Maalim Seif Hamad apinga CUF kuungana na CHADEMA

Maalim Seif Hamad apinga CUF kuungana na CHADEMA

huu uzi naona unachangiwa na watu wa ajabu ajabu tu,tena wanasapotiana ujinga ujinga,ngoja me nipite zangu.
 
...........CHADEMA KITASIMAMA KWA
MIGUU YAKE YOYOTE NA HAKIHITAJI
MSHIRIKA YEYOTE KATIKA JAMBO
LOLOTE.........

Nimepapenda hapo km ndivo alivomalizia.
 
Mkuu Ben lisemwalo lipo. Kama Katibu Mkuu amesema kuwa CHADEMA wamepewa fedha kuvuruga mchakato wa katiba, watashindwa vipi kuwahonga hao akina mtatiro na baadhi ya wabunge kufanikisha mpango wao?

ishu sio kusema ishu ni facts za malipo hayo. ishu ni nakala ya maandishi ya sharif akiwatuhumu wenzake amasivyo hii ni project ya lumumba kujaribu kulaghai watanzania. lakini mwsho wa siku raisi alisha waasa mjiandae kisaikolojia kupata msio ya tarajia...nafkiri alishawasoma vyema tu na muswada kama hata usaini atakuwa amewapa ujumbe mzito.
 
Kama kweli Maalim Seif ndiye kayasema haya basi atakuwa ni kiongozi mpuuzi sana mwenye kiwango cha juu cha ubinafsi.
SMZ haiwezi kuwawakilisha waqzanzibari katika suala la sheria mama ya katiba. Ni muhimu na lazima wananchi na wadau wengine nje ya serikali watoe maoni yao kwakuwa SMZ ilishirikishwa na serikali ya JMT kuandaa muswaada lakini ulipofikishwa bungeni basi kamati ya bunge inawajibika kwenda kwa wadau wengine kutafuta maoni yao kitu ambacho hakikufanyika.
Sitaki kuamini kwamba Maalim Seif ndiye mwenye kauli ya mwisho kwa mambo ya cuf hata kama wanachama wengi wanataka ushirikiano wa cuf na Chadema yeye peke yake anaweza kupinga na kuizuia cuf kushirikiana na Chadema kwakuwa ccm wanamshinikiza cuf isishirikiane na Chadema.
Bado nasubiri kauli rasmi ya cuf bila shaka Julius Mtatiro atatusaidia kuweka sawa jambo hili.
 
Last edited by a moderator:
Ngoma bado mbichi huyo ndiyo maalim nadhani wazanzibar wamemsuta kuungana na makfir chadema ingekuwa ni kuitukana zanzibar.

Kwenye ishu ya katiba wazanzibari ukafiri wameuweka pembeni, wanapambana na wahuni ccm wanaoshirikiana na Maalim Seif.

Sema lingine.....

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kwani kwa akili ya kawaida tulitegemea Maalimu aseme nini kwenye hili ?

Kwani nani hajui kua hata hiyo CUF yenyewe kaisaliti? wewe unadhani kwa msimamo ule wa CUF enzi zile hadi ikasababisha watu wapoteze maisha na wengine kupatwa na vilema vya kudumu kama wangejua wanafanya hivyo kwa aajili ya kumtafutia Maalimu ulaji wangejihangaisha kutoka hata majumbani mwao?

Anachokifanya Maalimu hapo sio kwa ajili ya maslahi ya wanzanzibar na watanzania hata kama CHADEMA wakija na hoja zenye mashiko kwa kiasi gani naamini asinge kubali kuungana nao .

Utani kidogo _CUF wanabahati yaani wangejitera tu kidogo wangeshuhudia mtiti wake twenty fifteen ,hata hivyo bado tuna nafasi kubwa ya kuungwa mkono na wanainji hata bila hao waliberali na lichama lao.
 
CCM hatuna muda wa marumbano. Waacheni wafu wazikane.

CUF wamezishtukia siasa za kisanii na kilaghai za CHADEMA.

Marriage of convenience. Mmoja hana base bara na mwingine hana base visiwani.

Hivi vyama ni kichekesho.

They'll never step out of their closed door and 2014 is just around the corner.


sasa mbona umeongea pumba sasa,
kama chama kimoja hakina base bara,na kingine hakina base visiwani,means vingeungana vingeweka base ya uhakika to the both sides,
Inashangaza kijana kuacha kutetea maslahi ya kitaifa pale yanapoikuba na kuvaa unazi wa kichama sampuli hii,hovyo kabisa
 
Anataka kutuaminisha kuwa cuf ndo wazanzibar,na kauli zake nibora zingetolewa na wazanzibar na wala sio Seif.na wenye kusema Chadema kinapotosha ni Wazanzibar na si vingine.
Wazanzibar mtanbue Seif alishaona bila kula na ccm hataongoza,hivyo hoja ya ccm iwe ya msingi, isiwe yamsingi lazima aipigie upatu ili aendelee kutawala.
Seif huna lakutwambia hapo.
 
Ndoa sasa itakuwa ndoano sikujua kama chadema ndiyo alikuwa mke na cuf ndiyo mume au vinginevyo.

Mbona husemi kuwa CDM walikosea kutaka kumuoa mke amba wanajua alishafunga ndoa na CCM. Huenda Maalimu kaona mbali hasa ukizingatia ugumu wa kutumikia ndoa mbili
 
Mkuu, sidhani kama kulikuwa na ndoa hapo ila nilichobaini ni kuwa CHADEMA (mwanamke) alikuwa anamtamani CUF (mwanaume) ila alikuwa anashindwa kumtongoza kwa kuogopa kuchomolewa na kuitwa malaya. uvumilivu ulipomshinda mwanamke akajitosa kumtongoza mwanaume na sasa amechomolewa
Sioni sababu ya kijana handsome(chadema-utamani mke wa mtu@CUF)
 
Kama ni kweli,Anapotuhumu viongozi wenzake kuwa wamehongwa na CHADEMA kwanini isiwe yeye kuwa amehongwa na CCM?
Kati ya viongozi hatari kabisa wa CUF ni huyu Maalim Seif,tuhuma alizotoa dhidi ya viongozi wenzake ni nzito(wao kuhongwa)kwa nini asingewasiliana nao kabla ya kutoa tuhuma hizi kwenye vyombo vya habari? Haoni kuwa amewadhalilisha..?
(2) Umoja ni Nguvu siku zote haoni kuwa ni bora akaungana na vyama pinzani kwa ajili ya kuiwajibisha serikali ya CCM hasa kwa yale ambayo ni ya muhimu sana kitaifa kama suala la Katiba Mpya kwa ajili ya maslahi ya wanainchi na nchi yao zaidi na sio chama..?
(3) Yeye kama Katibu Mkuu wa CUF kwa tamko hili hajamtendea haki Mwenyekiti wake wa chama(Prof.Lipumba) hata kama ameona amekosea isingekuwa busara kumtamkia maneno kama hayo hadharani(anacheza ngoma asiyoijua) jambo hilo ni hatari sana kwa Demokrasia ndani ya chama....anajaribu kuhodhi na kuteka nyara fikra za wanachama wenzake bila hata ridhaa yao(nenda kaseme)
(4) Wana CUF kwa maslahi ya Demokrasia ya hapa nchini kwetu Tanzania ambayo bado ni changa sana na ambayo sisi kama wanainchi lengo letu ni KUIKUZA na KUIBORESHA siku hadi siku,tuwe makini sana,na kufuatilia kwa karibu usemi na mienendo ya viongozi kama hawa ili hatima yake sasa na baadae, tuondokane na kujenga Imani kwa viongozi kama hawa na kuondokana na UTUMWA HUU WA DEMOKRASIA CHANGA ndani ya vyama vetu na Taifa kwa ujumla.
 
  1. Lakini maalimu Seif akumbuke hakuna uadui ktk siasa ila kuna propaganda aangalie Kenya vyama vilivyopingana lakini mwishoni vikaungana ili kutimiza malengo yao.NAomba tumuulize je SUK ambayo CUF Imeungana na CCM walikuwa marafiki?Si ndo hao walishirikiana na Yule jamaa Omari wa Mahita kuleta majambia feki eti wakisema ni ya CUF,wakajenga hoja kuwa ni cha kidini na kigaidi hadi kikaporomoka kiasi hiki?Iliposemekana CUF walishinda uchaguzi kukatokea matatizo makubwa sana hadi Tz ikazalisha wakimbizi kwa mara ya kwanza?Kama ndo hao hao CCM walianzisha yote hayo leo hii yupo pamoja nao ..ni lipi kubwa CDM walotenda ata wasikubalike ktk usirika?Na jee hayo wanayolalamikia ni kwa faida ya watu wote au ni chama pekee.Maalimu asiogope hawezi kupoteza ulaji alonao mbona?Kutoshiriki vikao ni haki yake kidemokrasia labda kama chama chake kitaamua vinginevyo.
 
Wadau,

Taarifa za kuaminika nilizopata kutoka chanzo cha kuaminika huko Zanzibar zinasema kuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amepinga kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama hicho kuingia makubaliano na CHADEMA ili kupinga muswada wa katiba mpya. Maalim Seif amenukuliwa akisema mbele ya baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa uamuzi huo si wa kichama bali ni msimamo wa baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao wamepewa fedha na CHADEMA ili wawe na msimamo wa aina moja. Maalim Seif anasema kuwa wanaoratibu mpango huo ni Naibu Katibu Mkuu, Julius Mtatiro kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge wa chama hicho kutoka Zanzibar. Taarifa zinasema kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Ibrahim Lipumba inaelekea kuwa ameingia kucheza ngoma ambayo haijui na matokeo yake anaonekana kupoteza mwelekeo na kukosa msimamo. Hoja zilizoainishwa na Maalim Seif za kupinga makubaliano hayo ni hizi zifuatazo;

  1. Hakuna kikao chochote cha chombo chochote cha kiutendaji na kimaamuzi cha CUF kilichoketi iwe Zanzibar au Tanzania Bara kujadili jambo hilo na kuweka msimamo wa chama.
  2. Maoni yaliyotolewa na Kambi Rasmi ya Upinzani juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba hayakuwa maoni ya vyama vyote vya upinzani bali yalikuwa ni maoni ya CHADEMA pekee waliyoandaa kwa muktadha wa kujipatia umaarufu Zanzibar
  3. CUF ni moja ya vyama vinavyounda serikali ya umoja wa Kitaifa Zanzibar. Kutokana na ukweli kuwa Serikali hiyo imeshirikishwa na yeye (Maalim Seif) ameshiriki katika kuboresha Muswada huo anaamini kuwa chama hicho kupitia Serikali ya Umoja wa kitaifa ambayo imepewa baraka na Wazanzibari wote kimeshiriki kutoa maoni yake. Hivyo madai kuwa Wazanzibari hawajashirikishwa si ya kweli na ni upotoshwaji mkubwa
  4. Misimamo ya viongozi wa CHADEMA dhidi ya Zanzibar mara zote imekuwa hasi na kwa hali hiyo hali iliyojitokeza ya viongozi wa chama hicho kujipendekeza kwa Wazanzibari imetafsiriwa kuwa ni ulaghai wa kisiasa.
  5. Zanzibar ina viongozi ambao ndio waliopewa dhamana ya kuwasemea Wazanzibari na si mtu mwingine ambaye misimamo yake dhidi ya Wazanzibari inajulikana
  6. Kwa muda mrefu, CHADEMA wamekuwa wakitoa kauli za kuudhi dhidi ya CUF na viongozi wake hasa wale wanaotoka Zanzibar kama vile CUF ni CCM B, CUF ni chama cha Kiliberali ambacho kinasupport ndoa ya jinsia moja na CUF imeolewa na CCM. Kwa kauli hizo, hakika muungano unaosema hasa na CHADEMA si wa kweli bali ni wa maslahi ya upande mmoja.
  7. CHADEMA wanataka kuitumia CUF kama daraja ili kujipatia wafuasi Zanzibar. hii ni kutokana na CHADEMA kuendelea kupoteza mvuto visiwani humo hasa kutokana na viongozi wakuu wa chama hicho kuwa na chuki binafsi dhidi ya Zanzibar. Aibu aliyopata Katibu Mkuu wa CHADEMA alipofanya ziara visiwani humo imechochea viongozi wa chama hicho kuona haja ya kuungana na CUF

Kutokana na hali hiyo, Maalim Seif ametoa msimamo ufuatao ambao anategemea kuuwasilisha kwenye vikao halali vya kiutendaji vya CUF na ambao amesema unaungwa mkono na viongozi wengi wa chama hicho;

  1. Yeye kama katibu Mkuu na mtu anayekubalika na kutumainiwa na Wazanzibari wengi hatashiriki kikao chochote na CHADEMA kujadili jinsi ya kukwamisha mchakato wa Katiba
  2. Yeye kama Katibu Mkuu hatashiriki ziara iliyotangazwa na CHADEMA ya kuzunguka nchi nzima kwa kile kinachodaiwa kuishtaki serikali ya ccm kwa wananchi
  3. CHADEMA wameonywa kutojipendekeza kwa CUF na wamekumbushwa msimamo wao kuwa CHADEMA KITASIMAMA KWA MIGUU YAKE YOYOTE NA HAKIHITAJI MSHIRIKA YEYOTE KATIKA JAMBO LOLOTE

Nawasilisha

CHADEMA haiwezi kuitegemea CUF, au kutegemea sapoti ya aina yeyote kutoka kwao, kwani ni ya kinafki na waTanzania wanajua unafki wa CUF

Mara baada ya Naibu spika kuwadhalilisha wabunge na KUB viongozi kadhaa waliongea na kutoa maoni yao akiwamo Ezekiel Maige wa CCM, naye kapewa hela na CHADEMA??

Zile taasisi za kijamii Zanzibar, zilizosema hazikushirikishwa kwenye maoni, pia zilipewa pesa na CHADEMA? na tuseme hata rasimu ya katiba iliyotoka ambayo inasema serikali tatu licha ya tume kupewa fedha nyingi kuandaa mchakato wa katiba walipewa pesa na CHADEMA ili kuleta serikali 3!

Jamani tuwe wakweli tuache siasa za kipuuzi, CHADEMA ina hela sana??

Maalim Seif anaogopa hatma yake 2015, hasa akiangalia moto wa Chadema, ni kweli yeye yupo kwenye serikali ambayo inataka kuchakachua maamuzi ya wananchi, ili apate credit anapaswa ajiunge na Chadema sio Chadema ijiunge naye,

Kama Chadema ingetaka kujiunga na wapinzani wake, ingejiunga hata Arusha, ingejiunga na CCM lakini mafuta na maji havichanganyikani

Prof Lipumba hakupewa hela na hata Mtatiro hakupewa hela ila they join to fight for the lost nation, they fight for Tanganyika, although they feer

Peapleeeees...... Poweeer

Joash Mussa
Member of Chadema
 
kuna thread imefutwa haraka niliweka challenge ya CUF ktk hili na umuhimu wa CDM kwa CUF...Nilijua maalimu hatakubali, ila desperately bila CDM kusema neno roho ya CUF haitopona.

CUF wanahitaji heshima, na heshima wataipata kwa kuipa nafasi nafsi CDM..ila itakuja with cost..kwa kukubali faida zote CDM watakazozipata....na CUF hawawezi pata vyote..yaani heshima bila CDM, na wakiikosa heshima ni wazi wataingia shimoni na CCM.

CUF wanahitaji kufuata Njia za CDM kwa kuwa karibuna na CDM ili wapate heshima ya kusimamia misingi ya chama,kuanzia mahakamani hadi uraiani.

Maalimu anayyo shida kukubalina na hiyo hali...nilijua atakumbushia udugu na CCM kuliko aone CDM wakipaa...anajua watakapoingia pemba na CDM km rafiki basi muda si mrefu watakuwa wkaigombania no mbili.

Mkuu utakuwa uli post utumbo kama kawaida yako ndio mana mods waka delete mkuu siku hizi umekuwa mzee huna hoja za msingi mkuu punguza viroba vya mchana jua kali
 
Kati ya viongozi hatari kabisa wa CUF ni huyu Maalim Seif,tuhuma alizotoa dhidi ya viongozi wenzake ni nzito(wao kuhongwa)kwa nini asingewasiliana nao kabla ya kutoa tuhuma hizi kwenye vyombo vya habari? Haoni kuwa amewadhalilisha..?
(2) Umoja ni Nguvu siku zote haoni kuwa ni bora akaungana na vyama pinzani kwa ajili ya kuiwajibisha serikali ya CCM hasa kwa yale ambayo ni ya muhimu sana kitaifa kama suala la Katiba Mpya kwa ajili ya maslahi ya wanainchi na nchi yao zaidi na sio chama..?
(3) Yeye kama Katibu Mkuu wa CUF kwa tamko hili hajamtendea haki Mwenyekiti wake wa chama(Prof.Lipumba) hata kama ameona amekosea isingekuwa busara kumtamkia maneno kama hayo hadharani(anacheza ngoma asiyoijua) jambo hilo ni hatari sana kwa Demokrasia ndani ya chama....anajaribu kuhodhi na kuteka nyara fikra za wanachama wenzake bila hata ridhaa yao(nenda kaseme)
(4) Wana CUF kwa maslahi ya Demokrasia ya hapa nchini kwetu Tanzania ambayo bado ni changa sana na ambayo sisi kama wanainchi lengo letu ni KUIKUZA na KUIBORESHA siku hadi siku,tuwe makini sana,na kufuatilia kwa karibu usemi na mienendo ya viongozi kama hawa ili hatima yake sasa na baadae, tuondokane na kujenga Imani kwa viongozi kama hawa na kuondokana na UTUMWA HUU WA DEMOKRASIA CHANGA ndani ya vyama vetu na Taifa kwa ujumla.

Maalim Seif, yupo kibinafsi na tamaa na tamaa ilimuingia mapema na akaridhika kuja kuitwa makamu wa rais, ni kiongozi aliyekata tamaa na kuona liwalo na liwe lazima niongoze

2015 sio mbali akigombea hata 25% hatapata Zanzibar, na hapo ndipo atashangaa ujinga alioufanya

CUF inaenda kufa, na CCM wanaenda kuwa KUB
 
Mkuu utakuwa uli post utumbo kama kawaida yako ndio mana mods waka delete mkuu siku hizi umekuwa mzee huna hoja za msingi mkuu punguza viroba vya mchana jua kali

wewe utakuwa mmojawapo ya hao mods....mbona matusi halafu huna evidence wala maelezo ya kuthibitisha unachoclaim......hujawahi fundishwa reasoning popote ktk maisha yako...?Naweza kufadhili ukasome hata beginners course..

Mbaya zaidi mwenyewe huna hakina ..."..Utakuwa.." halafu unaanza poromosha matusi km vile unaonge akitu real.....ipo kazi TZ...dada mmoja mkenya nairobi alikuwa nami bila kujua kuwa mim ni MTZ akamfukuza bitozi wa kitanzania,nilipomuuliza kwanini akaniambia hakuwa akipenda logic za watanzania....

km wewe logic ,ukimpa Fisi na uwezo wake wa kula kila kitu bado atakufa njaa porini..
 
Naona Anatoa Mawazo Yake Kama Yeye Ndo CUF Peke Yake Lipumba Kahongwa Pesa Mtatitro Kahongwa?? Hayupo Tayr Kuzunguka Tz Kuishtaki CCM Tena Kwenye Mchakato Ulio Andaliwa Na Chadema Huyu Mzee Ikulu Imemnogea Anaona Kama Cuf Wanataka Kuhalibu Mambo!! Viva Lipumba Viva Mtatiro Viva Mbowe

Kama ni kweli kaongea yawezekana ni uoga wa kunyimwa pension kama Mrema.....!!
 
Tusubiri hii habari itolewe kwenye vyombo vya habari ndio tujue kama habari ya kweli au sio ndio tuje kujadili au mods futa huu uzi
 
Sasa ngoma imeingia patamu. Sijui CHADEMA watakuja na lipi la kutueleza

habari hizo si za kweli. ni uzushi wa muandishi. nikweli hakuna makubaliano MOU kati ya CUF na CHADEMA lakini kuna common interest kwenye suala lianalozungumzwa.
 
Maalim Seif asiwe na haraka atakuwa Rais wa Pemba huru muda si mrefu maana rohoni huyu Bwana ndicho anachokitamani maana Uraisi wa Zanzibar {Pemba na Unguja} asahau kabisa.

Wakiwa ndani ya Muungano wanadai Zanzibar lakini nje ya Muungano kutakuwa na Pemba na Unguja - by J-Kambarage Nyerere.
 
Back
Top Bottom