Maandamano makubwa Songea!

Maandamano makubwa Songea!

Hali ni tete mpaka sasa,ofisi moja ya ccm imebomolewa,baadhi ya huduma za jamii zimefungwa,idadi kubwa ya wananchi ni majeruhi na wengine ni marehemu,watoto wa shule wakimbia hovyo,eti maisha bora kwa kila mtanzania ndio hayo?au amani na utulivu ndio hiyo ya watu kuuwawa?jamani niombeeni mpaka sasa mwanangu hajaonekana naendelea kumtafuta toka alipoenda shule,ni mtoto wa miaka saba
 
polisi sasa wamechoka,wameona watz mpo wa pole sana sasa wameamuwa kuwaua kama njugu kwani hamna haki ktk nchi hii,angalia pale iringa wamempiga risasi kijana wa chuo kikuu na kusema kuwa jamaa ni jambazi ,baada ya kumpiga risasi waka msachi na kumwibia marehemu pesa zake, haya saizi tena wapo songea kazi jamani

nimewahi sema hapa kuwa sisi wa pangu pa kavu kuuliwa na pilisi ni rahisi sana kwani ni swala la wao kusema jamaa ni ri jambazi tumelikuta na mabumu na bunduki,hapo wamepoteza ushahidi

nadhani ya sondea mtasikia tu,kuwa polisi walikuwa wanajihami na majambazi kutoka msumbiji na baada ya kuwasachi wamekutwa na mabumu ya kurushwa kwa mkono,kazi ipo jamani

poleni wana songea ndio maisha tuliyo jichagulia na hawa polisi wetu

jana nilikuwa naangalia ugiriki jinsi walivyokuwa wakiandamana,yaani polisi wanachofanya ni kuwarudisha nyuma waandamanaji na screen zao bila hata kufyatua risasi za moto,lakini tz jamaa ndio wanakojifunzia kuuwa
 
So sad news, RIP marehemu wetu, na walaaniwe hao polisisiem.
 
Kuna jinsi serikali inawasukuma wananchi wafike mahali waseme imetosha sasa hapo lazima itaelewa,maana mi sielewi kabisa matendo yake, pole sana ndugu,
 
Wote picha zinaonyesha wamepigwa risasi za mgongoni,je ni sahihi wakti inaonyesha huyu alikuwa anakimbia kujiokoa?

Hawa askari wetu Majambazi ni kwamba bado sheria kuhusu sehemu ya kupiga hawajaijua. Huyu mtu inaonyesha alikuwa anakimbia kujisalimisha either kwa kutii amri ya Polisi iliyowataka kuondoka.

Sasa ikiwa mtu anaondoka eneo hilo kisha unampiga Risasi, nini maana ya kuwataka kutawanyika. Si heri wangewapiga tu au kulipua BOMU moja ambalo lingetosha kuua watu wote. Kwani inaonyesha walikusudia kuua na siyo kutuliza ghasia.

ACHENI NISEME, HATA MKINI.......... ACHENI NISEME....... TANZANIA HAKUNA SERIKALI WALA JESHI. HIVYO KUANZIA RAISI, IGP, NA MAWAZIRI WAKE WOTE KWA NINI WASIJIUZULU ILI TURUDISHE AMANI TULIYOACHIWA NA BABA WA TAIFA LETU"

ACHENI NISEME HATA MKINIMWAGIA MAJI WASHA ACHENI NISE...........




MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Ni zaidi ya wiki mbili sasa kumekuwa na matukio ya wananchi kuchinjwa na watu wasiojulikana,matukio hayo yamekuwa yakihusishwa na imani za kishirikina kwa kuwa kila anayechinjwa alikutwa hana nyeti.Matukio haya yamekuwa yakitokea mfululuzo kila siku,Usiku wa kuamkia jana kuna mzee alikuwa anatoka msikitini usiku alichinjwa na usiku wa kuamkia leo kijana mwendesha boda boda naye amepoteza maisha kwa kuchinjwa achilia mbali mauaji yaliyofanyika siku ambazo sijazitaja hapa Huko nyuma wananchi walimfuata mkuu wa wilaya na Rpc kuhoji juu ya mauaji haya lakini wakuu hawa walipinga kutokea mauaji haya na kuwaita wananchi wanaopoteza maisha ni wahuni waliokuwa kwenye matukio yao ya uharifu.Wakuu hawa wamekuwa wakitumia local radio kukanusha kuwepo kwa mauaji hayo.Hatujui ni nini kilicho nyuma yao,Baada ya mauaji ya kijana muendesha boda boda yaliyotokea usiku wa kuamkia leo,wananchi walichukua maiti ya huyo kijana na kuandamana kuelekea kwa mkuu wa mkoa kumuonesha na kutoa hisia zao za kutokuwa na imani na jeshi la police Cha kushangaza jeshi letu la police lilishindwa kutumia busara na kuanza kutumia silaha za moto kuwatawanya waandamanaji hao tena sio tu kuwatawanya mabomu hayo yamelekezwa hadi kwenye nyumba za watu na mashuleni hali iliyopelekea shughuli zote za uzalishaji mali na ofici zote kama bank,masoko na maduka yote kufungwa huku wananchi wakitakiwa kutotoka nje.Hadi sasa wananchi wa 4 na police 1 wamepoteza maisha ktk vurugu hizo.Nimefanya mavungumzo na Rpc wa Ruvuma kwa kweli maneno anayoongea ni ya kutokokuwa na huruma wala kujali,nitayaweka mazungumzo hayo hapa muda c mrefu.Haya ndio matatizo ya kuwa na viongozi wasiowenyeji wa mahali husika.
 
na huyu ameisha aga dunia, hapo ni jirani na bombambili

424094_10150596342519504_666929503_8377096_350133664_n.jpg

masikini weee

hivi polisi huwa mnajisikiaje pale mnavyo ziona maiti mlizo zipiga risasi? ama mnasema "aisee nililenga vyema nikampiga mgongoni na ikisha mpata mshindo wake bwana huwa unasikika kwa mbariii hahahahah"

polisi muwe na huruma,mbona majambazi na wazee wa epa wanalisumbua taifa hili lakini hamuwalengi kwa bunduki zenu?
 
Hali hii inaruhusiwa vipi kuendelea? Nahodha anasemaje na hapa? nasi tuwaue Polisi?
 
Na hii nayo ya kisiasa!
Polisi wanahusikaje hapo! wrong suspect divert from reality!
 
Kikwete yuko wapi? Ongea neno moja tu Rais...

Mimi Raisi wenu nina ziara ya kwenda kugawa ng'ombe. na nyie subirini nitakuja kuwagawia. Najua leo mnakasirika lakini mkiona mgao wa Ng'ombe nyote mtachekelea kama wale wenzenu wa kule .................................... Yote mtayasahau haya



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Toba!!!!!!!
Au hao wa songea siyo wa tz?mbona
government bado kimya hakuna tamko???!

Eeeeeee Wewe unataka tamko la Serikali!!!!!!!!!!!

huko inasemekana bado mapambano yanaendelea. Sasa ukitaka watoe tamko ni kwamba wataamrisha Wanajeshi JWTZ na JKT wakapige mabomu pale.

Tusiombee tamko la Serikali kwani hawawatakii mema raia wao, bali kuangamiza kizazi chote kwa manufaa ya wachache.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
kutokana na ufirauni wa ccm,sasa ya leo songea ni CV jingine kujiongezea,washeni helcopa yenu sasa na paeni to Songea faster,we Zitto kabwe mpigie Mdee na mnyika.
 
Back
Top Bottom