Maalim Seif: Tunataka Zanzibar yetu!

Maalim Seif: Tunataka Zanzibar yetu!

Lakin tatizo halikimbiwi hila ni kulitafutia ufumbuzi,na huko Zanzibar nako ni muungano wa Unguja na Pemba bado pia matatizo yatakuwepo,kuvunja muungano cyo suluhisho ndugu.
 
serikali tatu ni porojo. Muungano uvunjwe, kwani zanzibar ni nchi huru. Kama kuna umuhimu wa kuwa karibu basi iwe shirikisho kama ilivyo jumuiya ya afrika mashariki. Mbona uganda na kenya hamkuzifanya serikali mbili. Hii ni kwasababu ni nchi kubwa na msingeweza kuziburuza. Acha zanzibar iwe huru wajipangie mambo yao kama tanganyika inavyo takiwa kuwa huru. Na hii imeleta matatizo sana wakati wa sharehe ya uhuru kujua ni uhuru wa tanganyika au tanzania
uvunjweeeee......!
 
Mkuu Muungano huu hautavunjika kirahisi kama unavyodhani!

Hautavunjika kirahisi...kwa maneno mengine unaweza kuvunjika ila kwa ugumu fulani hivi....maelezo yako yanalandana kwa mbali kama mawazo niliyoweka hapa jamvini jana ambayo ni:-

Kuna wanzanzibar kule hawataki kabisa Zanzibar ijitenge na Tanzania...! Ila kwa sababu ya ubabe na uoga wa watawala fulani huko basi wazanzibar hawa wanaendelea kukaa kimya.

Na hili kuthibitisha haya...siku Zanzibar ikijitenga kutoka Muungano wa Tanzania. Wazanzibar wengi wataomba kuamia Tanzania.

Ila mbaya zaidi kwa Zanzibar inayolazimisha kujitenga (kwa kutengeneza mazingira ya kuikwa Tanzania) ni kuwa wazanzibar waliokimya watalazimisha Kisiwa kilicho na ikulu ya Zanzibar kiwe sehemu ya Jamhuri ya Tanzania. Na hapa ndipo hawa wanaoshadadia kujitenga kwa Zanzibar kutoka Tanzania watakapoonja joto ya jiwe.

Subirini muone.
 
It is just a matter of time, Muungano huu wa kulazimishana utabaki historia.
 
Lakin tatizo halikimbiwi hila ni kulitafutia ufumbuzi,na huko Zanzibar nako ni muungano wa Unguja na Pemba bado pia matatizo yatakuwepo,kuvunja muungano cyo suluhisho ndugu.

Alie kuambia pemba na unguja ziliungana nani?au wewe ndie wale?
 
Tokea nikuone humu, leo naona kama umeanza kupona kwamba, kidogo yamekuwa kama mawazo ya mtu timamu

Wingu leo hamna.

By the way, huu Muungano mimi sielewi ni kwa faida ya nani. Warioba anasema ni bora kutumia gharama kubwa kuendesha serikali 3 vinginevyo Muungano utavunjika. Sasa mi najiuliza, ukivunjika tunaugua wapi?
 
Lakin tatizo halikimbiwi hila ni kulitafutia ufumbuzi,na huko Zanzibar nako ni muungano wa Unguja na Pemba bado pia matatizo yatakuwepo,kuvunja muungano cyo suluhisho ndugu.

Hayo ya Unguja na Pemba hayatuhusu , shauri yao ! tumechoka kubebeshwa gunia la misumali .
 
Wingu leo hamna.

By the way, huu Muungano mimi sielewi ni kwa faida ya nani. Warioba anasema ni bora kutumia gharama kubwa kuendesha serikali 3 vinginevyo Muungano utavunjika. Sasa mi najiuliza, ukivunjika tunaugua wapi?
Ukweli ni kwamba watu ni wanafiki. wenye akili timamu wanajua muungano ni huu hauna chochote cha maana, hivyo wanaogopa kusema moja kwa moja hakuna muungano, hivyo taratibu wana anzia kwa serikali tatu...Baadae watasema hakuna haja ya gharama za serikali ya muungano kwanza hauna faida, hivyo wataunjilia mbali. kama sikosei haya maswala ya viongozi wa din kuuwawa inawezekana kabisa ilikuwa ni njia ya kuwaonesha WaTanganyika kwamba wazanzibar hawataki kulzimsishiwa huu muungano
 
Uacheni Muungano ujivunje wenyewe Taratibu , maana baada ya serikali 3 , katika kipindi cha miezi 6 tu ya mwanzo , muungano Utabomoka wenyewe , wala hakuna haja ya kutoa Mapovu ! Kwa rasimu hii Muungano Chali miguu juu !
 
Lakin tatizo halikimbiwi hila ni kulitafutia ufumbuzi,na huko Zanzibar nako ni muungano wa Unguja na Pemba bado pia matatizo yatakuwepo,kuvunja muungano cyo suluhisho ndugu.

Alichokiunganisha mwanadamu, ruksa kukitenganisha isipokuwa hawezi kukitenganisha alichokiunganisha Mungu pekee. Muungano uliopo wa serikali mbili umeprove failure. Hali halisi inajionyesha na haihitaji kuambiwa. Kama bado tunautaka Muungano, ni budi tuuvunje kwanza huu uliopo na tutafute muundo mwingine ambao wananchi wa kila nchi watakubaliana nao.
 
Mkuu Muungano huu hautavunjika kirahisi kama unavyodhani!
Kwa kuwa lengo kuu la muungano lilikuwa kudumisha usalama na ulinzi katika pwani yetu; na kwa kuwa suala la maendeleo lilichukuliwa for granted kuwa yatapatikana; na kwa kuwa Zanzibar sasa baada ya kujiridhisha na usalama wake; na kwa kuwa Zanzibar inadhani kuwa kuendelea kuwa ndani ya muungano kunachelewesha maendeleo yake na ustawi wa Wazanzibari; na kwa kuwa Zanzibar inataka kujenga uchumi wa huduma(Service economy) badala ya uchumi wa rasilimali;

Basi ni wakati muafaka kwa muungano kuvunjwa kwa maslahi ya pande mbili! Kuendelea kuwa ndani ya muungano kutachelewesha maendeleo ya pande zote mbili na kuleta mfarakano ambao unaweza kusababisha uvunjifu wa amani!
 
Uacheni Muungano ujivunje wenyewe Taratibu , maana baada ya serikali 3 , katika kipindi cha miezi 6 tu ya mwanzo , muungano Utabomoka wenyewe , wala hakuna haja ya kutoa Mapovu ! Kwa rasimu hii Muungano Chali miguu juu !

Sawa kabisa utachomoka lakini wale jamaa wa JWTZ.......,!!!
hawata chomoka na nikosa kubwa kuliko kujiuwa kuwazungumzia
 
Chris, lkn serikali tatu sio sera ta CCM! Au nawe ni mpinzani ndani ya CCM?
Kuwa CCM sio lazima ukubaliane na kila kinachosemwa na CCM.
CCM ni binadamu kama wewe na wanaweza kufanya makosa kama wewe.

Suala la muungano sio suala la ccm ni suala kitaifa
 
Back
Top Bottom