Yaliyojiri Mahakama Kuu kesi ya Mbowe na wenzake. Superitendent Jumanne Malangahe atoa ushahidi, Kesi imeahirishwa hadi Nov 9, 2021

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
Baada ya Ijumaa kesi kuahirishwa, Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani.

Leo Jamhuri inaleta shahidi mwingine. Kuwa nami.

=====

Jaji ameingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa

WS Robert Kidando anasimama

Jaji: Ndiyo

Robert Kidando anatambulisha Jopo la mawakili wa serikali

  1. Abdallah Chavula
  2. Jenitreza Kitali
  3. Pius Hilla
  4. Nassoro Katuga
  5. Esther Martin
  6. Tulimanywa Majige
  7. Ignasi Mwinuka
Wote wanawakilisha Jamhuri katika kesi hii...

Wakili Peter Kibatala nae anasimama na anatambulisha Jopo la mawakili wa upande utetezi.

  1. Maria Mushi Evaresta
  2. Kisanga Hadija Aron
  3. Alex Massaba Idd
  4. Msawanga Seleman
  5. Matauka Dickson Matata
  6. Nashon Nkungu
  7. Fredrick Kihwelo
  8. John Mallya
  9. Peter Kibatala
Wakili wa Serikali: Shauri hili linakuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna Shahidi Mmoja, Tupo tayari Kuendelea

Kibatala: Tupo tayari Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali: Mmoja anaenda Kumfuata Shahidi JAJI yupo Kimyaaaa anaandika Kidogo

Peter Kibatala anaomba Radhi kwa Kuchelewa Kidogo

Jaji
: Shahidi wa ngapi huyo?

Wakili wa Serikali: Shahidi wa 8

Jaji: Majina yako

Shahidi: Superitendent Jumanne Malangahe

Jaji: Umri

Shahidi: 46

Jaji: Kabila

Shahidi: Msukuma

Jaji: Shughuli yako

Shahidi: Afisa wa Polisi

Jaji: Dini yako

Shahidi: muislam

Shahidi: Wallah wabillah taala nathibitisha kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa wa kweli, Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie

Wakili wa serikali: Kitambulisho Bwa Jummane Unafanya Kazi gani

Shahidi: Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha

Wakili wa Serikali: Majukumu yako ni nini

Wakili wa Serikali: Elezea hapa Mahakamani Tarehe 04 Mwezi August 2020 ulikuwa wapi

Shahidi: 04 August 2020 nilikuwepo katika Kituo Changu cha Kazi, Upelelezi Wilaya ya Arumeru, Nikiwa Ofisni Kwangu nilipigiwa Simu na Afande Kingai, Akinitaarifu kuna Safari Ni jiandae Ya Kwenda Kufanya Moshi, Mkoani Kilimanjaro

Wakili wa Serikali: ilikuwa Muda gani wakati anakupigia Simu

Shahidi: Ilikuwa Muda wa Saa 12 na Kitu

Wakili wa Serikali: ya Muda gani

Shahidi: Ya Jioni

Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea Kutokana na alichokutaarifu

Shahidi: Alikuwa afande ACP Ramadhan Kingai

Wakili wa Serikali: Katika Majukumu yako ya Upelelezi na Kusimamia Askari waliopo Chini yako no Shughuli gani katika Upelelezi hufanyika

Shahidi: Baada ya Shauri Kufunguliwa, ndipo Upelelezi Unapoanza kwa kuwakamata wa husika, Kupelele Shauri na Kukagua eneo la Tukio Pamoja na Kuku Sanya Vielelezo namambo Mengine kutokana Aina ya tukio

Detective Coplo Francis, Detective Coplo Goodluck pamoja na Dereva wa Gari Detective Constable Azizi

Wakili wa Serikali: Wakati Kingai anaingia Ofisini Kwako hawa wenyewe walikuwa wapi

Shahidi: Wali ingia Wote Ofisini Kwangu

Wakili wa Serikali: Elezea sasa baada ya Kuingia Ofisini nini Kiliendelea

Shahidi: Nilijiandaa na Saa 1 kasoro aliwasili nikiwa Ndani nikasikia Muungurumo wa Gari, nikampokea na Kwenda Ofisini Kwangu Kisha tukaketi

Wakili wa Serikali: Wakati Kingai anafika, Yeye alikuwa na nani?

Shahidi: Alifika na Askari Jumla walikuwa watano akiwemo yeye Mwenyewe, Insp Mahita,

Tukianza Safari ya Kuelekea Moshi

Wakili wa Serikali Pale Moshi Mlifika Saa ngapi?

Shahidi: Saa 2 Usiku

Shahidi: Afande Kingai akasema anaendelea Kupokea Taarifa Kutoka kwa Msiri wake Kutoka Kwa Msiri wake. Na hivyo Miongoni Mwa Wahalifu hao watatu walikuwa wameshawasili Moshi kwa ajili ya kutekeleza Uhalifu huo Akasema Jukumu letu ni Kuzuia Uhalifu huo Kutendeka na Kuhakikisha Wahalifu hao tunawakamata Baada ya Kumalizia kutoa Maelekezo hayo ilikuwa ni Takribani saa Moja

Shahidi: Afande Kingai Alianza Kutoa Taarifa Kwamba Kipo Kikundi Cha Kihalifu ambacho kinatarajia Kufanya Matukio ya Kihalifu hapa Nchini Ambayo ni Kulipua Vituo Vya Kuzuia Mafuta, Kuanzisha Vurugu na Maandamano, Kukata Miti na Magogo na Kuyaweka katika Barabara Kuzia Magari

Akatuambia amepata Taarifa wale Wahalifu Wapo Maeneo ya RAU Madukani, Walikuwa watatu na akatuelekeza Mwonekano wao na aina ya Nguo walizo vaa

Wakili wa Serikali: Elezea Sasa Kesho yake Asubuhi nini Kiliendelea

Shahidi: Tulikutana Kituo cha Mjini Kati pale Moshi akasema, Tuendelee Kupokea Taarifa Mpaka atakapojiridhissha Mazingira Yamekaaje

Shahidi: Tuliendelea Kuwepo Maeneo yake Mpaka Takribani Saa 6 Mchana Afande Kingai akatuita tena

Wakili wa Serikali: Kuhusiana na hicho alichowaambia Kingai Kuhusiana na Mwonekano wa Nguo ulikuwaje

Shahidi: Alisema Wawili Kati yao Wanamaumbo Madogo Madogo lakini wa mevaa Masharti Mekundu Kati ya wale wawili Mmoja Amevaa Shati la Maua Mekundu Mekundu, Mmoja amevaa Shati la
Maua Maua ya Kijani iliyopauka Na Watatu alivaa Jezi ya Mpira ya Taifa Stars ambayo ilikuwa na Rangi ya Blue

Wakili wa Serikali: baada ya Kuwa eleza Mwonekano wao.?

Shahidi: Alituambia tuelekee katika Eneo hilo Haraka tuweze Kufanya Ukamataji, Ndipo tuliondoka Kuelekea Eneo la Rau Madukani

Wakili wa Serikali: Mlipoondoka kuelekea Rau Madukani mlikuwa nani na nni?

Shahidi: Ramadhan Kingai Mimi Mwenyewe Inspector Mahita GOODLUCK Francis Na Dereva wa Gari Azizi

Wakili wa Serikali: Mlifika Saa ngapi?

Shahidi: Mchana Takribani Saa Saba

Shahidi: Tukaelekea Gari ambapo Afande RCO alikuwa ameelekezwa Eneo ambalo Wahalifu Wamekaa. Alisema Kwenye Grocery

Wakili wa Serikali: Grocery ilikuwa wapi?

Shahidi: Palepale Rau Madukani, Ambapo Kwenye Kona ya Barabara, Yenyewe ipo kando kabisa ya hiyo Barabara

Shahidi: Tuliegesha Gari yetu, Ndipo Afande RCO akamtuma Kwanza Inspector Mahita Kwenda Kujiridhisha Kama Watu wenye Mavazi na Mwonekano huo wapo

Wakili wa Serikali: Mahita alifanya nini

Shahidi: alishuka Kwenye gari, a Kapita Kwenye lile eneo na baada ya Muda Mfupi akarudi

Wakili wa Serikali: Baada Ya Kurudi Majibu yalikuwa nini?

Shahidi: Amewaona wamekaa Katika Kibanda

Wakili wa Serikali: Walikuwa wa ngapi

Shahidi: Watatu

Wakili wa Serikali: Nini kilofuata

Shahidi: Afande RCO katuamuru tushuke kwenye gari, Akatugawa. Makundi Mawili

Shahidi: kundi moja lilikuwa Kingai, Mimi na Goodluck, lingine Mahita na Coplo Francis

Shahidi: Alitoa Maelezo Kwamba Mahita Aelekee Upande wa Kushoto na Sisi tuelekee Upande wa Kulia

Shahidi: Mwonekano wa Eneo hilo ni kama hivi, Hapa Bara Bara imepita, Kuna Uwazi, Hapa pembeni Kuna Uwazi, na Ndipo Maduka Yanatizana Babarabarani, Kuna Banda lipo ambapo Lenyewe kuna uwazi Katikati na Limepakana na hiyo Glocery (Shahidi anaelekeza kwa ishara za mikono yake) Vilevile Kwenye Banda Kuna Uwazi wa Kuingilia, na Kwenye haya Maduka Kuna Choo lililopakana na Grocery

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa ile Taarifa aliyowapatia Mahita, Elezea ni wapi walikuwa watu hao

Shahidi: Walikuwa ndani ya eneo hili, Walikuwa wamekaa Grocery

Wakili wa Serikali: Sasa Ulisema Mpangilio wenu ulikuwa Mgawanyiko mara mbili, Je akina nani walipita Kushoto na akina nani walipata Kulia?

Shahidi: Inspector Mahita na Coplo Francis Walipitia Upande wa Kushoto, Mimi na Afande Kingai na Goodluck tulipitia Upande wa Kulia ambapo Kuna Banda hilo

Shahidi: Tukianza Kuelekea Katika Maeneo hayo Mawili Kama ambavyo Afande RCO alikuwa anaelekeza

Wakili wa Serikali: RCO ndiyo nani

Shahidi: Afande Mahita

Shahidi: Na pale tuliokuwa tunaenda watu walipokuwa karibu ni Coplo Francis na Inspector Mahita. Sisi wakati tunaelekea Kwenye hilo Eneo hatukuona Watu, tulipotaka Kuingia Kwenye huo Uchochoro hatukuona Watu Ghafla tukasikia Sauti, ambayo ilikuwa Sauti ya Inspector Mahita

Wakili wa Serikali: Ukisikia Mahita akisema nini?

Shahidi: "KAA CHINI, UPO CHINI YA ULINZI" kwa Sauti ya Juu

Wakili wa Serikali: Elezea Mlipofika Pale nini Kiliendelea pale

Shahidi: Baada ya Kufika Pale ACP Ramadhan Kingai aliwauliza Majina Yao Nao walijitambulisha kwa Majina ya Adam Hassan Kasekwa na Mwingine Mohammed Ling'wenya

Shahidi: tulitembea Kwa Haraka Kuelekea Kwemye hilo Eneo ambapo tuliwakuta

Wakili wa Serikali: Mliwakuta walifanya Nini?

Shahidi: Watu wawili walikuwa wamekaa chini

Kibatala: OBJECTION hiyo ni Leading

Shahidi: Coplo Francis alikuwa na silaha

Wakili wa Serikali: Silaha ya aina gani

Shahidi: SMG

Wakili wa Serikali: Kwa Upande wenu je

Shahidi: alikuwa nayo Goodluck

Wakili wa Serikali: Wakati mmesikia Amri ya a kukaa Chini Kitu gani Kingine alichofanya

Shahidi: Tulikutana anamalizia Kuwaambia Kwa Sauti kwamba wanatuhumiwa Kula Njama za Kufanya Vitendo Vya Kigaidi

Wakili wa Serikali: Wakasemaje?

Shahidi: hawakujibu Kitu wakati ule, Lakini Afande Kingai akasema ndiyo wenyewe, Na baada ya hapo a kawaambia kuwa Wanatuhumiwa Kula Njama kutenda Makosa ya Kigaidi, Baada ya Maelezo hayo aliniamuru Mimi Kufanya Upekuzi wa Maungoni

Wakili wa Serikali: Mwanzoni Mlisema Mlikuwa Mnaenda Kukamata watu watatu Je Mwingine Yupo wapi

Shahidi: Mtu wa tatu pale hakuonekana, Mpaka Afande Kingai aliulizwa Pale Mwingine Yupo wapi,

Wakili wa Serikali: Alikuwa anamuuliza nani?

Shahidi: Aliwauliza Watuhumiwa

Wakili wa Serikali: Eneo lipi walikuwa wamewekwa Chini ya Ulinzi Katika Eneo hilo

Wakili wa Serikali: Ukisema Upekuzi wa Maungoni Unamaanisha Nini?

Shahidi: Kupekua Ndani ya Nguo na Sehemu za Maungo yao

Wakili wa Serikali: baada ya hapo Ulifanya nini?

Shahidi: Nikamwambia Afande Kingai kuwa Ngoja Nikaite Watu kwa ajili ya kushuhudia

Wakili wa Serikali: Ukawafuata wapi?

Shahidi: Palikuwa na Maduka na Mabanda kwa hiyo niliamini kuna watu wanaoendelea na Shughuli zao Na hapo watu watu walikuwa Wamesha Anza Kusogea

Wakili wa Serikali: Zoezi la Kutafuta Mashahidi lilifanyikaje

Shahidi: Nili angalia Maeneo Kadhaa Nikaenda Kwenye Banda, Ni kauliza nani anaye husika hapa, Kwamba Kwakuwa Kulikuwa wazi basi Kuna Shughuli zilikuwa zinaendelea Baada ya Kuuliza hivyo alijitokeza Dada Mmoja kwa Jina la Anita Mtaro

Wakili wa Serikali: yeye alikuwa wapj

Shahidi: ikiwa amesimama Mbele ya Banda lake Kidogo

Shahidi: Hatua Kidogo Katika Banda, Katikati ya hayo Maduka na Pembeni Kidogo Kuna hayo Maduka

Shahidi: Pia nikijambulisha kuwa Mimi ni Afisa wa Polisi nikamuonyesha Kitambulisho Changu akakubali Kusogea

Wakili wa Serikali: palikuwa na Hatua ngapi au Umbali gani

Shahidi: Hatua Sita au Saba

Shahidi: Yule Dada alisita Kidogo, akaniuliza ataamini Vipi Kama Mimi ni Afisa wa Polisi Nikamtolea Kitambulisho Changu Cha kazi ambacho ni Chekundu, akakubali Nikaenda pia pale Grocery nikamkuta Dada Mmoja anaitwa Esther Nduhul

Wakili wa Serikali: Kuna Umbali gani Kutoka Watuhumiwa walipowekwa Chini ya Ulinzi?

Shahidi: Hapakuwa mbali sana Takribani kama Hatua 5

Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea

Shahidi: Nilijitambulisha Kwake kwamba Mimi ni Afisa wa Polisi na baada ya hivyo nilimuomba asogee kuja Kushuhudia

Ni kawaambia Wanatuhumiwa Kwa Vitendo Vya kula Njama ya Kutenda Makosa ya Ugaidi na hivyo nahitaji kuwapekua katika Maungo yao

Wakili wa Serikali: Baada ya Kupata Mashahidi nini Kiliendelea

Shahidi: Nikiwa uliza tena Majina watuhumiwa ambao walikuwa bado wamekaa Chini Wakajitambulisha tena kwamba ni Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Ling'wenya Na Mimi Nikajitambulisha kwao kwamba naitwa ASP Jumanne Malangahe

Wakili wa Serikali: Wakati huo Anita Mtaro na Esther Nduhulu walikuwa wapi?

Shahidi: Walikuwa palepale Wakishuhudia

Shahidi: nikatoa Vitu vyangu na Kunyoosha Mikono yangu Nikamwambia Mtuhumiwa wa Kwanza asimame,

Wakili wa Serikali: Ambaye ni Nani?

Shahidi: Adam Kasekwa

Shahidi: Nilimwambia ageuke Nyuma, Anyooshe Mikono Juu, alitii na nilianza kumpapasa Kuanzia Kichwani, Shingoni, Kifuani na Nilipo fika Sehemu ya Kiunoni nilihisi Kitu kigumu Upande wa Kushoto, Nilipitisha Mkono wangu nikishika kitu Kigumu na Kukichomoa, kilikuwa ni silaha

Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni sehemu gani?

Shahidi: Kwenye Mkanda au Pindo la Silaha

Wakili wa Serikali: Ikafuata nini Shahidi Nikaichomoa na Kuonyesha hii ni salaha, Ni Bastola na Nichomoa Magazine, ilikuwa na Magazine na Ndani ya Magazine Ilikuwa na Risasi tatu

Shahidi: Baada ya Kuuliza Mikono Mifukoni Mwake, Upande wa Kushoto sikuoata Kitu, Ila Upande wa Kulia Niliingiza nikatoa Simu Ndogo aina ya Itel Ila Pia nikatoa Kinailoni baada ya Kukitoa, ambacho Kilionekana kimeviringishwa nikakitoa nikakinyoosha ambacho Kilikuwa ni Kirefu Na Kilikuwa na Vitu Mfano wa Karanga

Wakili wa Serikali: Vilikuwa ni Vitu gani

Shahidi: Nilihisi ni Madawa ya Kulevya. Nikampatia Goodluck Nikaendelea kupapasa zaidi nikaingiza Mifukoni Mwake

Wakili wa Serikali: Vilikuwa Vingapi

Shahidi: Nili Sogea kwa Mtuhumiwa Nikaanza Kuhesabu Nilihesabu Zikawa 58 Ndani ya Simu palikuwa na Line Mbili Nilituma Goodluck aende kwenye Kuchukua Fomu ya Hati ya Kuchukulia Mali Nilianza Kujaza kwa kuitambua Ile Silaha.

Shahidi: Lakini Pia Nilijaza fomu Nyingine ambapo Nilijaza hizo Kete za Huo Unga ambao nilihisi ni Madawa ya Kulevya

Wakili wa Serikali: Ulifanya nini kwenye hiyo Fomu

Shahidi: Nilimuonyesha Mtuhumiwa akaangalia akasaini na Anita na Esther na wao wakasaini katika fomu zote Mbili

Shahidi: Ambayo ilikuwa imeandikwa Luger A5340 na namba hizo zilikuwa zimeandikwa Upande wa Kulia, Na pia niliorodhesha Risasi Tatu ndani ya hiyo Magazine Pamoja na Simu na line zake

Wakili wa Serikali: Ulikuwa unaorodhesha wapi?

Shahidi: Katika fomu hiyo, Hati ya Kukamatia Mali

Wakili wa Serikali: Ulifanya nini Kuhusu Mtuhumiwa Mohammed Ling'wenya

Shahidi: Kwanza baada ya Kumalizia Kujaza nilitoa Carbon Nakala ya Ile Fomu nikampa Adam Kasekwa ambaye nilimwambia akae Chini Nikamsimamisha Mtuhumiwa wa Pili na Yeye Nikamwambia ageuke

Shahidi: Naye nilianza Kumpekua Kichwani Na Kiwili wili chake sikuona kitu Nikaanza Kuingiza Mikono yangu Mifukoni Mwake Nikakutana na Simu Kubwa aina ya Tecno, Yeye pia nilimkuta na Vikaratasi Ambayo nilihisi ni Madawa ya Kulevya, nikavihesabu Mbele ya Mashahidi Vilikuwa 25

Vilevile nilifungua ile simu Nikaikuta ina line Mbili, za Hallotel na Airtel niliwaonyesha Mashahidi na Kuendelea Kuteremka Sehemu za Miguu lakini sikuona Kitu Nilichukua Fomu nikajaza na Fomu Nyingine Nilijaza hizo Kete ambazo nilihisi ni Dawa za Kulevya

Shahidi: Baada ya Kumalisha nilimpa Nakala mbili Nakala niliyojaza simu na Nakala ya fomu niliyojaza kete, Mtuhumiwa aliviona karidhika akasaini na Mashahidi wakasaini nikampa Nakala zake

Wakili wa Serikali: na Hivi Vitu ambavyo unasema Ulijaza eneo la Rau Baada ya hapo ulivipeleka wapi

Shahidi: Nilimkabidhi Goodluck ambaye nilikuwa namkabidhi tangu Mwanzo, na Pia Nikachukua fomu nikajaza na Kumkabidhi.

Wakili wa Serikali: Leo hii ukiiona ile Pistol Unaweza Kuitambuaje?

Shahidi: Kwa Serial Namba A5340

Shahidi: Na Jina lake lililoandikwa Luger

Wakili wa Serikali: Luger imeiona wapi

Shahidi: Luger Ipo Kushoto

Kibatala: OBJECTION naomba hilo Jibu liondolewe Kwenye Kumbukumbu za Mahakama

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi hatuoni tatizo, na Pingamizi Halina Mashiko

Kibatala: Nasema hivi Shahidi aliulizwa kabla hajashika Kielelezo na akaulizwa Utatambuaje akasema Kwa Serial Na Na hapa akaulizwa Umeitambuaje akasema Kwa Kuona Serial Na Wakili akasema Luger Ipo wapi Kitu ambacho Shahidi hakutaja, Ndiyo nasema huko nikumlisha Majibu Shahidi

Anasimama WS mwingine Pius Hilla

Kibatala: Hana haki Kusimama, Nimeweka Pingamizi, Amejibu Wakili Robert Kidando na Nimejibi tena huyu anasimama Kufanya nini?

JAJI: Ngoja tu tumsikilize...

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Baada ya Kutaja Na Kuonyesha Serial Namba, Wakili akauliza Neno +Luger lipo wapi, Ni swali tu ambalo Shahidi anatakiwa Kujibu kuwa Neno Luger lipo wapi, Kwa Maelezo Hayo ni swali Genuine, Na Kama litazuiliwa haiwezi kuwa sawa na hili Jibu naliondoa Kwenye rekodi, Labda Urudie Upya Swali

Jaji: Shahidi aliulizwa Vigezo ambavyo anaweza Kutambua Kielelezo, Kwa Serial Namba na Mahala ya hiyo serial Namba na Baada ya Hapo Wakili akauliza hilo Neno Luger Lipo wapi akasema hili hapa, ndiyo alichosema Kwa namna ambavyo Kibatala ameweka hoja yake nakubalina na Kibatala

Wakili wa Serikali: Shahidi Unakitu gani Kingine Unachiweza Kutambua Silaha hiyo?

Shahidi: Kwa Serial number zake, A5340 NA Kwa Jina la Silaha hiyo lipo Upande wa Kushoto Luger

Wakili wa Serikali: Naomba Kupatiwa exhibit P3 Mahakama inampatia

Wakili wa Serikali, Robert Kidando, anaifungua

Wakili wa Serikali: angalia Kielelezo hiki kama unakitambua, na Ukikitambua Utasema Kama unakitambua

Shahidi: Nakitambua

Wakili wa Serikali: Unakitambuaje

Shahidi: A5340

Wakili wa Serikali:: Ipo wapi

Shahidi: ANAONYESHA KWA KIDOLE

Wakili wa Serikali: na Risasi 3 zilikuwa wapi?

Shahidi: Zilikuwa ndani ya hii Magazine

Wakili wa Serikali: Sasa wakati Unatoa Ushahidi Wako Ukasema Baada ya Kupata Pistol hii kutoka Kwa Mtuhumiwa Adam kasekwa na Ukapata Risasi tatu, Onyesha Risasi hizo Umetoa wapi

Shahidi: Nilipata kwenye Magazine,

Wakili wa Serikali: Magazine hiyo Ipo wapi?

Shahidi: Hii hapa (ANAONYESHA KWA KIDOLE)

Kibatala: Mshtakiwa wa kwanza anaomba Kwenda uani kidogo

Jaji: kwenda kwake kutasimamisha Shughuli za Mahakama

Kibatala: suala la kukubaliana tu

Nashon: Kwa kuwa wakili wake nipo naomba Mahakama iendelee wakati anaenda uani

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba niendelee

Wakili wa Serikali: Kuna hitaji la Kisheria 196 cha CPA wakati Ushahidi Unachukuliwa, Mshtakiwa Anatakiwa awepo

Jaji: katika Mazingira anamwakilisha na ameridhia Kama wakili wake yupo inatosha, Je unahisi bado Kuna ulazima

Wakili wa Serikali: Tunaomba Guidance yako Mheshimiwa

Jaji: Kwanza Kwa staha, Ombi Lenyewe la Kwenda Uani, Records haiwezi Kuonyesha Kwenye records zangu, Kwanza ameshaingia

Wakili wa Serikali: Shahidi Umesema Wakati unampekua Mtuhumiwa Adam kasekwa Ukijaza Hati ya Kukamatia Mali, Je Leo Mahakamani Ukiiona unaweza Kuitambuaje

Shahidi; Kwa Mwandiko wangu, Majina yangu, Sahihi yangu na Vitu Nilivyo Orodhesha Hapa, Pamoja na Saini za Walioshuhudia Wakati wa Upekuzi na Majina yao

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa tunaweza Kupatikana Exhibit IP1 Mahakama inampatia Nyaraka

Wakili wa Serikali: Shahidi hebu Shika Nyaraka hiyo na uangalie na uweze Kuiambia Mahakama.

Shahidi, ANASOMA

Shahidi: nimeitambua ni Hati ya Vielelezo Nilivyo Pata kwa Mshitakiwa Adam Kasekwa

Wakili wa Serikali: Umeitambuaje?

Shahidi: Kwa Majina Yangu Sahihi yangu Mwandiko wangu Na Majina ya mashahidi Yapo. Pia Mtuhumiwa Mwenyewe Majina yake Niliandika ambayo yamo pamoja na Sahihi yake

Wakili wa Serikali: Ungependa Mahakama ifanye nini hiyo Hati ya Kukamatia Mali

Shahidi: ningeomba Mahakama Ipokee Hati ya Kukamatia Mali kama Sehemu ya Ushahidi wangu Hati inapelekwa kwa mawakili wa utetezi

Mawakili wa upande wa utetezi wanaikagua!

Nashon Nkungu: Kwa niaba ya mshtakiwa wa kwanza tunapinga uchukuliwaji wa nyaraka hii Na msingi wetu ni kwamba nyaraka hii imendaliwa kwa sheria ambayo haipo kwenye nchi yetu Hii siyo nyaraka ya kawaida, Bali msingi wake ni sheria tu

Nashon Nkungu: Lakini Nyaraka hii imenukuu Kifungu cha Sheria 38(3) Sura ya 20 ya mwaka 1985 iliyorekebishwa mwaka 2005 ambayo haijulikani, naomba isipokelewe sababu haijulikani sheria hiyo

Nashon anakaa chini baada ya kumuomba Mheshimiwa Jaji asipokee

Mallya: Kwa niaba ya mshtakiwa wa pili tunapinga kupokelewa kwa nyaraka hii kwa mawasilisho aliyosema Wakili Nashoni Nkungu Na Kuongezea tu hakuna marejeo ya sheria hii mwaka 2018 na hakuna mapitio ya sheria hii ya 38 imefanyiwa marekebisho Mwaka 2019. Na hatuwezi kujua kwamba walimaanisha kwamba ni 2019 na mara ya mwisho Kifungu cha 38 kimefanyiwa Mwaka 1993 baada ya hapo Hakuna Kama Kielelezo kinahusu Mahakama lakini siyo Ya Tanzania Ambayo Kwa MAHAKAMA yako Tukufu haina Sheria hii yenye Marejeo ya Mwaka 2018 Kusimama bila Sheria, Na Sidhani kama Wenzetu watabisha kwamba Kuna Marekebisho ya Sheria hii ya Mwaka 2018, Hii ni Nyaraka isiyo halali kwa Maana hiyo haiwezi kuishi Katika Nyaraka za Mahakama, Na Mallya amesema hapa Kwamba hata hawakuomba kama Kuna Marekebisho tunaomba Upitie

Fredrick Kihwelo: kwa niaba ya Mshtakiwa namba 03 tunapinga pia Kielelezo Kwa Njia ileile ya Kupinga kwa sababu Nyaraka imeletwa kwa Sheria ambayo Haipo kwenye Vitabu Vya Sheria zetu Tanzania Wakili Fredrick anaketi.

Kibatala: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Nne Tunaunga Mkono Pingamizi la wakili wa Mshtakiwa Wa kwanza, Kwa ufafanuzi ni kwamba... Nyaraka hii imeundwa Chini ya msingi wa Kisheria ndiyo Maana yenyewe inasema IMETOLEWA CHINI YA KIFUNGU..... inaonyesha wenyewe wanajua kuwa haiwezi

Kibatala: civil Appeal ya Mwenderosi VS Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ilisema Kwamba Overriding Objective haikuletwa Mahakamani Dhidi ya wadawa. Na Kuhusu Madhara ya Kuleta Nyaraka iliyonukuliwa Kinyume na Sheria usome...

Kibatala: Kesi ya Ardhi ya John Marco VS Joshua Malimbe ni Uamuzi wa Mahakama Kuu, lakini Mahakama ilirejea Mashauri kadhaa, Maamuzi hayo Robert VS Shibeshi Abebe, Na akarejea Mahakama ya Rufaa ya Mgonja Dhidi ya..... Na Kesi ya Anthony Tesha VS Anita Tesha ya Mahakama Ya Rufaa

Kibatala: Nisikuchoshe Mheshimiwa Jaji, Ni hayo tuh Na Nyaraka hii isipokelewe

Jaji: upande wa Serikali!

Wakili wa Serikali: Kutokana na Pingamizi hilo na Wamerejea Mashauri Kadhaa, ku support Hoja zao, Tunaomba Hairisho fupi tuweze Kulipitia, tuweze Kujibu na pia tunaomba Nakala ya Kesi hizo.

Wakili wa Serikali: Tukipata Hairisho la Saa Moja Linatosha

Jaji: Utetezi

Kibatala: Kwakuwa ni haki yao sisi hatuwezi Kuwapinga

Kibatala: Kuhusu Kuwapa hizo kesi, Tumetoa kwenye Tanzii ambayo ni Kifaa Kazi ila tunaweza Kuwasaidia wao Kupata

Jaji: Sahihi

Wakili wa Serikali: Kama zote zipo Tanzii haina shida tutazipata

Jaji: Kufuatia Maombi ya Wakili wa Serikali Robert Kidando Mahakama Inahairiswa Mpaka saa 7 na Dakika 20 Jaji anatoka Saa 6 Na Dakika 20

---------
Mawakili wa upande wa serikali wameonba kuongezwa muda wa dakika 30, mahakama ilikuwa irejee saa 7:20 saa za Afrika ya mashariki. Wameongezewa muda huo, Sasa Mahakama itarejea saa 7:50

Jaji Kaingia

Kesi inatajwa

Wakili wa Serikali, Robert Kidando: column yetu ipo vile vile na tupo tayari sasa kujibu hoja za upande wa utetezi

Kibatala: Sisi pia Upande wetu tupo tayari

Jaji anaandika

WS Robert Kidando:
Mheshimiwa Jaji tumesikikiza Pingamizi zilizoletwa na Upande wa Utetezi, Wakidai Kwamba Ile Hati ya Kukamatia Mali, (Seizure) iliyotolewa Mahakamani na Shahidi wa 08 Kwamba Imeandaliwa Kutoka na Sheria ambayo haipo Na walisema Kwamba Kinachoonekana Kwenye

Nyaraka Hiyo ni Criminal Procedures ACT ya Mwaka 1985 iliyorekebishwa 2018 Na wakasema katika hoja zao Kwamba Kifungu kile cha 38(3) hakijafanyiwa Marekebisho Mwaka huo.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Mwaka katika Nyaraka hiyo Upo, Katika Sheria ya tafsiri inasema kwamba, Hata chapter namba katika Sheria zilizofanyiwa Mapitio au Marekebisho Inajitosheleza, Na Chapter namba kwa Kielelezo Kilichopo Mahakamani, inajitosheleza Kwa Maana Ipo

Mheshimiwa Jaji katika Mazingira hayo kwa Uhakika Kabisa haiwezi kusemwa Kwamba Nyaraka hii Imetengenezwa Kupitia Sheria ambayo haipo, Kama Vile ambavyo Wenzetu wamejaribu Kusema, Na Pengine kwa Msisitizo waliouonyesha Kwa Kuonekana kwa Mwaka 2018 katika Seizure Certificate

Walisema Kwamba Hakuna Revision ya Mwaka 2018, Na Kwa Mwaka huo pia ilikuwa Hoja yao kwamba Kifungu 38 cha CPA hakikufanyiwa Marekebisho, Mheshimiwa Jaji ni kweli Kwamba Hakuna Marejeo(Revision) ya Mwaka 2018, Bila Kuongeza au Kupunguza ni kwamba Imeandikwa Kwamba 2018

Tukichukua Maneno ya Mallya Kwamba Hakuna Amandment ya 2018 ni kweli kabisa Kifungu 38 Kwa Mwaka huo Hakikufanyiwa Marekebisho Isipokuwa Vifungu Vingine Vilifanyika Marekebisho Mwaka huohuo

Mheshimiwa Jaji, Mawakili wasomi walirejea Mashauri Mawili Ku' Support Hoja zao Tukianza na Ndorosi na Wenzake Wawili wa Village Council dhidi ya Serikali

Samahani Mheshimiwa jaji, WS Robert Kidando anatafuta Kitu Kwenye Laptop yake hapa anainama.. WS Jenitreza Kitali anamsaidia.

WS Robert Kidando: Tunasheria Moja tu ya Criminal Procedure Act kwa Upande wa Tanzania Main Land

Wakili wa Serikali: Hivyo Mheshimiwa Jaji katika Mazingira kama Inavyoonekana P8 anayotaka Kuitoa hawezi Kuwa Sheria hiyo Haipo Katika Vitabu Vyetu Vya Sheria. Hoja hiyo Haina mashiko Tuna Criminal Procedure Moja tu..

Objective Ni sahihi kwamba Katika Mazingira Yale Palikuwa na Overriding Objective lakini Sasa Mazingira Yaliyopo Mbele Yako Mheshimiwa Jaji, Mazingira hayo hayapo Included katika Nyaraka zao Sasa Certificate of Delay ilikuwa haiwezi Kusimama, Kwa sababu Ilikuwa Pia inakwenda Kuangalia Kama Rufaa hiyo Ipo sahihi Mbele ya Mahakama na Kama Mahakama ina Uwezo wa Kuisikikiza Kwa Mazingira hayo hata Kama Wenzetu wataichukulia kuna Overriding

Wakili wa Serikali: Maazimio yalikuwa Katika Shauri hilo ni Tofauti kabisa, kwa Maana Ya Kwamba Kilichokuwa kinajadiliwa Kwenye Rufaa hiyo, Ni kukosekana kwa Barua Na Kwamba Barua hiyo ndiyo iliyokuwa inatoa Msingi Kwa Kutolewa Certificate of Delay, Sasa Kwa Sababu ya Barua hiyo halikuwa Mazingira hayo Mawili, Hivyo tupo katika Hatua Kwamba Nyaraka hii inaweza Kupokelewa na Mahakama yako tukufu Sasa tukirejea Mapingamizi ya Mawakili Wasomi Upande wa Utetezi

Pakawa na Tatizo la Kurejea Kifungu cha Sheria Ambacho akitumiki katika a Mazingira hayo Mheshimiwa Jaji tunarejea tena Kwamba Pamoja na Kukubalina na Hoja za Mahakama Katika Shauri hilo, lakini Kwa a Shauri hili Mazingira ni tofauti Mheshimiwa Jaji baada ya Kutofautisha

Wakili wa Serikali: Pia walirejea Shauri la John Marco Walirejea Kesi hiyo ya John Marco Dhidi ya Joshua Malimbe Wakisisitiza Swala la kunukui Kifungu kisicho Lakini tunarudia tena Kusema Kilichokuwa Mbele ya Mahakama Kuu ilikuwa ni Maombi ya Kuongezea Muda wa Kukata Rufaa Ndiyo Pakawa na hilo

Tunaomba Kurejea Shauri lililotamkwa Katika THE DIRECTOR OF PUBLIC PROSECUTION VS SHARIF ATHUMAN AND SEVEN OTHERS Katika Mahakama Ya Rufaa, Katika Paragraph ya Mwisho Ukurasa wa Saba na Paragraph Ya Kwanza Ukurasa wa nane WS Robert Kidando: ANASOMA hizo Paragraph.

Wakili wa Serikali: Hakuna hata Mmoja anayelalamikia Kwamba palikuwa na Ukiukwaji wa Sheria Non Compliance Kwenye Kupatikana kwa Nyaraka hii iwe Kwa Criminal Procedure Act au Kwa Sheria Nyingine yoyote Mheshimiwa Jaji Kanuni zinazoongoza Kupokelek wa kwa Nyaraka hizo, zipo wazi kabisa.

Wakili wa Serikali: Kwamba Kuna Mambo Matatu yametamkwa katika Shauri hilo ni RELEVANCE REALITY AND COMPETENCE Katika Jambo hili hakuna hata sehemu Moja limegusa Ushahidi huu katika Eneo hilo Hivyo Mheshimiwa Jaji kwakuwa hakuna Jambo hilo Tunaona Kwamba Mapingamizi ya Wenzetu Yamekosa mashiko Katika Kuleta Changa Moto Hati ya Ukamataji Mali (Seizure Certificate) Hoja Nyingine Mheshimiwa Jaji Ukiangalia Certificate Of Seizure ya Shahidi wa Nane anayoitolea Ushahidi inaonekana wazi kabisa

Na Kwa Sababu Shahidi aliye fanya Zoezi hilo Yupo Mbele ya Mahakama Nyaraka hii haiwezi Kuwa Challenged kwa aina ya Mapingamizi yaliyowasilishwa na Mawakili Wa Utetezi Hivyo Mheshimiwa Jaji tunaomba Pingamizi zote zilizowasiliahwa zituliliwe Mbali na Uweze Kupokea hiyo Seizure Certificate iliyotolewa na Shahidi Wa Nane Mheshimiwa Jaji kama Wakili analo la Kuongezea, Mimi naishi hapa Wakili wa Serikali Pius Hilla anasimama.

Wakili wa Serikali: Kuna CPA na The Police force and auxiliary Act ambayo pia Inakufungu cha 35 ambayo inampa Mamlaka Askari Police Kufanya Upekuzi Kama Ilivyo Kwenye Kifungu cha 38 cha CPA Hivyo Mheshimiwa Jaji na rejea Vifungu hivyo viwili 38 na 35 Kuonyesha Kwamba Kule Kilichokuwa Kigezo Cha Uhalisia Shahidi Wa 08 amekidhi ndiyo Maana Wenzetu hawakutaka Kujieleza huko Mheshimiwa Kuleta hapa Maswala ya Kunukuu Kimakosa Kwenye Nyaraka Kama hii, Ambapo Kwa Nyaraka iliyokuja hakuna Kitu kama hicho

Lakini pia Unaongozwa na Ushahidi wa Shahidi aliyepo Kizimbani Ambapo Shahidi Anapaswa Kutengenezea Misingi, Je Shahidi anaufahamu. Je Nyaraka ni halisi, Na hiyo ya Relevance ambayo imefanyika Vizuri. Haya Ndiyo Maswala Ya Msingi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji limezungumza swala la Wrong Citation ni Kwamba Uhalali wa Kielelezo Mheshimiwa haiwi Covered na Vifungu ambavyo Vilitumika Kwenye Documents Uhalali unaongozwa na Kanuni ambazo Zipo Kisheria ambazo Mwenzangu ametamgulia Kuzisema

Wakili wa Serikali: Hivyo Mheshimiwa Jaji tunaomba Pingamizi zote zilizowasilishwa zitupiliwe Mbali na Uweze Kupokea hiyo Seizure Certificate iliyotolewa na Shahidi Wa Nane Mheshimiwa Jaji kama Wakili analo la Kuongezea, Mimi naishi hapa

Lakini pia Unaongozwa na Ushahidi wa Shahidi aliyepo Kizimbani Ambapo Shahidi Anapaswa Kutengenezea Misingi, Je Shahidi anaufahamu, Je Nyaraka ni halisi, Na hiyo ya Relevance ambayo imefanyika Vizuri, hayo ndiyo masuala ya msingi.

Wakili wa Serikali: Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji limezungumza swala la Wrong Citation ni Kwamba Uhalali wa Kielelezo Mheshimiwa haiwi Covered na Vifungu ambavyo Vilitumika Kwenye Documents Uhalali unaongozwa na Kanuni ambazo Zipo Kisheria ambazo Mwenzangu ametamgulia Kuzisema yamekidhi Mheshimiwa Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji tunailila Mahakama Yako Kwamba Ione Mapingamizi hayana Uwezo ya Kuzuia Seizure Certificate na tunaomba Mapingamizi Uyatupilie Mbali WS Pius Hilla anaketi chini..

Kitu kama hicho Masuala ya Nukuu za Vifungu yanapaswa Kuletwa pale ambapo Mahakama inakuwa Moved in a Proper, pale ambapo Inakuwa ina Gurantee Orders Tofauti na Mazingira ya Kwetu Shahidi ndiye anapaswa Kutengeneza Misingi Na Maswala yote ambayo Shahidi anatemgemza Ushahidi

Wakili wa Serikali: Kwa Ushahidi uliotolewa na Shahidi Wa 08 zimekidhi KWAMBA Zimezingatiwa, Kigezo Cha Uhalisia Shahidi Wa 08 amekidhi ndiyo Maana Wenzetu hawakutaka Kujieleza huko, Mheshimiwa Kuleta hapa Maswala ya Kunukuu Kimakosa Kwenye Nyaraka Kama hii, Ambapo Kwa Nyaraka iliyokuja hakuna

Nyaraka yao ya Mawasilisho inapelekwa Kwa Jaji

Jaji: Kwa hiyo mmemaliza? Wakili wa Serikali: Ndiyo Mheshimiwa Jaji Nashon: Mheshimiwa Jaji Kwa kuanza,

Jaji: Mmefanikiwa Kupata Nakala na ninyi? Nashon Nkungu: Hatujapewa nakala WS: Mheshimiwa Hatukufanikiwa Kutoa Copy

Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji Ni sahihi Kabisa Kifungu 20 kiliwekwa Kwa Mazingira kadhaa wa Kadhaa bila Kututoa Nje ya Mazingira yetu Ukisoma Kifungu cha 20 Utaona Inazungumzia Mazingira tofauti A Mazingira tofauti B Mazingira tofauti Na C. Mazingira tofauti

Nashon Nkungu: Ukisoma Sheria hii lKifungu cha 14 Utaona Maana ya "Or" Ni Kwamba Inatumika Disjunctive, Ukitaka Risk ya Kutoa Full Citation unakuwa Umetakiwa Ku Cite Kila Kitu, Ukitake Risk ya Ku Cite Full Citation Uwezo Kuja Kudai Advantage hapa Mahakamani

Kulitafuta na was Ione Sheria Hiyo utakuwa umewanyima Haki zao, Sisi tunaona Kuna suala la Kuwanyima Haki zao, Pomia Kuna Hoja ya Wakili wa Serikali Robert Kidando Kwamba Hatukuonyesha Ukiukwaji wa Sheria, Hii mbona Inaenda Sawa kabisa na Ukiukwaji Wa Sheria za Nchi hii

Nashon Nkungu: Kwa sababu Utakuwa umetegenzea Mkanganyiko, Uki' take Risk ya Kuweza Ku Cite Unatakiwa aku Cite kitu ambacho ni Proper la sivyo Utakuwa Unatengeneza Confusion. Pia Washtakiwa kuhusu Haki yao, kwakuwa Washtakiwa walishapewa Nyaraka hizi na Kwamba walienda

Kinyume na Sheria, Ambapo Haupo kwenye Main yao wala Kwenye Majibu yetu Jaji Mimi nimemuelewa Kwamba amesema Anaomba atukumbushe Kwamba Kuna Kanuni Nyingine Katika zile Principle zenu 3 ambayo ni Ushahidi Usiwe Umechukuliwa Kinyume na Sheria

Nashon Nkungu: Kwamba ametuambia hapa Kesi ya DPP VS Athuman Sharif, Tunaomba Kumkumbusha Kwamba Moja ya Kanuni za Ushahidi ni kwamba Ushahidi Usiwe Umepatikana Kinyume na Sheria

Wakili wa Serikali: Pius Hilla OBJECTION Mheshimiwa Jaji Wakili anaongelea Kwenye Masuala ya Uchukuaji wa Ushahidi

Alieleza Pia Kuwa Shahidi Ndiye anabeba Comptence ya Nyaraka, Siyo Sahihi Sababu Kuna Nyaraka ambazo zinaweza Kuletwa Zenyenwe Bila Shahidi Kwa Hoja zetu hazi serve Porpose, Tunapinga Kwa Sababu hili ni suala la Msingi Sana kwa Wateja wetu.

NASHON Nkungu: Kusema Kwamba Hakuna Hoja hata Moja ambayo haimo kwenye Sheria hii Sisi tulichofanya tumekataa nyaraka kwa Sababu Siyo Competent Na kwanini Siyo competent ni kwa sababu hii ni Nyaraka ya Kisheria siyo tu Nyaraka ambayo unaweza Kutengeneza Vyovyote

Nashon Nkungu: Mahakama hii Izingatie Hoja zetu ambapo sisi tunaona Nyaraka hii ni Mfu, Tunaomba Mahakama Yako iweze Kubalance, Nahitimisha na wasilisho langu la awali kwamba naomba Nyaraka hii isiingie Kama Kielelezo Cha Mahakama, Kwakuwa haina Sheria inayotambulika Rasmi

Tafsiri yangu ni Kwamba anaelewa Kwamba hiki kilicho andikwa Hapa Hakikidhi Pia alirejea Sura ya Kwanza wa Tafsiri ya Sheria zetu ana akajiongoza Sehemu Ndogo Sana 20 (1) Kuna Mahala Muhimu sana hakutaja Mahakama iangalie, Mimi Nitataka sasa Mahakama Ingalie Kifungu 20(3)

Mallya: Mheshimiwa Jaji Mambo Mawili Muhimu Mahakama ikaya' note, Jambo la Kwanza Wakili wa Serikali Msomi Robert Kidando amekiri hakuna Sheria iliyofanyiwa marekebisho Mwaka 2018 Pili, Amekiri Kwamba Tangu Mwaka 1993 Mpaka kesi hii inaanza Hakuna Marekebisho ya Kifungu cha 38

Mheshimiwa Jaji tafsiri yake Neno "NA" ni kwamba ukavisome kwa pamoja Sasa Usijusumbue Mheshimiwa Jaji wala Vifungu hivyo havipo Kwenye hiyo Sheria ya 2018 Marejeo tushasema ni Kifungu cha 20(3) Kwa Sheria za Utafsiri Kaka yangu Kidando ajue maana ya Heading

Mallya: Ukitaka Kurejea Sheria Unapaswa Usome pia Kifungu hiki, Mahakama iangalie Sasa Kwanini Wakili Kidando amekimbia Kifungu hiki Amasema tuangalie kuhusu Kifungu cha 35 sasa asome Pale Juu Kwamba NYARAKA HII IMEANDALIWA KWA KIFUNGU CHA 38(2) NA KIFUNGU CHA 35

Mallya: Hapa Hakuna Mahala ambapo Shahidi ametengenza Msingi, labda atuambiw Kwanza Amechukuaje Mali za watu kwa Sheria ambazo hazipo Kisha ndiyo aje atuombe hapa Hapakuwa na Ufuatwaji wa Sheria, Aliwasainisha watu Kwa Sheria ambayo Haipo Mheshimiwa Jaji ya kwangu ni hayo tu

Kutaja Kwa ufupi Labda swali litakuwa Tukirudi kwenye Kielelezo Je wametaja Sheria Kwa ufupi? Jibu ni Hapana.. Na Kama waliangalia Kwa Kutaja CAP Namba Wasingeandika Mpaka Mwisho, Alichotaka Kufanya ni Marekebisho Ya Kielelezo Chao IP 1, ambapo sisi tunaona sio sahihi..

Fredrick Kihwelo: Kabla Sijazungumza yale niliyopanga Kuzungumza naomba Nimuunge Mkono Wakili wa Serikali Robert Kidando Kwamba Kuna Criminal Procedure Act Moja tu, Ambapo nakubalina na Yeye kwamba ni CAP 20 na Marekebisho yake ya 2019, Hakuna ya Ziada, Na Kwamba Sheria Inaweza

Fredrick Kihwelo: Katika Mawasilisho Yao Mawakili wa Serikali hawajatoa Rejea ya kesi yoyote ambayo inasema Kukosewa Kwa Rejea siyo Hoja, Kwa hiyo ni Maombi yetu Nyaraka isipolelewe kwa kuwa wameleta Kinyume na Sheria, Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji...

Ndiyo hoja yetu unakuja kwamba Rejea Ilitakiwa CAP 20 ya 2019, Compliance lazima Uwepo ambapo Chief Government Printer anaitaja Sheria husika, Hakuna Upenyo Wa Kuingiza hapo, Kama ambavyo Maamuzi Yakisha fanyika Kwenye Mahakama ya Ardhi, Ndiyo Maana Kutumika "Neno " May

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nianze Na Kifungu cha 20 cha CAP 1 ambapo kama Wenzetu, "Where a written Law feffred to....." Kwa hiyo Neno ACT hayakutumika Kwa Bahati Mbaya, Lakini tunasisitiza Kifungu C hayo Maneno Hayakutumika Kwa Bahati Mbaya...

Kwenye kesi Ya Mwenderosi tunachokiangalia siyo Material Bali ni Kanuni hasa panapokuwa na Masuala ya lazima ya Sheria.. Ukikosea unakuwa Umepoteza. Kwenye Kesi Ya John Marco ni Hoja kwamba Wrong Citation is Facto, nashukuru Hawajapinga hilo..

Kibatala: Ukitake Risk kutaja Sheria Nzima Ujue hupaswi Kuchanganya, Kama ambavyo Mchapaji Mkuu anaitaja Sheria husika, Kwanini Hiyo Documents imechukua Uamuzi wa Kurejea Sheria Yote na Je Nini Kiliwafanya Wachague kuandika Sheri Yote..

Nyaraka wakati Umenukuu Sheria isiyo, Jibu ni Hapana, Na Pia statutory Document na awajabisha Wenzetu kwamba ID1 Ni statutory Documents, Kwamba Power ambazo Zipo purported Zenyenwe..

Kibatala: Hoja yao Kwamba Nyaraka hii siyo Motion inayohitaji Kuzingatiwa Zaidi, Hiyo ni Fallacy Argument, Kwa sababu Documents Unahitaji Competence ya Shahidi, Na Relevance ya Document Yenyewe, Na Tutaoa Mfano Miwili Kwa mfano Umetoa Nottice to Produce Kama Umetoa Ombi la

Kibatala:
Na kwenye kesi ya Athuman Sharif na Wenzake wamezungumzia hiyo Relevance na Materiality ambapo Shahidi anatakiwa awe Competence, Hata act anayosema Wakili wa Serikali Robert Kidando Yenyewe Inamatatizo tuh, Namaliza Kwamba Mapingamizi yetu ni ya Muhimu na halali.

Asante sana Mheshimiwa Jaji Kibatala anaketi, Jaji anaendelea kumaliza kuandika, anaomba ile Nyaraka...

Jaji: naombeni ile Document

Jaji: natizama muda naona kama sitoweza kufanya maamuzi muda huu, Kwa maana hiyo naomba tuhairishe mpaka kesho asubuhi Mawakili wa pande zote wanakubaliana nae

Jaji: Utetezi kuna Nyaraka yangu nimewaazimisha naiomba

Kibatala: Correct

Jaji: Shahidi tunakuonya kwamba, kesho utatakiwa kuwa tena mahakamani Saa 3 Asubuhi, Na washtakiwa wataendelea kuwa chini ya Magereza mpaka kesho asubuhi saa 3

Jaji amemaliza, anatoka
 
Tupo tunafuatilia, quorum (akidi) ya kijiwe chetu pia imekamilika kusikiliza kijiditali mwenendo wa kesi hii kwa umakini kinachoendelea huko mahakamani.

UZITO WA PINGAMIZI LA UPANDE WA MAWAKILI WA UTETEZI KUHUSU HATI YA KUKAMATIA MALI HAUKUFUATA SHERIA ZA TANZANIA WACHAMBULIWA




AWALI MTAFARUKU BAADA YA WATU WAZUIWA KUINGIA LEO 8/11/2021 MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI
08 November 2021 .Taharuki Nzito Yajitokeza Leo Mahakamani, Mawakili Wa Mwenyekiti Wa Chadema Freeman Mbowe Watishia Kujitoa Katika Kesi


Baadaye watu waruhusiwa kuingia na kesi ikaendelea kufuatia mawakili wa upande wa utetezi kuelezea umuhimu wa umma kupata haki ya kusikukiza mwenendo wa kesi

MWANZO MWISHO WA KILICHOTOKEA LEO KESI YA MBOWE, KIBATALA ATOA PINGAMIZI ZITO JAJI ASIMAMISHA KESI


 
Baada ya Ijumaa kesi kuahirishwa, Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani.

Leo Jamhuri inaleta shahidi mwingine. Kuwa nami.

=====
Huyu Jumanne ndiye yule akiwa na wenzake walimuwekea mzee wa watu meno ya ng'ombe kwenye mizinga yake na wakamwambia Ni meno ya Tembo wakampola milioni 100?

2754997_Ar1.jpg
 
Baada ya Ijumaa kesi kuahirishwa, Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani.

Leo Jamhuri inaleta shahidi mwingine. Kuwa nami.

=====

Jaji ameingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa

WS Robert Kidando anasimama

Jaji: Ndiyo
Huyu jumanne ndo aliefukuzwa na kazi??
 
Ushahidi wa Leo ni mzito Sana ukizingatia huyu shahidi ni msukuma timu jiwe pia, mahita aliulizwa kama huyu Jamaa kasimamishwa kazi patamu hapa maswali kibao, maswali ya kumpakazia mtu ndovu yatakuepo Leo, kipindi Cha jiwe mabilionea wa uwizi nusra waibuke , Mungu muweza wa yote
 
Baada ya Ijumaa kesi kuahirishwa, Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani.

Leo Jamhuri inaleta shahidi mwingine. Kuwa nami.

=====

Jaji ameingia
Huyu ndie alimuwekea Mzee Maeda pembe feki za ndovu kwenye mzinga wa nyuki. Na kudai milioni mia. Ati leo ni shahidi kesi ya ugaidi.
Tena anatoka Arumeru kwenda kukamata Moshi, kwenye utawala wa RPC / OCD mwingine bila taarifa. Yaani Siro ni ZERO kabisa na hii filamu yake.
 
Baada ya Ijumaa kesi kuahirishwa, Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani.

Leo Jamhuri inaleta shahidi mwingine. Kuwa nami.

=====

Jaji ameingia
Hadi raha yaani kila nukta dereva ana tajwa. Baada ya juzi Mahita kuchafua hali ya hewa. Huyu kapelekwa darasani kwamba asisahau kumtaja dereva. Hii movie ni ya utopolo kabisa hii.
 
Back
Top Bottom