Maandamano (DEMOSTRATION)

chachu

Senior Member
May 17, 2011
141
16
Je mbadala wa maandamano tutumie njia gani kudai haki?

NAOMBA WANA JF TUTOE MAONI KWA MADA HII.
Nawakilisha
 
Je mbadala wa maandamano tutumie njia gani kudai haki?

NAOMBA WANA JF TUTOE MAONI KWA MADA HII.
Nawakilisha
Haki zinazodaiwa zipo za aina nyingi labda nikufafanulie kidogo
1. Haki za wafanyakazi - Maandamano katika kudai haki kwa kundi hili si lazima sana stahili ya ili kundi ni KUFANYA MGOMO

2. Haki za raia kudai vitu muhimu kutoka serikali yao - Kundi hili linaweza kutumia sanduku la Kura kutekeleza madai yao kwa kutochagua chama au viongozi wasiofaa na kama hili linashindikana kama ilivyo sasa kwa Utawala huu wa CCM kwani hawawezi kuondoka kupitia sanduku la Kura kwa stahili hii MAANDAMANO hayakwepeki lakini yanatakiwa maandamano ya ujasili kama yalivyofanyika/ yanayofanyika katika nchi za kiarabu

3. Haki kwa wanafunzi mashuleni na Vyuoni - Wao mara nyingi mbinu nzuri ya kutumia huwa ni kugoma kuingia darasani na inaposhindikana hilo nao pia MAANDAMANO huwa ni lazima kupeleka ujumbe kwa viongozi wa juu wa serikali.
 
Kila atakayeandamana kudai haki atapigwa tu! Polisi hawana mchezo. Wameshapewa ruksa na Pinda.

Zipo njia mbadala za kudai haki kwa amani. Maandamano yamepitwa na wakati. Watu watapigwa virungu na kuumizwa bure.
 
Maandamano ndio mtaji wa CHADEMA, kuwatoa sadaka watu waliokata tamaa na maisha
 
Maandamano ni last ultimatum kwa sauti zilizopuuzwa....!
Kuna njia ya kufikisha tatizo kwa wahusika physically au kwa njia ya barua au mwakilishi.....
Kuna kuendelea kufuatilia feedback ya appeal yako to the problem....
If the problem persist and ears of leaders are completely closed.....then demonstration must be applied!
 
mawazo hayo hayakinzani sana, karibuni tuendelee kuchangia ili kuboresha katiba mpya. nashukuru kibogo sanduku la kura thats can be perfect, kuliko kupoteza muda barabarani
 
Last edited by a moderator:
Je mbadala wa maandamano tutumie njia gani kudai haki?

NAOMBA WANA JF TUTOE MAONI KWA MADA HII.
Nawakilisha

Walicho fanya wenzetu wakazi wa Arusha jumapili ni dawa tosha ya mbadala wa maandamano yaaaniii kimya kimya!!! Saa ya ukombozi imefika
 
Back
Top Bottom