Maandamano ya CHADEMA Arusha: Mabomu yarindima, raia wauawa na viongozi wakamatwa

Duh..kumbe ndio mnatoa hapa;

Kumbe Assumsption ni kuwa: Vote turn-out ilikuwa almost 100%(Big NO)
Kikwete Alipata kura: 5,000,000 kati ya kura 18,000,000 zilizopigwa ambayo ni 27%;
Katika 12,000,000 ambao hawakupiga kura, imekadiriwa Dr. Slaa alipata 9,500,000, hivyo ukijumlisha na kura 2,000,000 alizopata ana 64%

Ndizo data zenu hizi?great thinkers??
Je kwenye hizo data unachopinga hasa ni nini ?

Mie nilidhani data kama hizi ni wafuta bange pekee ndio wanaoweza kukubali makasa kama haya; kumbe ata wasomi wazima wenye akili timamu nao wanaingia tu kichwakichwa? sasa naamini kuwa Watanzania tuna matatizo makubwa kuliko tunavyodhani, wake up men!!

Mtu yeyote aliyeshiriki au kuufuatilia upigaji kura katika uchaguzi ule, atakubali bila ya shaka kuwa turn-out ilikuwa ni less than 50%; tusiongeeongee vitu kama watu wasio sawa kichwani
Kwa kuwa wewe uko sawa kichwani, ni kitu gani kilisababisha turn-out kuwa less than 50% ? Ninavyojua mimi nisiye sawa kichwani turn-out ilikuwa kubwa tu.
 
CCM bado hawajajua what Arusha is, 10 dead, Arusha haijawahi tokea, revenge u will see, man to man, si Arusha, sijui polisi wataishi Central,
 
Ndugu wananchi tuache jazba na hamaki!! damu ya watanzania wenzetu Polisi na Raia imemwagika!!! wakati huu si wakati wa kuchochea chuki na kuropoka kila kinachotoka mdomoni matokeo yake ni kupalilia chuki na kuzidisha machafuko huku wanaoathirika ni binaadamu wezetu!!

Huu ni wakati wa kutuliza bongo na kupunguza hamasa ili hasira za wananchi zisizidi mipaka na tuiombee nchi yetu Amani kwani hakuna kitu muhimu zaidi kwa sasa kuliko utulivu! tukizidi kuchochea chuki na hasira ndugu zangu tutajikuta tunaingia ktk kapu waliloingia majirani wenzetu wa Kenya, Rwanda, Burundi, Somalia nk!!!

Hasa JF great thinkers nawaomba tuache JAZBA na Katu tusichochee moto! wengi wa JF hawako Bongo wako Ulaya na Marekani! kauli zenu zitasababisha machafuko ya kisiasa na mwisho wake ni mbaya kwani utabadilika kuwa wa kisiasa na kuwa wa kidini na kikabila!!!

Mimi nalaani mauaji haya bila kujali alieuwawa ni Polisi au Raia lakini kwa sasa natanguliza Amani kwanza halafu sheria ije baadae!!!
 
Poverty and low growth are often symptoms of corrupt, incompetent government, which can give people a reason to rebel however, you people, as long as my fellow Tanzanians have lost their live unnecessarily, I will denounce this. Both politicians and Police should act on this. I feel sorry that things have gone that far especially in one of peaceful and beautiful cities in Tanzania with lots of natural attractions, this unrest has negative impacts to both our peace and economy that is why I say you should do something.
 
Nafikiri viongozi walioamrisha haya wapelekwe The hague,, Itapendeza kama kama hati za kukamatwa kwao zitatolewa wakiwa madarakani ili hata safari zao nje ya nchi wasitishe kama ilivyo kwa Rais wa Sudan
Kwa mtazamo wangu nguvu kubwa iliyotumika kusambaratisha maandamano ingetosha kabisa kudhibiti hilo tishio la uvunjifu wa amani kama zile taarifa za kiiteligensia zilikuwa na ukweli. Katika hali ya kawaida IGP lazima alikuwa na taarifa kamili kuwa uvunjifu huo ungetokea wapi, na mchakato wake ukoje, kama wahusika walikaa kikao cha siri, au walipanga kwa njia ya simu nk, hivyo kuwadhibiti watu wenye lengo hilo alikuwa hahitaji makachero zaidi ya 10.
 
Dk Slaa atangaza maandamano nchi nzima Wednesday, 05 January 2011 21:06

eeslaa.jpg

Dk Willibroad Slaa.

Mussa Juma na Moses Mashala, Arusha
Mwananchi

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kufanya maandamano nchi nzima, kupinga utendaji wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete na ukiukwaji wa taratibu katika chaguzi mbalimbali.

Akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara jana katika viwanja vya NMC mjini Arusha, ambao ulihitimishwa kwa vurugu kubwa na mabomu baada ya wananchi kutaka kwenda kuvamia kituo kikuu cha polisi kwa lengo la kuwatoa wabunge waliokuwa wanashikilia, Dk Slaa alisema sasa wamesitisha mazungumzo ya aina yoyote na serikali ya Kikwete.

"Tumevumilia sana, sasa inatosha...tunataka serikali ya Kikwete isitawalike tena kwani haki hakuna... Tunaomba Jumuiya za Kimataifa zituelewe...Uchaguzi uliopita matokeo yalichakachuliwa tulikaa kimya, lakini sasa basi,"alisema Dk Slaa.

Alisema kitendo cha polisi kujiingiza katika siasa na kukataza mara kwa mara mikutano na maandamano ya Chadema, ni moja ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

"Leo polisi wamemwaga damu, wamekamata hadi wabunge akiwemo kiongozi wa upinzani bungeni (Freeman Mbowe)..Jambo hili lazima likomeshwe,"alisema Dk Slaa.

Dk Slaa, mgombea wa Urais uliopita kwa tiketi ya Chadema, alisema haridhishwi na utendaji wa Rais Kikwete na vyombo vyake kama polisi na wizara mbali mbali.

"Maisha ya watanzania bado ni magumu...serikali inapandisha bei ya umeme...hawataki kutueleza Dowans kwanini walipwe,...tumechoka na lazima wananchi sasa tuamke,"alisema.

Katika mkutano huo, Dk Slaa alilaani kitendo cha kukamatwa wabunge na kupigwa hadi kujeruhiwa wa wananchi, huku akiwasimamisha majeruhi hao jukwaani wakati alipokuwa akihutubia.

Diwani CCM ahamia Chadema
Katika mkutano huo, diwani maarufu wa CCM wa kata ya Sombetini, Alfonce Mawazo alitangaza kujiondoa katika chama chake na kujiunga na Chadema kwa kile alichoeleza kuwa amechoshwa na ukatili wa CCM.

Mawazo ambaye alihamia CCM mapema mwaka juzi akitokea TLP alipokuwa pia diwani wa kata hiyo, alisema amekuwa akiunga mkono sera mbali mbali za Chadema zikiwemo sera binafsi za aliyekuwa mgombea wa Urais wa chama hicho, Dk Willibroad Slaa.

"Naomba niwaeleze wazi kuwa hata katika uchaguzi mkuu mimi ingawa nilikuwa mgombea wa udiwani wa CCM, nilimchagua Dk Slaa,"alisema Mawazo.

Hadi jana jioni vurugu kubwa zilikuwa zinaendelea, huku polisi kadhaa waliokuwa wanawatawanya wananchi, wakipigwa na majengo, kadhaa ya CCM, yaliharibiwa.

Mapambano ya polisi na raia yalilipuka upya yakianzia kwenye mkutano wa NMC pale wananchi walipoonyesha nia ya kwenda polisi kuwakomboa wafuasi wa Chadema waliokamatwa jana mchana wakati wakiandamana.

Polisi wazidiwa, waomba msaada

Katika kile kilichodhihirika kuwa ni polisi kuzidiwa nguvu, kundi la askari liliondoka jana usiku katika chuo cha polisi (CCP) mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro kwenda mjini Arusha kuongeza nguvu za kuwadhibiti Chadema.
Askari hao wanafunzi ni wa awamu ya pili, wakilifuatia kundi la wenzao wanaodaiwa kuwa zaidi ya 50 ambao waliondoka CCP Moshi jana saa 11 alfajiri kwenda mkoani Arusha ambako kulizuka vurugu kubwa huku baadhi ya wananchi wakijeruhiwa.
 
Ndiyo tatizo la kuongozwa na mswahili, mnywa kahawa na kashata, mpenda misifa. Kwake kila kitu ni sawa.
 
Ndugu wananchi tuache jazba na hamaki!! damu ya watanzania wenzetu Polisi na Raia imemwagika!!! wakati huu si wakati wa kuchochea chuki na kuropoka kila kinachotoka mdomoni matokeo yake ni kupalilia chuki na kuzidisha machafuko huku wanaoathirika ni binaadamu wezetu!!

Huu ni wakati wa kutuliza bongo na kupunguza hamasa ili hasira za wananchi zisizidi mipaka na tuiombee nchi yetu Amani kwani hakuna kitu muhimu zaidi kwa sasa kuliko utulivu! tukizidi kuchochea chuki na hasira ndugu zangu tutajikuta tunaingia ktk kapu waliloingia majirani wenzetu wa Kenya, Rwanda, Burundi, Somalia nk!!!

Hasa JF great thinkers nawaomba tuache JAZBA na Katu tusichochee moto! wengi wa JF hawako Bongo wako Ulaya na Marekani! kauli zenu zitasababisha machafuko ya kisiasa na mwisho wake ni mbaya kwani utabadilika kuwa wa kisiasa na kuwa wa kidini na kikabila!!!

Mimi nalaani mauaji haya bila kujali alieuwawa ni Polisi au Raia lakini kwa sasa natanguliza Amani kwanza halafu sheria ije baadae!!!
 
Wananchi Tusiogope Kuandamana Polisi na Jeshi Wanafamilia Kama Sisi Wananchi Wanajua Jinsi Gani Maisha Yalivyo Magumu na Kushindwa Kwetu Kwenda Mbele na Maendeleo. Tuongozane Barabarani Kuwaunga Mkono Wote Waliopigwa na Kuuliwa na JK. "10 Hawajakufa Bure"

"Watanzania Nguvu Tunazo na Nchi ni Yetu"
 
Fight the Power............
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wananchi tuache jazba na hamaki!! damu ya watanzania wenzetu Polisi na Raia imemwagika!!! wakati huu si wakati wa kuchochea chuki na kuropoka kila kinachotoka mdomoni matokeo yake ni kupalilia chuki na kuzidisha machafuko huku wanaoathirika ni binaadamu wezetu!!

Huu ni wakati wa kutuliza bongo na kupunguza hamasa ili hasira za wananchi zisizidi mipaka na tuiombee nchi yetu Amani kwani hakuna kitu muhimu zaidi kwa sasa kuliko utulivu! tukizidi kuchochea chuki na hasira ndugu zangu tutajikuta tunaingia ktk kapu waliloingia majirani wenzetu wa Kenya, Rwanda, Burundi, Somalia nk!!!

Hasa JF great thinkers nawaomba tuache JAZBA na Katu tusichochee moto! wengi wa JF hawako Bongo wako Ulaya na Marekani! kauli zenu zitasababisha machafuko ya kisiasa na mwisho wake ni mbaya kwani utabadilika kuwa wa kisiasa na kuwa wa kidini na kikabila!!!

Mimi nalaani mauaji haya bila kujali alieuwawa ni Polisi au Raia lakini kwa sasa natanguliza Amani kwanza halafu sheria ije baadae!!!

Watu wengine bwana, wewe unakopy na kupaste huu mchango wako kwenye kila thread inayohusu Unyama ulofanyika Arusha. Tumekujibu mpaka tumechoka. Ingekuwa mama yako, dada zako na wadogo zako ni kati ya hao waliouwawa ungetushauri tukae kimya kusubiri mkondo wa sheria?....Kwa sheria ipi?...ni hii ya Tanzania ambayo kila mwenye mamlaka na fedha anaweza kuipindisha kwa maslahi yake?
 
Yaani badala ya kulaani mauaji au kuonyesha hata chembe ya masikitiko..wewe kila mchango unaotoa ni kuonyesha kwamba wa kulaumiwa ni Dr. Slaa.

Well, Inasikitisha..lakini hatuna budi kutambua kwamba wakati wengine wanaogopa hata kuangalia maiti ya binadamu, wapo ambao huchomoa maini katika maiti hizo na kufanya kitoweo. Watu kama nyie ni Kuwakemea kila mmoja kwa imani yake.
 
Watu wengine bwana, wewe unakopy na kupaste huu mchango wako kwenye kila thread inayohusu Unyama ulofanyika Arusha. Tumekujibu mpaka tumechoka. Ingekuwa mama yako, dada zako na wadogo zako ni kati ya hao waliouwawa ungetushauri tukae kimya kusubiri mkondo wa sheria?....Kwa sheria ipi?...ni hii ya Tanzania ambayo kila mwenye mamlaka na fedha anaweza kuipindisha kwa maslahi yake?

Katumwa huyu na mafisadi wenzake ili aifanye kazi hii mtindo mmoja.

Watu wengine bwana, wewe unakopy na kupaste huu mchango wako kwenye kila thread inayohusu Unyama ulofanyika Arusha. Tumekujibu mpaka tumechoka. Ingekuwa mama yako, dada zako na wadogo zako ni kati ya hao waliouwawa ungetushauri tukae kimya kusubiri mkondo wa sheria?....Kwa sheria ipi?...ni hii ya Tanzania ambayo kila mwenye mamlaka na fedha anaweza kuipindisha kwa maslahi yake?

Hakuna ubaya kupaste nasaha muhimu kwa taifa kwani kila thred inayohusu vurugu za Arusha zinaonekana zinafanana kwa wengi kutaka kuchochea fujo na kusababisha machafuko! sasa huu ni wakati wa kuhubiri Amani tena kwa kuikariri kila dakika!! na wewe kama unaipenda TZ utashirikiana na wapenda Amani kinyume chake utakuwa ni miongoni mwa maadui wa nchi yetu wanaotaka nchi isambaratike na sijui ni kwa faida ya nani!!!!
 
Maandamano yaliyofanyika Arusha ambako inasemekana kuna watu wamepoteza maisha...je yaliruhusiwa kisheria na vyombo vya usalama au la?
 
Back
Top Bottom