Maandamano ya oktoba 29, 2025 hayawezi kufanikiwa, japo nia yake imewapa ujumbe mkubwa mafisadi

Maandamano ya oktoba 29, 2025 hayawezi kufanikiwa, japo nia yake imewapa ujumbe mkubwa mafisadi

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
15,773
Reaction score
35,992
Ningetamani haya maandamano yatokee na sisi tufanye mapinduzi dhidi ya mafisadi na viongozi wahuni, lakini Kwa vyovyote hili halitawezekana

Mafisadi na wahuni watafanikiwa kufanya uchaguzi fake Kwa amani na kujitangaza kushinda na baadaye kujiapisha na kupigiwa mizinga na jeshi letu,

Sababu Kwa nini maandamano hayatafanikiwa

1. Hakuna kiongozi wa maandamano
Yaani watu wanahamisishwa waandamane hawana kiongozi wao wa ku organise

2 Kuandamana kuelekea wapi na ujumbe Gani?
Watu hawaelewi wataandamana kuelekea wapi? Ikulu? Vituo vya police? Kambi za jeshi? Serikali za mitaa? Ofisi ya mkuu wa mkoa?
Yaani mtu wa Ngara, Tandahimba, Mwanga, Iramba, Katavi n.k ataamka anaandamana vipi? Si kuonekana chizi mtaani

3. Agenda za maandamano hazipo wazi?
Tunapinga uchaguzi?
Tunapinga ufisadi?
Tunapinga utekaji na mauaji?
Kuuza bandari?
Masai kukosa makazi?
Yaani watu waandamane Kwa lipi zito?
Nadhani ingekuwa agenda 1 tu. Kama Kenya wao walipinga mfumko wa bei hasa unga na mkate na walifanikiwa.
Napel walipinga ufisadi

4 Ujumbe haufiki Kwa Watanzania wengi.
Hamasa za maandamano zipo mtandaoni tu, ila watu wengi hawana muda na mtandao wala hawajui nini kipo huko, ingekuwa maandamano yanatangazwa kwenye redio, TV na magazetini hapo hii kampeni ingefikia wengi

5. Watanzania wengi washaamua kutopiga kura.

6. Hofu na unafiki wa Watanganyika.
Watanganyika wataandika mtandaoni ila kwenye vitendo ni makondoo na mijitu mijinga mno

7. Nguvu ya mafisadi
Mafisadi yameungana na yapo tayari kuhakikisha maandano hayafanikiwi.
Yanahonga watu na viongozi

8. CHADEMA kutokubeba hii agenda ya maandamano
Hiki ndo Chama kina wafuasi wengi, kukaa kimya Kuna ashiria haya ni maandano hewa tu
 
Random Demonstrations ndiyo huwa mbaya zaidi.

Na maandamano yasiyo na kiongozi ndiyo huwa yanafanikiwa zaidi, maana mkiwa na kiongozi akikamatwa tu basi wengine mnapoteana au mnaishiwa morali.

Maandamano yaliyowaangusha viongozi wa nchi wengi duniani hayajawahi kuwa na viongozi wa maandamano.

Hata jinsi ya kuwatisha waandamanaji huwa ngumu, mfano mpaka sasa vyombo haviwezi kujua vimkamate nani na vimuache nani.

Cha mwisho, maandamano ya aina hii huwa hayana formula. Na hii huwafanya hata vyombo vya ulinzi visijue wajigawe vipi.

Wanaweza kuweka nguvu kubwa Ubungo mataa, ila nyomi likaanzia Temeke linakuja Town Centre.

Au nyomi likaanzia Mbagala kuelekea Town Centre.

Au nyomi likaanzia Tegeta huko kuelekea Town Centre.

Kimsingi maandamano ya namna hii ndo yana chance kubwa ya kufanikiwa kwa sababu raia wanakuwa wametapanyika na nyie polisi hamtajua mzuie wapi na muache wapi.

Na maandamano is all about nyomi la watu.

Kitendo cha watu kufika 2000 tu, basi moto unakuwa umeshawaka maana hapo hata mje polisi 500 hamtaweza kufanya chochote.
 
Haya ya kwetu yamekosa hamasa yapo tu mtandaoni ila mtaani hakuna kitu
 
The Black Swan: The Impact of the Highly Improbable by Nassim Nicholas Taleb

Mwandishi anasema :
  • Black swan(Bata maji mweusi) ni matukio yaliyo nadra saana kutokea Ila matokeo yake ni makubwa ya kushangaza.
  • Binadamu hujifunza tu pindi matukio hayo kutokea.
  • Mifano, 2008 uchumi kuanguka, Nepal, kuibuka kwa Internet, kuibuka Ai, kifo Cha Jiwe n.k
  • Uchambuzi wa mambo kwa usahihi na kujipanga sio kinga ya Black swan.
  • Watu hufikiri wanajua yajayo na namna ya kukabili, Ila ni kujifariji tu(cognitive bias)
  • Kujipanga kimatukio yanayo tazamiwa kutokea ni tofauti na Tukio Moja litakalo vuruga mpangilio mzima.
  • Black swan hutela matokeo yasiyo tarajiwa na japo tahadhari zote zilizingatiwa.

Ushauri wa Mwandishi :
  • kuwa ngangari muda wote na si kuwa lainilaini.
  • Kujipanga saana ndio kutabiri uwezekano wa kutokea ya kutokea.
  • Jitahidi "kuchukuliwa Poa" huenda ndio msaada kuliko "kujipanga sana"

Black swan ni njia ya kukumbusha Binadamu kuwa "Yasiyo Tabirika" siyo kwa hayawekani bali, "HAYAEPUKIKI"

Naunga mkono Hoja.
 
Juhudi za kuandamana post election naziunga mkono
 
Sasaivi ilitakiwa kuanze maandamano madogo madogo kuwapa watu morali. Kusubiri tar 29 hiyo ndo watu wote watoke sio kweli.
 
Vipi uliwaona wazee wa makomborero tarehe 29 oktoba na kuendelea 🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom