Maandamano ya CHADEMA Arusha: Mabomu yarindima, raia wauawa na viongozi wakamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ya CHADEMA Arusha: Mabomu yarindima, raia wauawa na viongozi wakamatwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtego wa Noti, Jan 4, 2011.

 1. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Leo Chadema wameanzisha maandamano ya amani Arusha kupinga uchaguzi wa meya wa Arusha ambao haukufuata taratibu sahihi. Maandamano haya ni baada ya kupewa kibali na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha, Kamanda Andengenye.

  Hata hivyo jana jioni IGP Mwema alifuta kibali hicho cha kuandamana kutokana na kile alichokiita taarifa za ki-intelijensia kwamba kutakuwepo na uvunjifu wa amani katika maandamano hayo. Pamoja na amri hiyo ya mkuu wa jeshi la Polisi, wananchi wengi wlijitokeze kuandamana hapo Arusha kitendo kilichopelekea polisi kurusha mabomu pamoja na risasi za moto hata uwanjani Unga Limited Habari za kuaminika zinasema kuwa Viongozi wa juu wa Chadema wamekamatwa na wako chini ya ulinzi wa polisi. Aliyekamatwa ni Mwenyekiti wa chadema Mh. Mbowe, Mbunge wa Arusha Mh. Lema na Mbunge wa Rombo Mh. Selasini.  My take...
  Tutaandamana mpaka kieleweke!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  We are cowards that's why we cannot even fight for our true rights, wanasema eti tuishie kwenye mazungumzo, YAPI na YANINI?
   
 3. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  mi hasira zishanipanda maana huu upuuzi umezidi...hao chadema mbona hawatupi modality?????????????????
   
 4. m

  matshs Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 53
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  ukiona hivyo ujue mgaya bado wanamchakachua na kibali cha kuruhusu maandamano
   
 5. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  na hii itaifanya hiyo tume ya jk itutengenezee katiba kwa maamuzi yao wenyewe...
   
 6. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  huyo mgaya ni kiboko, hao chadema nao vipi? mbona wametuambia wanaandaa maandamano ya nchi nzima...inakuwaje!!!
   
 7. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Hata mimi nayasubiri kwa hamu. Tutanyamazia upuuzi hadi lini???
   
 8. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hivi kweli... hii issue imekaaje na nilisikia na wafanyakazi nao watakuwa na maandamano ya kupinga umeme..... kweli kuna sababu ya kushirikiana kwenye hii issue na kuonyesha kutokuridhika kwetu.....
   
 9. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Chadema yaandaa maandamano kupinga bei mpya ya umeme

  Hussein Issa na Eveline Kijumbe

  CHAMA Cha Demokrasia (Chadema), kimeandaa maandamano makubwa nchi nzima kupinga bei mpya ya umeme iliyotangazwa Desemba 20 mwaka huu na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura).

  "Tutawaunganisha wanachama wetu wote wa mikoani tujumuike pamoja katika maandamano hayo ili kudai haki zetu za msingi, "alisema Mkurugenzi wa Oganization na Mafunzo wa Chadema, Singo Kigaira.


  Kigaira aliwataka wafuasi wa chama hicho, wanachama na wananchi kuacha woga akieleza kuwa kila kitu kinahitaji mipango na katika maandamano hayo, kiongozi wa mipango hiyo ni Chadema.


  Awali akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Habari wa Chadema, Erasto Tumbo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa chama hicho kimeamua kuandaa maandamano hayo baada ya kutambua kuwa bei hiyo mpya ya umeme inamwumiza mwananchi wa kawaida.


  "Maandamano hayo tutayafanya mwezi Januari na tutaomba wananchi watuunge mkono kwa sababu hii ni haki ya msingi. Hakuna sababu ya kuonewa hapa. Junuari tutatangaza siku maalumu ya maandamano hayo,"alisema Tumbo.


  Aliendelea "Katika hali ya kawaida kabisa, mtu anakuwa na matumizi ya Sh1000 kwa siku, leo hii unampandishia umeme kwa asilimia 18.5, unadhani maisha yatakuwa rahisi kweli?"


  Kwa mujibu Tumbo, Serikali ingeweza kutumia njia nyingine mbadala kuboresha upatikanaji wa umeme nchini bila kuwapandishia wananchi bei ambao kimsingi ni mzigo kwao  Tucta kuandamana siku yoyote kuanzia kesho
   
 10. Wikiliki

  Wikiliki JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 529
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Chama cha CHADEMA kitafanya maandamano kesho Arusha(yameruhusiwa na polisi) yataongozwa na Dr. Slaa,pia wabunge wote wa CDM watakuwepo pamoja na madiwani wote wa Arusha mjini watakuwepo. Yataanza saa tano asubuhi eneo la Philips na kuishia uwanja wa NMC.
   
 11. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Good je na maandamano ya kupinga kupanda kwa umeme yanafanyika lini?
   
 12. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,986
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa

  Kama alivyosema rafiki yetu Waberoya kwenye thread nyingine, kwenye speech yako kuhusu Dowans endelea kupiga kichwa (JK) na si mkia (RA/EL).

  Tuko nyuma yako....iwe mvua liwe jua!!
   
 13. k

  kev Senior Member

  #13
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tuko pamoja meya feki kesho atafute pa kwenda kesho arusha meya wa wananchi.pipoooooo pawa
   
 14. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Lengo litakuwa ni nini? Basi kila raheli Chadema
   
 15. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  kila la heri wanaharakati wote waliopo arusha, na pia msiache kututaarifu kwa kutu update mambo yatakavyokwenda. Asanteni sana.
   
 16. Wikiliki

  Wikiliki JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 529
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wana jf baada ya RPC wa Arusha kuruhusu CHADEMA Kufanya maandamano ya amani na mkutano wa hadhara kesho IGP Mwema ameitisha mkutano na waandishi wa habari na kukataa maandamano. Source taarifa ya habari chanel ten saa moja ucku.
   
 17. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  ni muhmu kuunganana kundamana kwa nguvu zote...lakini polisi wamekataa hata hayamaandalizi mabaya ya arusha...
   
 18. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Sasa anakataa nini IGP? Ilichobaki ni Chadema kuingia tu barabarani. Huu niupuuzi mtupu! Mwaka huu lazima watahaha sana CCM na serikali yao... ila wajue hawana wapenzi siku hizi ni watu wenye vested interests na they will abandon the ship very soon...
  Polisi hawana nguvu ya kisheria kutoa kibali chochote cha maandamano.. wao wanatoa tu ulinzi.. wakishindwa wakae pembeni...
   
 19. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  ndio maana tunashindwa kupata haki zetu maana kila maandamano eti lazima turuhusiwe na polis,katiba ibadilishwe tuwe tunaadamana tu bila hata hicho kibali labda taarifa tu!!!
   
 20. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  utahimili virungu vya hawa jamaa? maana wanatwanga hasa...
   
Loading...