Maandamano ya wanahabari Sept 11, 2012

Ninyi ni waandishi wa habari lakini mnafikisha ujumbe wenu kama hamjiamini vile?.. Sioni meseji nzito nzito kwenye mabango zinazoonyesha hasira zenu!.. Waswahili husema, "Ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni!"
 
Nchimbi mafia ni moja ya watu wanaolitumia vibaya jeshi la polisi na sielewewi hapo alikwenda kufanya nini kama hakuwa na mwaliko zaidi ya kupenda sifa lakini sishangai labda kwa sababu kichwa kikubwa na masikio madogo vinaathiri uwezo wake wa kuchanganua mambo,hata songea ana hali mbaya sana!!!!!!!!!!!!!!!
 
Waziri wa habari amefika Jangwani kuongea na waandishi wa habari walioandamana kwa ajili ya kifo cha Mwangosi lakini amezomewa vibaya, na walipoulizwa waandishi ni wangapi wanataka awahutubie wote wamemkataa, ikabidi aondoke kwa aibu kubwa.

safi sana akome kiherehere
 
Viongozi wetu wanapenda sana kuhudhuria vikao vya mazishi na kutoa rambirambi kubwa zaidi ya kuyatazama matatizo ya wananchi na kuyatolea suluhu inayoendana na wakati husika. Tusome alama za nyakati jamani! Siku hizi kila mtu ana uelewa wa afanyalo na hamna anaeweza kupelekeshwa na viongozi uchwara walio na dhamira mufilisi wanaothubutu hata kutumia polisi kujinufaisha. Kwa staili hii nchi itakua haitawaliki na amani itatoweka kwasababu polisi watakua kama adui kwa wananchi badala ya kuwa walinzi. Hawa polisi sio kwamba wana nia ya kuwauwa wananchi bali wanaamriwa ingawaje wengi wao hawataki hata yale wanayoyafanya!! "Dunia imebadilika na ukiona tunapoelekea ujue ukoloni unarudi rasmi". Kiongozi kuzomewa sio utashi wa kisiasa bali ni kutokusoma alama za nyakati kwa kuyafanya ya kale enzi za kisasa. Raisi upo wapi mbona hatuoni tamko lako kuhusu mauwaji haya? Please tunataka haki itendeke pande zote amani yetu mturudishie na si masilahi ya viongozi na vyama yatangulizwe! It is very painful
 
Hawajamfukuza,kama wangemfukuza manake wangegomea hata sauti na mwangwi wa sharubu zake usisike ktk vipaza vyao"lakin ajabu kila mwandish alimpelekea kipaza chake pale Nchmbi aliposhuka jukwaani...na kwa ujinga huu Nchimbi akapata nafasi ya kufikisha ujumbe wa kile alichokusudia
 
Inabidi msimame kidete kulinda mshikamano wenu wanahabari umoja ni nguvu
 
Unapoiongoza jamii yenye uwezo mkubwa wa kifikra kuliko wewe uliyepewa dhamana ya kuongoza yapaswa uwe makini sana lakini nadhani Nchimbi hakulitambua hilo.
 
Nchimbi kafukuzwa kwa aibu na waandishi wahabari wanasema yeye kaja kuwapokea kama nani wakati hawajamwalika
- yeye amegoma kuondoka, sasa hapa fujo tu angalieni channel 10 laivu


Ndo akome huyo waziri mwenye ubongo wa mende, alikataa kujiuzulu, na sasa anang'ang'ania mkutano wa watu, kama hupendwi hupendwi tu, asanteni wanahabari kwa kumpa za uso laivu. I like this.
 
Huyu Nchimbi anaongea nini sasa?
Eti anabwabwaja ya kwmb maisha ya mtanzania inaheshimika!

Jamani maisha yetu yanaheshimika jamani??


Hapanaaaaaaa....wanatesa wananchi utadhani wao sio watanzania wenzetu....akili zao finyu lazima ziwacost na serikali yao mbovu ya ccm inayofumbia macho uovu wote
 
Naunga mkono maandamano, kama haki ya msingi ya kila raia kutoa maoni yake. Siungi mkono kitendo cha kuzomea waziri, kwa kuwa tendo la mauaji, si dhamira ya serikali wala chama chochote cha siasa, bali ni utendaji kazi mbovu wa mtu mmoja na wala si jeshi la polisi.

Ficha upumbavu wako japo kwa sekunde,serikali na jeshi unalolitetea vimebaki uchi kwa kupiga sarakasi huku wamevaa taulo!Wenye mawazo kama yako na Tendwa ni HATARI kwa nchi.Shame on you
 
ningependa moja ya maazimio iwe ni maandamano kama hayo kila mwezi kwa muda wa miezi sita ili swala la unyanyasaji na mauaji ya polisi liendelee kukaa ndani ya vichwa vyao.
 
Samahani wakuu....hivi katika hao waandishi' je kuna mwandishi yeyote aliyekuja hapo kutokea CLOUDS MEDIA?
 
Back
Top Bottom