Maandamano ya CHADEMA Arusha: Mabomu yarindima, raia wauawa na viongozi wakamatwa

JK nchi imemshinda anaogopaaa kivuli cha pipo pawa!!...kila kitu wanasingiziaa intelijensia wamekuwa. Watabiri siku hizi....kazi kweli kweli...anajuta heri angekubali kuachiaa urais awe one term president angekuwa na title pekeee
 
OMBI LANGU KWA WATAKAOKUWEPO KWENYE MAANDAMANO:

Kama utafika hapo na itakuwa vema viongozi wa CHADEMA wakaambiwa kabisa kuwa lazima ziwepo Camera, Video camera za kutosha kupiga picha kila tukio la ajabu. Pia watu waandae kabisa simu zao tayari kupiga picha.

Wasiwasi wangu mie ni kuwa isijetokea baadhi wa ya wapinzani wa Chadema, wakaanza kurusha mawe kwenye nyumba za watu au biashara zao au mali nk nk na hapo ije isemwe ni Chadema.

Pia kama itatokea FFU au POLISI au hata jeshi wanaanza kupiga watu, basi matukio yote yawe yamerekodiwa kwa wingi na hapo miaka ya mbeleni yaje yatumike kuwapandisha hawa akina Charles Taylor wa Tanzania.
 
Wana jf baada ya RPC wa Arusha kuruhusu CHADEMA Kufanya maandamano ya amani na mkutano wa hadhara kesho IGP Mwema ameitisha mkutano na waandishi wa habari na kukataa maandamano. Source taarifa ya habari chanel ten saa moja ucku.

Kwa sababu zipi???
 
Iv ikitokea Watu wengi kwa pa1 kama coinsidence wawe wanaenda kwenye huo Mkutano Je itakuwa ni Maandamano!!Wana Arusha nendeni kwa Staili hiyo tuone hao police watafanya nin coz hayo c Maandamano bali Wananchi wapo njia moja kwenda Mkutanoni.
 
We are cowards that's why we cannot even fight for our true rights, wanasema eti tuishie kwenye mazungumzo, YAPI na YANINI?
Don't generalize bhana if ua coward ua the only one.Mimi na familia yangu tushaanza maandamano siku nyingi saiv nafanya mpango wakujitengenezea nishati yangu mwenyewe ya Umeme.
 
Nawaomba ndugu zetu wa Arusha kwa sababu mmepata fursa hiyo, wakilisheni hasira za watanzania kuhusu malipo ya kifisadi yanayotaka kufanywa na hawa mahafizina.... Jk kanitoka rohoni mwangu hadi kichefuchefu..
 
MKuu,
Arusha inazizima leo.
Kwa habari ya matangazo, wamezunguka mji mzima kuwaandaa wananchi kwaajili ya maandamano hayo...
Naamini itakuwa ni patashika, maana raia wa hapa huwaambii kitu juu ya Mbunge kipenzi chao, G.Lema..
 
POLISI imeruhusu kufanyika kwa mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha leo, huku ikizuia maandamano ya aina yoyote.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jioni, Mkuu wa Polisi, (IGP) Said Mwema, alisema amezuia maandamano hayo baada ya kupata taarifa za kiintelejinsia kuwa yangesababisha vurugu na uvunjifu wa amani.

Alisema kabla ya uamuzi huo, Chadema iliomba kibali cha kufanya maandamano na mkutano huo leo na kuruhusiwa lakini baada ya uchunguzi ameamua kuzuia maandamano hayo ili kuepusha vurugu ambazo zingeweza kujitokeza.

"Polisi inaendelea kukusanya taarifa za tishio hilo na mengineyo yanayohatarisha uvunjifu wa amani na yanayofanana na hayo kwa lengo la kuhakikisha utulivu kwa wananchi wote unakuwepo," alisema IGP Mwema.

Alifafanua kuwa Polisi haina nia ya kuzuia kufanyika kwa maandamano ya aina yoyote, kwa kuwa yapo halali kisheria lakini uamuzi huo unatokana na dalili za kutokea kwa fujo.

Alisema pamoja na kuruhusu mkutano huo, Polisi itaimarisha ulinzi wa kutosha tofauti na kawaida ili kuhakikisha utulivu na amani vinatawala wakati wote wa mkutano huo.

"Tunawaomba wazazi wasiruhusu watoto wao kuingia katika mikusanyiko mitaani ambayo kimsingi inaweza ikawaletea madhara kutokana na hali iliyopo kwa sasa wakati huu ambao kuna tishio, bado tunaendelea kufuatilia kujua undani wake,"alisema IGP Mwema.

Source Habarileo
 
Katika kukabiliana na maandamano ya wana- CDM jijini Arusha,kuna taarifa kuwa polisi wanapelekwa kwa wingi mkoani humo hasa kutokea Moshi.chanzo changu cha habari kinathibitisha kuliona basi la Police academy moshi likiwa limejazwa polisi waliovalia magwanda.tusubiri tuone sakata hili!
Nawasilisha...
 
mnafiki huyo mwema na mungu amlaani, kama kungekua kuna uwezekano wa kulishtaki jeshi la police ingekua safi sana, hebu fikiri watu wamejiandaa kufanya maandamano ya amani halafu mwishoni unaahirisha. Huo ni usaliti na hakuna demokrasia ya kweli hapo.
 
Dk. Slaa kuongoza maandamano Arusha leo

na Janet Josiah

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa pamoja na viongozi wengine, leo anatarajia kuongoza maandamano na mkutano wa hadhara mkoani Arusha kupinga unyanyaswaji na ubakwaji wa demokrasia unaofanywa na vyombo vya dola hasa Jeshi la Polisi.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Dk. Slaa alisema maandamano hayo yatakuwa na ujumbe tofauti tofauti kuieleza serikali namna vyombo hivyo vya dola vinavyokiuka sheria na hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi wa mameya wa halmashauri.

Alisema maandamano na mkutano huo utaelezea mambo yote yanayoendelea katika halmashauri za Hai, Mwanza na Arusha kuhusu umeya; yatazungumzwa ili kuwapa Watanzania na serikali hali inayoendelea.

"Lengo kubwa la maandamano ya amani na mkutano mkubwa wa hadhara ni kutaka kuwaelezea Watanzania na serikali, machafu yahusuyo unyanyaswaji wa demokrasia katika uchaguzi wa mameya unaoendelea.

"Suala la kuandikwa kwa Katiba mpya na kitendo cha kinyama cha kumshambulia na kumuumiza hadi kulazwa hospitali mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, uliofanywa na askari polisi mkoani humo vitawekwa hadharani" alisema.

Dk. Slaa alisema ingawa katika halmashauri ya Kigoma Mjini tayari kitendawili kimeshateguliwa, bado Watanzania wanahitaji kujua kinachoendelea katika halmashauri nyingine ambazo hazijafanya uchaguzi na kwa nini hakuko shwari.

Alisema kutokana na hali hiyo, wameamua kufanya maandamano ambayo yamepata kibali cha Jeshi la Polisi mkoani humo na baadaye kuwapa taarifa ya kufanya mkutano wa hadhara kwa ajili ya kupatiwa ulinzi.

Hadi sasa halmashauri za mikoa ya Arusha, Mwanza na Hai hazijaweza kufanya uchaguzi wa kuwapata mameya, kutokana na hisia za kuwepo kwa uchakachuaji, kutofautiana juu ya njia za kupiga kura na mbunge wa viti maalum kuteuliwa kupiga kura.

Hata hivyo, uchaguzi kwenye halmashauri ambazo Chama cha Mapinduzi (CCM) kilionekana hakina upinzani, ulifanyika bila ya matatizo ikiwa ni pamoja na manispaa za mkoa wa Dar es Salaam.
 
Polisi yaruhusu mkutano, yazuia maandamano

Imeandikwa na Oscar Job; Tarehe: 4th January 2011

2ij4sk0.jpg

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kuhusu jeshi hilo kuzuia maandamano ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yaliyopangwa kufanyika mjini Arusha leo. (Picha na Fadhili Akida)

POLISI imeruhusu kufanyika kwa mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha leo, huku ikizuia maandamano ya aina yoyote.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jioni, Mkuu wa Polisi, (IGP) Said Mwema, alisema amezuia maandamano hayo baada ya kupata taarifa za kiintelejinsia kuwa yangesababisha vurugu na uvunjifu wa amani.

Alisema kabla ya uamuzi huo, Chadema iliomba kibali cha kufanya maandamano na mkutano huo leo na kuruhusiwa lakini baada ya uchunguzi ameamua kuzuia maandamano hayo ili kuepusha vurugu ambazo zingeweza kujitokeza.

"Polisi inaendelea kukusanya taarifa za tishio hilo na mengineyo yanayohatarisha uvunjifu wa amani na yanayofanana na hayo kwa lengo la kuhakikisha utulivu kwa wananchi wote unakuwepo," alisema IGP Mwema.

Alifafanua kuwa Polisi haina nia ya kuzuia kufanyika kwa maandamano ya aina yoyote, kwa kuwa yapo halali kisheria lakini uamuzi huo unatokana na dalili za kutokea kwa fujo.

Alisema pamoja na kuruhusu mkutano huo, Polisi itaimarisha ulinzi wa kutosha tofauti na kawaida ili kuhakikisha utulivu na amani vinatawala wakati wote wa mkutano huo.

"Tunawaomba wazazi wasiruhusu watoto wao kuingia katika mikusanyiko mitaani ambayo kimsingi inaweza ikawaletea madhara kutokana na hali iliyopo kwa sasa wakati huu ambao kuna tishio, bado tunaendelea kufuatilia kujua undani wake,"alisema IGP Mwema.
 
Sidhani kama polisi wataweza kuzuia peoples power.inaovyoaminika waandamanaji watatokea kona zote za mji.
 
Justice is like NATURE, it awaits nothing!

There is always the rise and fall of everything, every body,... but never JUSTICE!
 
unafiki tu na hofu ndio inayowasumbua, masikini wanahangaika na bado kiama chao kipo karibu mkwere hata maliza miaka 5 kwa amani.a
 
Nani atakayeweza kulifunika jua na ungo hata lengo lake likafanikiwa??? CHADEMA juu kwa juu leo mpaka kieleweke Arusha.
 
Wana-Jf mlioko ndani ya jeshi la polisi na nyinyi mlioko Ikulu, Dar Makao Makuu, Mombo, Moshi na Monduli hebu leteni nyepesi nyepesi jamvini kuli yanapojiri.

Hi Said Mwema aliweza kupata mzigo wa Ma-Bomu ya kutoa machozi kwa wakati na idadi itatosha au hapa?? Kwetu sisi hapa nyepesi nyepesi ni kwamba mikutano yetu katika vitongoji mbalimbali Arusha ilifanikiwa sana na maandamano ya leo ni ngoma uwanjani kabisa.

Vyombo vya habari vya kimataifa navyo walifika tangu siku tatu zilizopita.
 
Back
Top Bottom