Kwamba taarifa zote zilifuatwa. Hata ilipobidi rufaa ilikatwa kwa waziri:
"Silence gives consent."
Kesho tutamwagika mitaani kwa maandamano yatakayokuwapo kila tarehe 9 ya mwezi hadi hoja zetu zitakapojibiwa.
Kwako Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, rais wetu mpendwa wa JMT:
"Kuna tetesi za polisi Mbeya kuandaa risasi za bahati mbaya kuuwa na kujeruhi watu kesho."
Bahati mbaya inapigiwa je mahesabu yake leo?
"Wewe ni muislam mwenye hofu ya Mungu."
Kulikoni haja ya majibu ya hoja kupangiwa majibu ya risasi, virungu, kujeruhi au kuuwa?
Kemea polisi hawa wenye wajibu kama wewe na sote wengine wa kuilinda katiba ya nchi.
Kulikoni wengine kukuchumia wewe dhambi hata mbele za Mola?
Kulikoni usitume mwakilishi wako kuwasikiliza wananchi hawa wasiokuwa na chembe ya shari akakuletea mrejesho?
Kulikoni kutaka kuipoteza fursa hii ya kuiunganisha nchi kwa vitendo?