo.
Wewe ni mbumbumbu,Samia ndio kaleta mfumuko wa bei? Hujui kwamba ni global issue iliyosababishwa na covid?

Usipate shida kama vipi hamia huku mfumuko wa bei uko chini Sana maisha ni simple 😀😀

Screenshot_20220106-211054.png


Screenshot_20220106-211127.png


Screenshot_20220106-141853.png


Screenshot_20220106-141709.png


Screenshot_20220106-133419.png


Screenshot_20220104-065943.png
 
Asante Sana Wana Iringa, Dar es salaam tutakutania viwanja vya Jangwani.
Nimepata Pia taarifa kutoka Arusha watakutania nje ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Mbeya wameniambia watakutania viwanja vya airport ya zamani, songea karibu na uwanja wa Majimaji.
Hivi nasubiri mikoa mingine ili nitoe taarifa rasmi
Wakija unitag
 
4by94 na mtindo huru ni wafuasi wa Magufuli wasio amini uongozi wa Samia, watufafanulie haya;

1. Wao wanapinga mikopo mbona Magufuli alikopa tril 29 kwa miaka mitano tena kwa riba kubwa au Ndiyo wale waliokuwa wanadanganywa kuwa tunatumia fedha zetu!

2. Pamoja na mikopo mikubwa hiyo miradi mingi haikumalizika na mingine haikufikia hata nusu mf reli, bwawa, je fedha za kumalizia zitatoka wapi?

3. Ndugai alikuwa wapi wakati mikopo ya awamu ya tano inafika kiasi cha tri 70 mbona hakuwahi kutwambia lakini pia alikubaliana na tozo iweje leo kuhadaa Wananchi kwa tril 1.3 isiyo na riba tena itakayorudishwa baada ya miaka 20.

4. Uhuru wa maoni mmeuona leo kuwa ndipo unaminywa, je kipindi cha Magufuli nani alithubutu kuongea lolote ? Mnajifanya mmesahau wakosoaji wa Magufuli walivyopigwa risasi na kuhojiwa na huyohuyo Ndugai, Roma, Lissu, Maaskofu, wabunge wenyewe J Slaa, wanahabari akina Mayalla, na matumizi mengine mabaya ya sheria na kanuni kama vile kuingiza wabunge wasiostahili na mengine mengi.

Kama mlikuwa na maslahi wakati huo basi imepita.
huezi kubariki makosa kwa kosa lililopita , huo ndo ujinga tunao sisi wabantu
 
Tozo hazikuanza jana Ndugai alipojiuzulu, na isitoshe Ndugai ndio kazileta. Mbona hamkuandamana? Sio kwamba hatujui umuhimu wa maandamano, hatuko tayari kuungana na wanafiki.
Kaangalie ile clip , Ndugai ashatoa majibu ya swali lako
 
Kwa taarifa yako, kibali tupo hatua ya mwisho kupata, kwani Pia polisi wanaotoa vibali wamechoshwa na haya yanayoendelea nchini na sarakasi za serikali.
Taarifa zimeshafika katika vijiwe vyote vya bodaboda Dar, na machinga wote
Polisi wa ufipa labda
 
Back
Top Bottom