Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,346
- 9,846
Kwanza kabisa walaumiwe walioliharibu Bunge...hapa list ni ndefu ila Spika Ndugai hawezi kukwepa hizi lawama, pamoja na Polepole, Bashiru, Mwendazake, n.k
Hawa wamesababisha majadiliano yaliyopaswa kufanyika bungeni yafanyike mtaania...
Na hili ni tatizo maana mijadala ya mitaani ni unguided, uninformed na endless...
Nimeligusa hilo hapo juu kidogo maana kimsingi ndio lililozalisha huu mjadala wa 'mikopo na nchi kupigwa mnada' kati ya Rais Samia na Spika - Ndugai.
Nitagusia kidogo huu mjadala kisha nitamalizia na athari zake kwa imani ya wananchi juu ya watu wanaowaongoza.
1. Deni letu la taifa lina usiri mkubwa sana. Hapa Nape aliwahi kusema kuna haja ya kulifanyia 'audit' na kutafuta thamani ya fedha kwenye miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea. Hoja hii ikawa chungu kuliko 'mbilimbi' na mara moja ikazalisha timu ya 'wahuni' na 'viroboto'. Kama kawaida hoja ikageuka kioja na baadae ikafa kifo cha kawaida..japo umuhimu wa hoja yenyewe utaendelea kuwa hai.
2. Mama Samia ameongelea 'concession loans' zitakazoanza kulipwa baada ya miaka 20. Ukweli ni kwamba;
● Baada ya hiyo miaka 20 mama hatakuwa madarakani na hivyo sio yeye atakayelipa hayo madeni. Najua pia na yeye analipa madeni ya nyuma...HAPA...hapa ni pakiangalia sana. Utaratibu wa kiongozi kutengeneza tatizo leo litakalokuja kuonyesha makali wakati hayupo madarakani sio utaratibu mzuri kwasababu haya matatizo yatakua juu ya wananchi na vizazi vyao.
● Rais atakayekuwepo baada ya miaka 20 atahitaji pia kufanya miradi ya maendeleo kutokana na uhitaji wa jamii wakati huo, je itakuwaje? Miradi inayotegemewa kulipa hii mikopo ni pamoja na Ule wa umeme wa bwawa la Nyerere ambao kwakweli nina mashaka nao sana.. mvua ikigoma pale tutavuna tu kambale ambao sidhani kama watalipa deni. Kuna ule mwingine wa Shirika la Ndege ulioanza kuingiza hasara kabla hata haujaanza..big doubt!
3. Kauli ya Ndugai kwamba hii nchi itapigwa mnada.. hii ni alert kubwa sana kutoka kwa kiongozi wa mhimili wa bunge. Hii ni kengele ya hatari.
Ila kama kuna viongozi wa ajabu nchi hii nadhani Ndugai amewazidi wote.. yeye binafsi ameitia nchi hasara, misimamo yake imekuwa ikitegemea hali ya hewa ya siku hiyo. Huyu ameshiriki kugeuza bunge kuwa kituko na kutengeneza msingi wa maamuzi mabovu mengi ambayo mwendazake aliyafanya. Wakati wote deni linakuwa alikuwa akiangalia na kukaa kimya... leo miradi iko katikati ya utekelezaji na uchumi ukiwa umeyumba vibaya, anataka wananchi watozwe ili kuikamilisha... sasa sijui watatozwa nini??
Yote kwa pamoja, majibizano ya 'titi for tati' kati ya rais na spika wa bunge hayana afya kwa ustawi wa taifa...
Haya majibizano yanapeleka ujumbe kwa wananchi kuwa jikoni mambo sio mazuri. Eee..na sio mazuri kweli.. kama wapishi wanasema chakula kimeungua, basi yawezekana kweli kimeungua..
Mitaani watu wanachagua upande.. kuna wale wanaomsupport mama na kuna wagalilaya walio upande wa mwenzao..
Mwisho wa haya mabishano mtaani ni kufa kwa imani ya wananchi dhidi ya viongozi wao...hence..Anarchy!!