Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,792
- 71,206
Uko sahihi mkuu, vielelezo hivyo vitamsaidia sana Ocampo kama itabidi hapo baadae maana naona viongozi wetu wanataka wafungiwe The Hague kwa kukiuka haki za binadamu na sio Ukonga kwa ufisadi mwaka 2015. Wamegundua jela za huko zina nafuu kuliko hizi wanazoziendesha wao sasa.OMBI LANGU KWA WATAKAOKUWEPO KWENYE MAANDAMANO:
Kama utafika hapo na itakuwa vema viongozi wa CHADEMA wakaambiwa kabisa kuwa lazima ziwepo Camera, Video camera za kutosha kupiga picha kila tukio la ajabu. Pia watu waandae kabisa simu zao tayari kupiga picha.
Wasiwasi wangu mie ni kuwa isijetokea baadhi wa ya wapinzani wa Chadema, wakaanza kurusha mawe kwenye nyumba za watu au biashara zao au mali nk nk na hapo ije isemwe ni Chadema.
Pia kama itatokea FFU au POLISI au hata jeshi wanaanza kupiga watu, basi matukio yote yawe yamerekodiwa kwa wingi na hapo miaka ya mbeleni yaje yatumike kuwapandisha hawa akina Charles Taylor wa Tanzania.