Maandamano ya kumlaani Spika Makinda

Kulikomboa Bunge ambalo linaficha uozo wa Serikali kupitia mgongo wa Kigagula nako ni mojawapo ya juhudi mbali mbali za kuikomboa nchi iliyopokwa na magamba. Makucha ya magamba yamejikiita pia ndani ya Bunge la Tanzania ndio maana madudu mengi yanatokea nchini kutokana na kuwa na Bunge fisadi.

Kama Bunge hili lingekuwa makini katika kupambana na maovu chungu nzima yanayofanywa na mafisadi ndani ya Serikali basi mafisadi wengi sasa hivi wangekuwa wanachezea mvua lupango badala ya kuendelea kupeta mtaani. Bunge pia linahitaji kukombolewa toka kwenye makucha ya magamba ili Bunge hili liweze kuwa wawakilishi wa kweli wa wale wanaowachagua Wabunge kuwa wawakilishi wao badala ya kuweka mbele maslahi ya magamba.

Mkuu BAK, kuandamana nchi nzima, kumlaani Spika na Naibu wake, is a good thing, tutajitokeza kwa wingi kuhudhuria maandamano hayo na kuipongeza Chadema kwa nguvu zetu zote, tena tulaani hadi kwa albadir!, then what?. Hicho ndicho Watanzania wanachotaka kuelekea 2015?.

Kwa maoni yangu, its high time Chadema ipunguze "populist" issues na ijikite kwenye "liberation strategies" kuwaeleza Watanzania itawakomboaje kutoka katika makucha ya CCM!.

Mtu ukiwa umekabwa na kupiga tuu mayowe ya kuomba msaada bila juhudi za dhati za kujinasua, mwisho utaishiwa pumzi na mkabaji kuishia kujinyongea kwa ulaini kabisa!. Maendeleo ya Tanzania yamekuwa yakikabwa na CCM kwa miaka yote 50 iliyopita, kuendelea kupiga mayowe "tunakabwa, tunakabwa!", inatosha!, sasa tunataka kuzikia juhudi za kujinasua!.
Pasco.
 
wabunge wa cdm hawana nidhamu na wanaendekeza fujo na lugha za kejeli bungeni je nyinyi hamlioni hilo?namsupport ana makinda 100 % anafaa mno kuwa spika.
lazima umtetee huyu wifi yako kwenye uzembe huu, ila mtahadhalishe juu ya nguvu ya Uma. You can fool some people sometimes but you cant all the people all the times. Nyie pakeni rangi za kucha tu na kuvaa ma wig, mkidhani watanzania hawa ni wale wa mwaka 47!
 
Kulikomboa Bunge ambalo linaficha uozo wa Serikali kupitia mgongo wa Kigagula nako ni mojawapo ya juhudi mbali mbali za kuikomboa nchi iliyopokwa na magamba. Makucha ya magamba yamejikiita pia ndani ya Bunge la Tanzania ndio maana madudu mengi yanatokea nchini kutokana na kuwa na Bunge fisadi.

Kama Bunge hili lingekuwa makini katika kupambana na maovu chungu nzima yanayofanywa na mafisadi ndani ya Serikali basi mafisadi wengi sasa hivi wangekuwa wanachezea mvua lupango badala ya kuendelea kupeta mtaani. Bunge pia linahitaji kukombolewa toka kwenye makucha ya magamba ili Bunge hili liweze kuwa wawakilishi wa kweli wa wale wanaowachagua Wabunge kuwa wawakilishi wao badala ya kuweka mbele maslahi ya magamba.
Mkuu, BAK, nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%, kuna swali nimeuliza, na ninaendelea kuuliza na kuuliza na kuuliΩa tena!, bunge ni uoza, CCM ni uazo, serikali ni uoza!, tumewaambia Watanzania kuhusu uoza wote huu tangu 2010 mpaka leo 2013, bado tunaendelea tuu kuandamana na kufanya mikutano nchi nzima kuelezea kuhusu uoza huu na ule?!. Jee hayo ndio mahitaji ya Watanzania kwa sasa kuelekea 2015?!. Kama mpaka leo tunaendelea kulaumu tuu na kulalamika, lini mtawaeleza Watanzania, nini Chadema, mtawafanyia nini?. CCM imefanya madudu for the past 50 years!, jee kazi ya Chadema ndio hii tuu ya kuendelea kuyapigia makele madudu ya CCM?!, ni lini sasa mtaanza kueleza kile ambacho nyinyi Chadema inaweza kukifanya ili tuwaaminiye tuwape nchi 2015?!.

Kama mnaamini maandamano na mikutano ya kulaani na kulaumu ndicho Watanzania wanachohitaji kwa sasa kuelekea 2015, then its fine, endeleeni kuandamana na kufanya mikutano nchi nzima halafu subirieni CCM ishinde tena na nyinyi muendeleze maandamano na mikutano nchi nzima hadi 2020, na 2025, na 2030 and on and on and on kama alivyosema Mkuu Le Mutus!.

Pasco.
 
Kuna namna mbali mbali ya kuikomboa nchi iliyopokwa na mafisadi ikiwemo maandamano na mikutano ili kuwahabarisha Watanzania mbali mbali waelewe matatizo makubwa nchini yanasababishwa na nini ili katika uchaguzi ujao waweze kutumia haki yao vizuri na kutokichagua chama ambacho kinachelewesha au hakijali maendeleo ya nchi.

Chadema kwa sasa haiwezi kuwafanyia Watanzania chochote kile kwa kuwa haijashika madaraka. Nchi gani duniani ambayo uliona chama pinzani kikawafanyia wananchi wa nchi hiyo mambo makubwa bila kuwa chama tawala!? Hata katika nchi za magharibi hili la chama pinzani kufanya mambo makubwa kwa Wananchi bila kuwa na Serikali ni jambo gumu sana.

Hivi unaishi nchi gani hadi hii leo hujui mambo mbali mbali ambayo CDM imewaahidi Watanzania pindi ikiweza kushika madaraka? Kama huyajui basi fanya homework yako usingoje BAK akutafunie.

Mkuu, BAK, nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%, kuna swali nimeuliza, na ninaendelea kuuliza na kuuliza na kuuliΩa tena!, bunge ni uoza, CCM ni uazo, serikali ni uoza!, tumewaambia Watanzania kuhusu uoza wote huu tangu 2010 mpaka leo 2013, bado tunaendelea tuu kuandamana na kufanya mikutano nchi nzima kuelezea kuhusu uoza huu na ule?!. Jee hayo ndio mahitaji ya Watanzania kwa sasa kuelekea 2015?!. Kama mpaka leo tunaendelea kulaumu tuu na kulalamika, lini mtawaeleza Watanzania, nini Chadema, mtawafanyia nini?. CCM imefanya madudu for the past 50 years!, jee kazi ya Chadema ndio hii tuu ya kuendelea kuyapigia makele madudu ya CCM?!, ni lini sasa mtaanza kueleza kile ambacho nyinyi Chadema inaweza kukifanya ili tuwaaminiye tuwape nchi 2015?!.

Kama mnaamini maandamano na mikutano ya kulaani na kulaumu ndicho Watanzania wanachohitaji kwa sasa kuelekea 2015, then its fine, endeleeni kuandamana na kufanya mikutano nchi nzima halafu subirieni CCM ishinde tena na nyinyi muendeleze maandamano na mikutano nchi nzima hadi 2020, na 2025, na 2030 and on and on and on kama alivyosema Mkuu Le Mutus!.

Pasco.
 
Maandamano ni njia ya kufikisha ujumbe kwa muhusika. Aina za jumbe ni ujumbe wa kuunga mkono na ujumbe wa kupinga/kulaani tukio au mtu.
Mwitikio wake ni wingi au uchache wa waalikwa ambao ndio waandamanaji na mwisho kupokea ujumbe husika.
 
Yametimia, yanafanyiwa kazi Jumapili hii, ila nimeuliza, tukishaandamana kulaani nchi nzima, then so what?!.
Pasco.

Pasco. Kama hujawahi kuona nguvu ya maandamano huishi dunia hii. I swear it won't be the same again!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Arushaone, ndio maana jamaa wanayazuia maandamano yenu kwa taarifa za ki inteligensia kuwa the hidden agenda behind haya maandamano ni rehersals tuu za kutuandaa sisi Watanzania, tuwe kama wenzetu Wamisri tutengeneze Tahriri Squire yetu, ili 2015 yafanywe maandamano makubwa kabisa kuelekea moja kwa moja hadi Magogoni kwa kutumia nguvu ya umma endapo kwenye sanduku la kura, mtazidiwa maarifa!.

Nani atayaruhusu!.

Pasco.
 
kikubwa si kuongozwa na hisia za kichama.tanzania ni zaidi ya vyama.makinda kapoteza umakini amebakia kuweweseka.lkn huwezi kumuondoa kwa kutumia cdm.tunahitaji mambo ya kitaifa yashughulikiwe na taifa zima.ubinafsi na kuvitukuza vyama ni kasumba na tutaendelea kuishuhudia ccm ikiongoza dola
 
Mambo mengine tunajifanya kuiga pasipo kutumia busara kuyafikiri kwa kina kama huu ni wakati wake.

Kwa mtazamo wangu,sifikiri eti kuandamana ndio suluhusho la matatizo ya msingi kama ajira kwa hao wanaoambiwa kuandamana na badala yake wanatumia gear ya kuandamana ili kuficha udhaifu uliomo ndani ya vyama vya siasa juu ya wao kuungana pamoja ili kuiondoa madaraka serikali wanayosema ni ya ukandamizaji wa haki.

Kama kweli hawamtaki Ndugu Spika na Naibu wake basi wasiingie bungeni ili kushinikiza matakwa yao,vinginevyo hii itakuwa ni siasa nyingine ya mwezi February.
 
Mkuu Arushaone, ndio maana jamaa wanayazuia maandamano yenu kwa taarifa za ki inteligensia kuwa the hidden agenda behind haya maandamano ni rehersals tuu za kutuandaa sisi Watanzania, tuwe kama wenzetu Wamisri tutengeneze Tahriri Squire yetu, ili 2015 yafanywe maandamano makubwa kabisa kuelekea moja kwa moja hadi Magogoni kwa kutumia nguvu ya umma endapo kwenye sanduku la kura, mtazidiwa maarifa!.

Nani atayaruhusu!.

Pasco.

mkuu 2010 kuna mpuuzi mmoja jimbo la Msalala aliiba ma box ya kura za urais kwa ulinzi wa polisi! Later fastjet akampa uwaziri! Chunguza huu ukweli.
 
Yametimia, yanafanyiwa kazi Jumapili hii, ila nimeuliza, tukishaandamana kulaani nchi nzima, then so what?!.
Pasco.

Pasco kadri ninavyokusoma katika posts na threads mbalimbali natambua kiu yako ya kutaka mabadiliko ya haraka. Lakini Pasco tunakubaliana kuwa watanzania wenzetu hawa wamekuwa wazito sana wa kuyapigania mageuzi wanayoyataka na kuwaachia wenzao wachache na wao kubakia kunung'unika tu kila uchao.
Nadhani na wewe uungane nasi kuwapigania watanzania hawa kivitendo, usiishie kuandika makala za kuilaumu Chadema tu bali uingie kilingine kupigana nasi bega kwa bega na historia itakukumbuka sana kwakuwa tunaokukumbuka enzi zile za mambo ya kitimoto and the likes tunatamani kukuona ukitoa chagizo lile kwa mara nyingine.

Zipo njia nyingi za chama kuwasiliana na wananchi/wanachama/wapenzi wake mojawapo ambayo ni ya haraka na effective ni kupitia maandamano na mikutano ya hadhara. Maandamano na mikutano ya hadhara inafanyika ikiwa ni mbinu mojawapo ya kutekeleza mikakati fulani iliyopangwa na wakati kama huu ni muhimu kutumia fursa ya vurumai zilizotokea bungeni kuwafahamisha ukweli wa mambo jinsi ccm kupitia kiti cha spika ''wanavyobaka'' kanuni za bunge.
 
Last edited by a moderator:
kikubwa si kuongozwa na hisia za kichama.tanzania ni zaidi ya vyama.makinda kapoteza umakini amebakia kuweweseka.lkn huwezi kumuondoa kwa kutumia cdm.tunahitaji mambo ya kitaifa yashughulikiwe na taifa zima.ubinafsi na kuvitukuza vyama ni kasumba na tutaendelea kuishuhudia ccm ikiongoza dola
 
Mkuu Tuko, nimekusoma kuhusu, maandamano nchi nzima!, jee hiki ndicho Watanzania wanachokitaka kwa 2015?.

Nilidhani its high time kwa Chadema not to concentrate kueleza kile ambacho CCM haikufanya for the past 50 years, bali kile ambacho Chadema itafanya ili ichaguliwe 2015!.

Pasco.
kile ambacho CCM haihafanya for 50 years ni pamoja na kuzuia sauti za wananchi kutetea nchi yao kupitia bunge. CDM kuandamana kumpinga spika ina maana kuwa wanawasaidia watanzania wafaidi thamani ya mabilioni ya kodi zao zinazotumika kuendesha mhimili huu wa nchi.
Pili, CDM kuandamana kumpinga spika ni juhusi za kurescue fursa yao ya kutumia jukwaa la bunge kuwaeleza wananchi itafanya nini beyond 2015 ambacho CCM haijafanya kwa miaka 50. Kwa namna bunge linavyoendeshwa sasa CDM imepokonywa fursa ya kutumia jukwaa la bunge kujitangza.
Bw Pasco utakubaliana nami kuwa mic za bungeni zilisaidia sana kupaaza sauti kuhusu EPA, Richmond, BOT twin towers, Mramba+Yona+mgonja, mabilioni ya uswis, ngeleja+mhando+tanesco, twiga wa kia, mgao wa umeme na madudu mengi mengine.
Serikali ya CCM kupitia kwa Makinda na Ndugai wamezima mic za bunge kwa hiyo wananchi hatutapata tena nafasi ya kutetea nchi yetu kupitia bunge.
Je, Mr Pasco, tukae kimya?
 
Mkuu, BAK, nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%, kuna swali nimeuliza, na ninaendelea kuuliza na kuuliza na kuuliΩa tena!, bunge ni uoza, CCM ni uazo, serikali ni uoza!, tumewaambia Watanzania kuhusu uoza wote huu tangu 2010 mpaka leo 2013, bado tunaendelea tuu kuandamana na kufanya mikutano nchi nzima kuelezea kuhusu uoza huu na ule?!. Jee hayo ndio mahitaji ya Watanzania kwa sasa kuelekea 2015?!. Kama mpaka leo tunaendelea kulaumu tuu na kulalamika, lini mtawaeleza Watanzania, nini Chadema, mtawafanyia nini?. CCM imefanya madudu for the past 50 years!, jee kazi ya Chadema ndio hii tuu ya kuendelea kuyapigia makele madudu ya CCM?!, ni lini sasa mtaanza kueleza kile ambacho nyinyi Chadema inaweza kukifanya ili tuwaaminiye tuwape nchi 2015?!.

Kama mnaamini maandamano na mikutano ya kulaani na kulaumu ndicho Watanzania wanachohitaji kwa sasa kuelekea 2015, then its fine, endeleeni kuandamana na kufanya mikutano nchi nzima halafu subirieni CCM ishinde tena na nyinyi muendeleze maandamano na mikutano nchi nzima hadi 2020, na 2025, na 2030 and on and on and on kama alivyosema Mkuu Le Mutus!.

Pasco.
Pasco unataka CDM iwaambieje watanzania kuhusu itakachowafanyia siku wakiipa madaraka? Kupitia sms au email?
Mi naamini bunge ni media muafaka na kwa vile wamwnyimwa kusemea huko, wanaenda kusemea kwenye mikutano. Au?
 
Pasco kadri ninavyokusoma katika posts na threads mbalimbali natambua kiu yako ya kutaka mabadiliko ya haraka. Lakini Pasco tunakubaliana kuwa watanzania wenzetu hawa wamekuwa wazito sana wa kuyapigania mageuzi wanayoyataka na kuwaachia wenzao wachache na wao kubakia kunung'unika tu kila uchao.
Nadhani na wewe uungane nasi kuwapigania watanzania hawa kivitendo, usiishie kuandika makala za kuilaumu Chadema tu bali uingie kilingine kupigana nasi bega kwa bega na historia itakukumbuka sana kwakuwa tunaokukumbuka enzi zile za mambo ya kitimoto and the likes tunatamani kukuona ukitoa chagizo lile kwa mara nyingine.

Zipo njia nyingi za chama kuwasiliana na wananchi/wanachama/wapenzi wake mojawapo ambayo ni ya haraka na effective ni kupitia maandamano na mikutano ya hadhara. Maandamano na mikutano ya hadhara inafanyika ikiwa ni mbinu mojawapo ya kutekeleza mikakati fulani iliyopangwa na wakati kama huu ni muhimu kutumia fursa ya vurumai zilizotokea bungeni kuwafahamisha ukweli wa mambo jinsi ccm kupitia kiti cha spika ''wanavyobaka'' kanuni za bunge.
Mkuu Mwita Maranya, asante nimekupata, nimeguswa, na sasa ninajitafakari, nikikata shauri, utajua tuu!.
Pasco.
 
Mwanamke mpumbavu huivunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe mwache BINTI KINDA aivunje CCM kwa mikono yake mwenyewe

Tabia ya huyu mama na jinsi anavyoendesha bunge sio ya kawaida; nahisi ana stress kutokana na kufiwa na baba watoto wake hivi karibuni ndio maana anakuwa irrational!!
 
Back
Top Bottom