Ni lini Spika Job Ndugai atajibu tuhuma za yeye na Wabunge kuhongwa Pesa na serikali ya Magufuli ili kupitisha miswada mibovu ya sheria kandamizi?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
85,613
2,000
Mh Mbowe katika hotuba yake kwa Taifa pamoja na mambo mengine mengi aliyoyazungumza, pia alizungumza kwa msisitizo sana jinsi Bunge la Tanzania lilivyogeuzwa kuwa Muhuri wa kupitisha Sheria mbovu za ukandamizaji pamoja na kuunga mkono bajeti za serikali zenye makando kando.

Mbowe alitamka bila kumung'unya maneno kwamba Spika na Naibu wake waligeuzwa kuwa Watumishi wa serikali kwa kulazimishwa kuhudhuria kila hafla ya Magufuli , kama haitoshi Mbowe aliendelea kusema Spika na Wabunge wa CCM walihongwa pesa taslimu ili kupitisha bajeti na miswada ya hovyo , huku akisema anao ushahidi wa jambo hilo na akiombwa atauweka hadharani bila shaka yoyote ile

Sasa swali langu dogo ni hili, ni LINI JOB NDUGAI atajitokeza hadharani kukanusha hili ama kulitolea ufafanuzi?
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
29,557
2,000
Sasa ni wakati mzuri wa kuisambua Rubber Stamp Parliament ya Mwendazake ikiwezekana Uchaguzi urudiwe.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
47,262
2,000
Ndugai ni takataka kabisa huwa sitaki hata kusikia sauti yake, wagogo wamekosa kabisa mtu?
 

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
3,869
2,000
Mambo ni mengi muda mchache...!

Huyu Mbowe atoe tu ushahidi kwani anataka nini. Eti mpaka aombwe Mfyuuu zake
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
105,139
2,000
Nadhani kama watanzania tusisubiri yeye apange ni wakati gani bali tumlazimishe kupitia kwenye majukwaa mbali mbali .
 

nygax

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,302
2,000
Sheria kandamizi huwaathiri wananchi wengi wakawaida. Hivi ni hawahawa wanachi ambao walijitokeza kwa wingi(pengine haijawahi kutokea) kumsindikiza hayati JPM ktk safari yake ya mwisho ndiyo waliogandamizwa na sheria za awamu ya tano? Kama ni kweli kwamba watanzania hawa waliomsikitikia kwa kiwango kile ndiyo wanaogandamizwa na sheria hizo basi tunasafari ndefu sana mkuu.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
51,905
2,000
1618302414332.png
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom