Maandamano makubwa Songea!

Tatizo polisi wetu ni mwiko kuamini mkubwa anakosea pamoja kuwa wengi wao walifanya vibaya kidato 4 hata akili ya kuzaliwa nayo imeporwa na nani? Kwanini wasitake kujua chanzo na kulishughulikia bila kumdhuru mtu? Mi nadhani wanajidhalilisha kuwa bongo zao ni kapu tupu linalosubiri kuwekewa takataka na halina uwezo wa kuchuja. Yaani wanashirikiana na wauaji kuwaua Watanzania wanaolalamikia haki yao ya kuishi?
 
sababu ya hayo mauaji ni nini? ushirikina ujambazi au, naona habari iko upande mmoja.
 
Picha ziko kwenye hii blog,songeayetu.blogspot.com nashindwa kuzi upload anayeweza afanye hivyoo!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kuna tatizo hapa. Jeshi la polisi limehoza kupindukia
Kuna matattizo katika trainning ya jeshi.
Sidhani kama yaho ndio mafunzo wanayoyapata kule CCP na kuingineko.

Polisi wanajiona kuwa ni Miungu watu wanaoweza kuwatisha raia na hata kuua saa yeyote kama uko Songea na kuingineko.

Wengine wanazungukaga na piki piki wakiwa na mitutu bila kazi yeyote maalumu na ya maana kwa umma ili kutisha raia.

Sishangai!
Tunaongozwa na wakoloni weusi na vyombo vyao vya usalama ndio hivi
Wakati wa ukoloni kulikua na kitu kinaoitwa gunboot diplomacy ya kutengeneza hofu kwa raia na inashangaza mpaka sasa hayo yanaendelea.

Taifa na watu wa Songea wanahitaji maelezo ya kina juu ya mauaji ya raia na katika kudai hayo nao wanauwawa. This is bustard!
 
There is a difference between Wikipedia and Wikileaks.....hiyo red sijui ulimaanisha ipi hapo!?

Mleta mada hajasema wikileaks, sasa we mbona unaleta kitu kisichoandikwa na mleta mada? Soma ujumbe ulioletwa hilo ndilo muhimu, kwani yaliyoandikwa ni uongo? Au yaakuunguza maini?
 
Mleta mada hajasema wikileaks, sasa we mbona unaleta kitu kisichoandikwa na mleta mada? Soma ujumbe ulioletwa hilo ndilo muhimu, kwani yaliyoandikwa ni uongo? Au yaakuunguza maini?
Dah! Joooob true true!
 
Wote picha zinaonyesha wamepigwa risasi za mgongoni,je ni sahihi wakti inaonyesha huyu alikuwa anakimbia kujiokoa?
 
Kutoka Blogu ya songea yetu moja ya marehemu ni huyu hapa na polisi wakiwa kazini



Marehemu



Mwandishi wa TBC akiwa anajihami na risasi za polisi
 
viongozi+wetu.jpg

PICT0021-1.jpg
PICT0024-2.jpg
PICT0020.jpg
PICT0024-1.jpg
 
Tatizo polisi wetu ni mwiko kuamini mkubwa anakosea pamoja kuwa wengi wao walifanya vibaya kidato 4 hata akili ya kuzaliwa nayo imeporwa na nani? Kwanini wasitake kujua chanzo na kulishughulikia bila kumdhuru mtu? Mi nadhani wanajidhalilisha kuwa bongo zao ni kapu tupu linalosubiri kuwekewa takataka na halina uwezo wa kuchuja. Yaani wanashirikiana na wauaji kuwaua Watanzania wanaolalamikia haki yao ya kuishi?

kweli kabisa mkuu, polisi wetu wanatia kinyaa. hawana kabisa uwezo wa kufikiri kwa
akili zao, (kama wanazo).
 
weka picha we need pictures

Kwenye hali kama hii mtu ukipiga Picha na makamanda Waadilifu wa Afande Mwema wakikuona unawapiga picha hapo ujue ndio mwisho wa Uhai wako. Lazima watakufyatulia Risasi na kukumaliza.

Yabidi utumie akili na umakini katika kupata picha hapo.

MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA = TULIAHIDI - TUMETAFAKARI - TUNATIMIZA



HEKO VIONGOZI WETU WEMA KWA RAIA WAKE TANZANIA. LAZIMA TUVUNE TULICHOPANDA



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kwa mliosikiliza radio na kuangalia ITV mmejulishwa kinachojiri songea asubuhi hii ni mapambano ya askari na raia

CHANZO CHA MAPAMBANO
Kuna raia wanauawa tangu juzi na matukio yanaripotiwa ila askari hawachukui hatua yeyote ile zaidi wanasema ushahidi hawajauona,usiku wa kuamkia leo limekua tukia la 5 raia kuuliwa na askari kama kawaida yao hawatoi ulinzi kwa raia wao.

Asubuhi raia (Watoto, vijana, wazee) wakaamua kuwatolea uvivu askari na kuandamana hadi kituo cha polisi kudai haki ya kulindwa na kuishi raia walikua wengi kuliko uwezo wa askari wa kile kituo hivyo waliona hapa wakiwa wakali kituo kitachomwa moto maaana walikuja na jazba raia wakawaambia taarifa ziko kwa mkuu wa wilaya raia bila simile wakaanza maandamano hadi kwa mkuu wa wilaya kufika huko naye akanawa mikono kama pilato akasema mkuu wa mkoa ndo liko mikononi mwake.

Raia hawakuishia hapo wakalianzisha hadi kwa mkuu wa mkoa huku wakiimba "TUMECHOKA KUUWAWA" hadi kwa mkuu wa mkoa, hapo ndo movie ilpoanzia kumbe raia wakati wanaenda kwa mkuu wa mkoa inaaminika simu zilipigwa kwa mkuu wa mkoa na askari wanaolinda (FFU) wakafunga geti hapo ndo ikawa vuta nikuvute raia wakaweka kambi nje huku wanaimba nyimbo "MKUU WA MKOA UNAWAOGOPA RAIA WAKO JIUZURU", muda si mrefu gari ya FFU likawasiri likiwa na askari wa kutosha kwa vile raia hawakua na silaha wala ugomvi wakaamua kubaki huku wanaimba.

Askari kama kawaida yao wakawa wanazidi kusogelea huku wakitoa ishara wananchi watawanyike huku wananchi wakigoma hawatoki hadi mkuu wa mkoa naye atoke nje hapo ndo askari wakaanza kufyatua risasi za moto na raia wawili wakafa.habari zikafika mjini raia wameuliwa na askari hapo ndo mji ukazizima raia wakaingia mitaani askari waliokua mitaani walianza kupata upinzani mkali hd askari wawili wamekufa hadi hivi sasa, imebidi jeshi liingilie kati na mji wote kufungwa hivi ss mjini ni makundi ya wanajeshi na askari ndo yametawala hakuna maduka wala mabenki yanayofanya kazi

VIFO
Nimeshuhudia raia wawili na askari mmoja tu kwa macho yangu kwa sehem niliyokuwepo,kiujumla inasadikiwa raia zaidi ya wa4 na askari 2 ndo wamekufa,mji umepoa kabisa na mm ndo niko nyumbani ila ntarudi later mjini kuchukua news zaidi ili niwajulishe


Nawakilisha
 
Kuna habari kuwa kuna maandamano na mapambano baina ya raia na polisi huko songea na watu watatu wameuawa tayari. Raia wanapinga mauaji yanayoendelea huko songea bila polisi kuchukua hatua.walio huko watujuze zaidi kinachoendelea

source: Live coverage radio maria
 
Nimeona mzee,kwakweli yasiyowezekana tokea popote duniani yanatokea tanzania songea,watu wanapinga wenzao kuuwawa na majambazi kinyama,polisi inaacha majambazi inaua raia ambao hawana hatia,all in all movement has started,r.i.p wote waliouwawa leo poleni mliopoteza wapendwa wenu.songea aweakening/uprising....god bless you all!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom