Patriote
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 1,718
- 1,047
Nape ni msemaji mkuu wa tume ya uchaguzi???mbona mnatuchanganya??matokeo halisi si yanatangazwa na Tume??Nape katoka wapi hadi aisemee tume ya uchaguzi??tutaamini vip hayo matokeo?? Wakati hizo taarifa zinawasilishwa kwa Nape kutoka Tume ya uchaguzi Nape alikuwa mwenyewe wakati anayapokea hayo matokeo??mbona hapa anataka kutujengea hofu juu ya utaratibu mzima wa kutoa matokea???Kwa mujibu wa matokeo ya Nape Nnauye CCM imepata kura 26266 na CDM kura 22443, hii ikiwa ni tofauti ya kura 3823. Kwa wachambuzi makini wa siasa(wasio na ushabiki), ushindi huu si dalili njema kwa CCM, kwa sababu zifuatazo:
1. CCM imeporomoka kutoka kura 35674 hadi kura 26266 ikiwa na maana zaidi ya wapiga kura 9408 wameikataa CCM ndani ya miezi 11
(okt 2010-sept 2011)
2.Upinzani umepanda kutoka kura 11321 hadi zaidi ya kura 22443, ikiwa na maana kuwa imani kwa upinzani imeongezeka
3. CCM imeshindwa kuvunja rekodi yake yenyewe, kwa hiyo anayetakiwa kutembea kifua mbele si CCM bali CDM
Nasema hii ni dalili mbaya kwa CCM kwa kuchukulia mfano thabiti wa Uchaguzi mdogo wa jimbo la Biharamulo julai 2009. CCM walishinda kwa kura 17561 dhidi ya upinzani uliopata kura 16898(CDM 16700 na TLP 198), lakini ulipofanyika uchaguzi mkuu 2010, CDM waliibuka kidedea baada ya kulitwaa jimbo hilo.
Kama taarifa ya Nape ni sahihi, CCM wanaweza kufurahia kwa kuwa wameudhibiti ubunge wa Igunga, lakini wasifurahie kuwa wameshinda. Ni ishara nzuri sana kwa CDM na wapenda mageuzi kwa ujumla, hata Nape na makada wengine wa CCM wanajua hili.
CCM, TAA NYEKUNDU IMEWAWAKIA. FURAHINI KWA TAHADHARI
I STAND TO BE CORRECTED