Hili ndilo tatizo hasa la kuingia mkataba na Ibilisi, anakumiriki mwili na roho, pia kujitwalia uwezo wa kukufanya chochotea kile atakacho.
Mwili wako ni mali ya ibilisi
Roho yako ni mali ya Ibilisi.
Mbele ya Ibilisi huyu hakuna tofauti kati ya tofari na Roho yako
Tumetumia nafasi zetu, haki zetu na akili zetu zote kufanikisha kuiweka CCM madarakani na kuipa nguvu ya kikatiba.
Tumeiweka CCM madarakani kwa;
kuchelea maovu ya utawala wa CCM,
kukubali wito wa CCM wa Kuogopa mabadiliko ya kisiasa,
Kuwaachia wezi wa kura wa genge la kiCCM kutimiza matakwa yao binafsi
Kuhongwa vijikanga na vijiTshirts ili kuuza utu na haki,
Kuyakataa maendeleo kwa nguvu zetu zote na kukubali mfumo wa uliotuweka tena katika utumwa kikoloni ndani ya nchi yetu wenyewe.
Kukumbati mahabithi kwa ujira mduchu huku wao CCM wakifaidika na Kuiza ncho yetu kwa Makampuni ya Kimataifa kama Barick Gold Mines na mengineyo yanayo miriki ardhi yetu kwa nguvu,
Kuhifadhi wala rushwa na mafisadi ili kuendelea kulinda himaya yao watoto wao wajukuu zao na ukoloni mambo leo ulioturudisha tulipokuwa kabla ya Dember, 9 1961.
Ili kuwaondoa CCM madarakani,Tunahitaji zaidi ya mara mbili ya juhudi zilizotumika kuwaweka madarakani.
Sisi Wananchi ndiyo tumewaweka madarakani CCM, ni sisi wananchi tutakao watoa CCM madarakani.
Wananchi tusitegemee shujaa au nabii kutoka juu kuj kuiondoa CCM.
Kuiondoa CCM madarakani ni kazi yetu Namba 1 na muhimu kuliko hata milo yote mitatu ya siku,
CCM wapo madarakani kwa sababu wanachi tunaridhia kuwepo kwao madarani.
Bila ridhaa yetu wananchi CCM hawawezi kuwepo madarakani.
Bila wananchi kuafiki kwa namna moja au nyingine CCM hawawezi kuwa madarakani.
Yawezekana kabisa nia mioyoni mwetu haiafiki CCM kuwepo madarakani,hata hivyo vitendo vyetu,tabia zetu, mienendo yetu na mazoea yetu ya kuamini kila lisemwalo TBC au kutoka kwa viongozi wa serikali yanaafiki CCM kuwepo madarakani.
Ni Pale tu Nia zetu zitapoendena na Vitendo vyetu, zitakapoendena na mienendo na tabia zetu ndipo CCM itapoondoka madarakani na kubaki katika vitabu vya Historia kama Utawala haramu wa Vizuka Makaburu weusi wa Tanzania.
Wananchi tuna uwezo wa kufanya lolote kuleta haki usawa na fursa ya maendeleo kwa wote lakini uwezo huo umekuwa ukigubikwa na woga, unyonge,utengano na hali ya kukata tamaa.
Mnyonge na Mnyonge ni sawa na wenye nguvu kumi.