NYARONYO KICHEERE: Hati ya Kiapo juu ya Ujio wa Nchimbi JANGWANI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NYARONYO KICHEERE: Hati ya Kiapo juu ya Ujio wa Nchimbi JANGWANI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, Sep 15, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,210
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  HATI YA KIAPO JUU YA UJIO WA NCHIMBI JANGWANI

  Na Nyaronyo Kicheere
  Ndugu wanamabadiliko,
  mimi nakubaliana na wale wanaosema dk nchimbi alialikwa jangwani. nimelazimika kuingilia kati na kutoa ushahidi wa kiapo kwa vile naona kama vile ukweli hausemwi. maoni yangu ni kwamba watu wakubali ukweli hata kama unauma na ukweli wenyewe unapatikana kutokana na ushaidi wa mazingira (circumstantial evidence):
  KIAPO CHENYEWE;


  MIMI nyaronyo mwita kicheere, mtu mzima, mpagani na mkazi wa tungi, kigamboni, dar es salaam, tanganyika territory (pamoja na sehemu za ziwa nyasa), NAAPA kwa mizimu ya nyamongo na KUTAMKA yafuatayo:


  1.
  KWAMBA mimi nyaronyo mwita kicheere, nilikuwepo, nilishiriki na nilichunguza kwa makini nyendo za watu fulani fulani kwenye maandamano ya wanahabari yaliyofanyika jumanne wiki hii kwa hiyo nafahamu ukweli wa haya ninayoyaeleza hapa chini.

  2. KWAMBA baada ya kuandamana kutoka ofisi za channel ten hadi viwanja vya jangwani hatukukuta maandalizi yoyote ya maana pale viwanjani jangwani kwa maana kwamba hakukuwepo jukwaa wala vipaza sauti.

  3. KWAMBA muda mfupi tu baada ya kuwasili zilisikika sauti na minong'ono ya chinichini hasa ya akina mama wakipinga ujio wa dakitari wetu mtukuka nchimbi na kwamba kwa sababu ya ufupi wake nchimbi hakuwa ameonekana kwa wengi wala kufahamika kuwa alikuwapo.

  4.
  KWAMBA mimi binafasi nilichukua jukumu la kuwahoji wale wanahabari wa kike, kama huyo nchimbi wanayemlalamikia ni nani, na yuko wapi, na kaja kufanya nini pale jangwani kama yeye si mwanahabari.

  5.
  KWAMBA wanahabari wale wa kike walinielekeza mimi pamoja na wenzangu tuliokuwapo jirani nao mtu waliyedai ni dakitari mtukuka nchimbi na wakadai kuwa mtu yule hakuwa na lolote la kuuambia ummati ule wa wanahabari kwa sababu wauaji ni serikali na nchimbi ni sehemu ya serikali.

  6. KWAMBA mimi pamoja na wenzangu tuliokuwa tumesimama jirani na wanahabari wale wa kike tulisaidia kusema na kupaza sauti kuwa nchimbi hahitajika kwenye mkutano ambao serikali ilikuwa inalaaniwa kwa vitendo vya watendaji wake na hasa polisi ambao wanapaswa kulinda amani, mali na uhai wa raia lakini wao wanashiriki kuua!

  7. KWAMBA nchimbi kwa kujiamini kabisa alitukonyeza kuashiria kufahamiana sana na sisi na kwamba yeye ni mwenzetu. zipo ishara, vitendo na mwonekano (body language) vinavyoashiria kuwa mhusika ni mwenyeji tena alwatan na hivyo hababaiki wala kuterereka na yanayotokea mfano ukonyezaji.

  8. KWAMBA kitendo cha kutukonyeza badala ya kuondoka viwanjani jangwani kilituudhi wandishi na hasa wanahabari wa kike ambao waliongeza sauti zao kumkana nchimbi na kumtaka aondoke jangwani ili kuwaacha wanahabari waomboleze peke yao kifo cha mwenzao.

  9. KWAMBA pamoja na kelele za "nchimbi ondoka kuongezeka", msemaji wa jukwaa la wahariri (charles misango) alipopanda kwenye rundo la udongo lililogeuzwa jukwaa kutokana na kutokuwepo maandalizi ya maana naye nchimbi alimfuata jirani na kupanda jukwaa lile la rundo la udongo kama mtu aliye tayari kutoa hotuba.

  10. KWAMBA hapo ndipo uzalendo ulipowashinda wandishi na kilichofuata ni biashara inayofahamika kwetu wote wanahabari, mashushushu (ambao siku ile hawakuwa wanahesabika pale jangwani kwa wingi wao), mapolisi na wananchi kwa ujumla.

  11. KWAMBA baada ya sakata lile la kumwondoa nchimbi mkutanoni na akaondoka kwa aibu zote zinazoweza kuelezeka, wandishi wa itv walimfuata pembeni na kumhoji na baadaye siku hiyo kumwonyesha na kumtangaza nchimbi eti wakitaka kujua sababu za yeye kuvamia maandamano ya wanahabari.

  12. KWAMBA kwa uelewa wa mtu wa kawaida, itv wanashukiwa kuhusika na kumwalika nchimbi jangwani. kwa nini wamfuate mtu kumhoji baada ya kumtimua? unamtimua wa nini kama unamhoji na kumtangaza si bora ungemwacha basi akahutubia wandishi halafu mkapata habari ya kuonyesha na kutangaza kama lengo na nia yenu itv ilikuwa habari za nchimbi na siyo maombolezo ya mwangosi? kitendo hiki hakivumiliki na kilitudhalilisha sana wanahabari. mnamfukuzaje mtu halafu mnamkimbilia kumlamba miguu?  13. KWAMBA ninakumbuka kuwa hii si mara ya kwanza itv kufanya jambo la kinafiki na la hovyo kama hili. huko nyuma, wandishi waliwahi kukubaliana kutomquote wala kumwandika waziri Mkuchika hata angefanya nini duniani hapa. lakini siku mkuchika alipokuwa anahutubia jambo fulani na akatamka mema kadhaa kumhusu mwenyekiti wa IPP r.a.mengi maamuzi ya wanahabari yalitupiliwa mbali na mkuchika akatangazwa na kuonyeshwa kwenye runinga za itv na ipp akimsifia bwana mkubwa bila kujali mgomo uliokuwepo!


  14. KWAMBA pamoja na itv mtu mwingine ninayemtuhumu na kumshutumu kwa kumwalika nchimbi ni katibu wa jukwaa la wahariri bw. nevil meena. huyu bwana alitoa hotuba nzuri sana lakini akamalizia hotuba yake na maneno mabaya sana.

  15. KWAMBA meena alisikika akisema; hatuna ubaya na nchimbi, tunampenda nchimbi, hatuna ugomvi na serikali, hatuna ugomvi na polisi! jamani mwenye mkanda na akausikilize vizuri. sasa kama wanahabari hawakuwa na ugomvi na serikali maandamano ya nini? kama wanahabari hawana matatizo na polisi je matamko na kulaani alikuwa analaaniwa nani na kwa nini? kama wanahabari hawakuwa na tatizo na nchimbi je kwa nini walimtimua? mimi nina mashaka makubwa sana kuwa huyu bw. meena ndiye alimwalika nchimbi.

  16. KWAMBA nyie wahariri kupitia kwa katibu wenu mlikuwa mnajipendekeza kwa nchimbi kwa nini? nyie wahariri mlikuwa mnajifanya wazuri kwa nchimbi eti wabaya ni wanahabari wanaomtimua nchimbi mlikuwa mmeahidiwa nini? si bure, mpaka mkajitoa bila aibu vile kumtukuza nchimbi, serikali na polisi kupitia kwa meena baada ya kutoa hotuba ya kulaani na kukerwa na serikali na polisi, hakukuwa bure kuna jambo. mlimwahidi aje na mtampatia nafasi ya kuongea naye kwa kujua 2015 yaja kajiingiza kichwa kichwa na kaja kweli.

  17. KWAMBA baada ya hotuba zile kabla hatujaondoka jangwani nilikaa jirani na wahariri fulani (nawakumbuka watatu, jesse kwayu wa nipashe, bakari machumu wa the citizen na dennis msacky wa mwananchi) na hapa jesse kalikoroga kwa kuhoji "hivi nchimbi hawezi kuelewa mahali pa kuhudhuria na wapi kutohudhuria?"

  18. KWAMBA kwa mshangao wa wengi dennis msacky alijibu kwamba nchimbi kagain political capital! jibu hili lilipingwa na wote, jesse, bakari nakumbuka hata mimi nilipinga. tukajaribu kumwonyesha msacky namna alivyoaibika nchimbi na hakupata ujiko wowote huku yeye aking'ang'ana "ehe huoni yeye kafika hapa ni waziri pekee aliyekuja hii ni njema ni political capital"! hakuna aliyemsikiliza na sote kwa pamoja tulimbamiza hadi akakubali kuwa rafiki yake kachemka. nasikia dennis ni rafiki yake kipenzi dk nchimbi. nami nasema namtilia shaka sana dennis kuwa naye alihusika kumwalika nchimbi jangwani.
  kicheere, tungi kigamboni tanganyika territory


  Uthibitisho:
  mimi nyaronyo mwita kicheere nathibitisha kwamba yote niliyoyasema hapo juu hasa aya ya 1 -18 ni kweli tupu na si kitu kingine bali ukweli mtupu.
  kicheere, tungi kigamboni tanganyika territory


  ubaya ni kwamba ukweli huu unalifanya jukwaa la wahariri kuwa jukwaa la wanafiki hata kama si wote ni wanafiki. watu wako kwenye jukwaa kugain materially na politically. yaani kujiweka katika good books of government!!!!!!!! usiku mwema
   
 2. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sanaa imemshinda. Najua lengo lake ni zuri kuonyesha kuwa jina la Kikwete linalipa, lakini amekwenda mbali zaidi ya alipopaswa kwenda. Sababu alizotoa kwenye kiapo chake zinatosha kukubalika kisanaa lakini si kisheria.
   
 3. m

  mkupuo JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Na mimi Mkupuo Kilanga, mtu mzima,pandikizi,mwanaume wa ukweli, mpagani na mkazi wa Nanjilinji, tanganyika territory (pamoja na Unguja & Pemba), NAAPA kwa mizimu ya nanjilinji na KUTAMKA yafuatayo:
  1.Kwamba maelezo yako yanaonesha ukweli,
  2.Kwamba kwenye msafara wa mamba na kenge wapo,
  3.kwamba inji hii inaangushwa kwa kiasi kikubwa na wachumia tumbo kama baadhi ya hao waandishi wa ITV,
  4.Kwamba kuanzia leo nitakipotezea kituo cha TV cha ITV KAMA NILIVYOFANYA KWA TBC,
  5.Kwamba tumegundua Jukwaa la wahariri siyo la msaada kwetu cc waandishi wa habari,
  6.Kwamba leo tumejua kwa nini waandishi wa habari hatuheshimiwi tunapokuwa kazini kwa sababu ya njaa zetu.
  7.Kwamba n.k
   
 4. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  watanzania tuna tabia za unafiki sana. huu ni usaliti mkubwa.
   
 5. N

  Noboka JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,144
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Hata mimi ambaye si mwandishi nilivyomuona siku ile Meena nikajiuliza oooh, sasa hawa jamaa wameshasalitiana, lakini kwenye msafara wa mamba na kenge wamo, Nyarongo msikate tamaa
   
 6. j

  joely JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,030
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Hauitaji kuwa na akili sana kujua meena alipozungumzia habari ya nchimbi alikuwa anawang'ong'a waandishi wenzake kwa kumfukuza nchimbi.
  shame on you meena
   
 7. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kuna aliyeiweka tayari.....sasa zimekuwa 2.....mods ondoeni 1 tafadhali!
   
 8. The Fixer

  The Fixer JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 1,361
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ha ha ha haaaaaa Nyaronyo Kicheere sishangai kwa mtindo uliukosa hata U - DC mwenzako Meena ndio anauwinda hivyo kwani we hujui kuwa ma DC wanatokaga IPP Media anza kuhesabu kwa yule wa Bahi mpaka hapa Juzi wa Hai, Utagundua kitu !
   
 9. Mzururaji

  Mzururaji JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,236
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Dah mwanahalisi kufungwa tumemiss vingi mia mia muwe mnafungukia humu
   
 10. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Njaa tu ndio zinazo waumbua nyie waandishi,hamna chochote cha maana!
   
 11. Osia

  Osia Member

  #11
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 1, 2012
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh! Asa mi nadhani hapa c kenge tu kuwamo hofu yangu ni kua vima nao wamo!!!!
   
 12. Mzururaji

  Mzururaji JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,236
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  ku kot srid lote refu haraf unajaza pumba mi cjaona cha maana walimu njaa madokta njaa polis njaa waandishi njaa we upo wap mbona husem au ndo wote wapga debe kwe daladala
   
 13. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kaka yangu Kicheere, mbuya ore!
  Kwanza pole sana kwa msiba wa mwandishi mwenzako Bwana Mwangosi, hakika msiba huu umekugusa sana. Niliona siku ile tata ulivyotaka hata kurukia mtu kichwa ili Dakta Nchimbi apotee mbele ya upeo wa uso wako. Pole sana.
  Nimeisoma makala yako yote, ni makala ambayo mtu akiisoma mara moja ni rahisi kufahamu uliiandika ukiwa kwenye mood gani!
  Kaka Kichere, uandishi wa habari ni moja ya fani ambazo zimejaa mamluki wengi wa kutosha kuwapoteza pale mnapotaka kuungana kufanya jambo ambalo linaweza kuisumbua na kuitia kashkash serikali ya CCM.
  Mamluki wa ana hiyo wamejaa kuanzia wenye vyama vya waalimu, madaktari, TUCTA, shirika la reli nk.
  Hawa jamaa ili uweze kuwatambua yakubidi uwe na jicho la tatu, kwani ukiwaangalia kijuujuu ni watu walioko mstari wa mbele kuwaunganisha na kuwahamasisha watu lakini kumbe ndio wavurugaji wakuu.
  Kwa tulipofika sasa, inabidi tuwe makini sana na hawa tunaowachagua kutuongoza hasa tunapopigania haki zetu, vinginevyo tutakua tunatwanga maji kwenye kinu.
  Pole sana kakangu Nyaronyo Kicheere.
   
 14. Hashpower7113

  Hashpower7113 JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 452
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 80
  Naunga mkono hoja ya mwalimu wangu, mtu mzima, mpagani, mkaazi wa Tanganyika aliyeapa kwa jina la mizimu ya Nyamongo! Nyaronyo... keep on telling em snitches truth! No honour on the dark side of the law!
   
 15. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 512
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,553
  Likes Received: 18,238
  Trophy Points: 280
  Kuhusu Jukwaa la wahariri, nilishasema siku nyingi hawa ni puppets!.

  Fanya folloup ni nani analigharimia?!. Kama ilivyo kwa MOAT, he who pays the piper may call the tune!.

  Kwa kumbukumbu zangu, chama halali cha waandishi wa habari, Statutoty association ni Tanzania Journalist Association (TAJA). Hivi vingine vyote Tamwa, Jet, Moat, Jukwaa la Wahariri, Ajat, Misa, Shirikisho la Wanahari etc, nyingi ni NGO na vingine ni makampuni ya watu na ulaji!.
  Pasco.
   
 17. Ndukidi

  Ndukidi JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 821
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Jamaa namkubali, hata mimi ni mwalimu wangu huyu jamaa!!!
   
Loading...