Maalim Seif Hamad apinga CUF kuungana na CHADEMA

Maalim Seif Hamad apinga CUF kuungana na CHADEMA

Da mechi za kimataifa zimetunyima uhondo wa epl
 
hivi ni kweli kwamba njaa ndiyo ilimshawishi seif kukubali serikali ya mseto ?
 
Jamani hii habari ni
moja ya picha kali sana sawa na za kihindi tu, na ipo kama ifuatavyo;
Kwanza crew nzima inaonesha ni ya Tangayika ambapo

SCRIPT WRITTER: Atakuwa ni yule kijana anayeropoka hovyo
EDITOR: Hii kazi alishika mzee wa mabomu licha ya kuwa atakuwa
ameshiriki kazi nyingine nyingi ili kuwezesha filamu hii kali.
GRAPHICs DESIGNER: Hii nafasi mzee wa tembo atakuwa amemudu vizuri
sana. Nafasi kubwa kabisa za mwisho ni kama hivi;
DIRECTOR: Hii kazi imefanywa vizuri sana na CCM.
PRODUCER: LUMUMBA PRODUCTION 2013.
Haki zimehifadhiwa ila zimevuja.

Lengo la picha ni kuchonganisha na kuvuruga muungano wa wapinzani kwa
sababu unaonekana kuwa HATARI zaidi kwa CCM juu ya katiba mpya.

mkuu, tusiweke dhana ambayo haipo. taarifa hii si ya kupuuzwa au kuiletea mzaha
 
Yaani haoni wazi kuwa mswada uliopitishwa hauna maslahi kwa Wazanzbari, au anaona kuwa kuunga mkono mtizamo wa CHADEMA kutaleta ufumbuzi kinyume na agenda yake ya kuuvunja Muungano, au haoni kuwa CUF huku bara imebanwa mno na haifurukuti kwa sababu ya kukubaliana kutoipinga CCM kwa nguvu kwa sababu za muafaka? Ukweli ni kuwa CUF wasipobadilika na kurudi kuwa chama cha upinzani badala ya chama cha muafaka watakuwa na hali ngumu zaidi huko tuendako! Fikra za Maalim hazikisaidii!
 
wacha uongo wewe!!!
Maalim hata hayupo nchini wiki ya pili hii!!!
Nyie maccm vp??

mkuu, kuwa au kutokuwa nchini si sababu. hata dr slaa mara nyingi amekuwa akielezea jambo lolote anapokuwa nje ya nchi na amekuwa akishiriki mijadala mingi humu jf
 
Nimepata kushauri kwamba CUF ishirikiane na CHADEMA kuondoa Chama cha Mafisadi madarakani: Katika mpangilio huo, Lipumba angegombea Ubunge Tabora badala ya kuendelea na taaluma yake ya kugombea u-Rais. Tukishinda angekuwa Spika. Maalim angekuwa Naibu Waziri Mkuu wa JMT.

Kama pendekezo sasa ni CHADEMA na CUF kuungana na kuwa chama kimoja, mambo yatanoga zaidi kwa vile muungano huo utashinda. Hata kama CCM itaendelea kuongoza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, itawezekana kuendelea kushirikiana na Serikali ya Muungano kama ilivyo sasa.
 
Haya ni maneno ya uongo...!Habari haina chanzo..! imejaa longo longo kibao,eti chanzo cha kuaminika bila kukitaja? Kachukue mgawo wako Lumumba, Safari hii imekula kwenu.....!
 
Maalim seif aliwaingiza cuf choo cha kike yeye anaona anazeeka wacha ajipatie ulaji bna
 
Chadema kinafaa kuungana na jamaa yao shetani tu wala siyo chama cha siasa.

nyie makuadi hamna akili vichwani mwenu hizo taarifa ni za kitaa wala sio za maalimu sefu,mlivyo wendawazimu mnadhani sote tuko kiivyo,kama kuna mashetwani hapa tanzania ni maCCM,madharimu,mauwaji na mafedhuri makuadi wa kisiasa mnafikiria kutumia ------ vichwa vimebaki kufugia nywele.
 
kwahiyo ni upi msimamo wa CUF kwenye ishu nzima ya mswada wa katiba mpya!!!?????:deadhorse:
 
Naona Anatoa Mawazo Yake Kama Yeye Ndo CUF Peke Yake Lipumba Kahongwa Pesa Mtatitro Kahongwa?? Hayupo Tayr Kuzunguka Tz Kuishtaki CCM Tena Kwenye Mchakato Ulio Andaliwa Na Chadema Huyu Mzee Ikulu Imemnogea Anaona Kama Cuf Wanataka Kuhalibu Mambo!! Viva Lipumba Viva Mtatiro Viva Mbowe
 
inamaana hana imani hata na prof?
Kuna uzi uliletwa hapa ukisema kuwa CUF ni ya Wazanzibar, nilitaka nibishe lakini nguvu ya makamu kushinda ya mwenyekiti mwenyewe ni uthibitisho usio rasmi. Hawa nia aina ya viongozi ambao bila kufanya wao kitu basi ni bora kisifanyike kabisa kuliko kufanywa na mwingine.

 
shetan wa demkrasia. inamaana anasapoti waliyoyafanya ccn bungeni kuhusu katiba?
 
Hii shuhuli sasa inanoga,taratibu naanza kuiona CUF ya bara na CUF ya Zanzibar,kuna msemo kwenye siasa kuwa hakuna adui wala rafiki wa kudumu,Maalim Seif anasindikizwa na vingora wakati Lipumba tunasubiri wote taa za barabarani ziruhusu,kijana mwenzetu Mtatiro keshaona hakuna mwanga mbele ndani ya CUF bara,nini kitafuata wanajua wenyewe CUF.
CDM wamekumbuka kuwa hakuna adui wa kudumu na sasa pengine wamejirudi na kuamua kutaka ushirika ili kumtoa kirusi CCM........CUF bara msirudi nyuma simamieni kucha hivyo hivyo mpk kieleweke.
 
Wadau,

Taarifa za kuaminika nilizopata kutoka chanzo cha kuaminika huko Zanzibar zinasema kuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amepinga kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama hicho kuingia makubaliano na CHADEMA ili kupinga muswada wa katiba mpya. Maalim Seif amenukuliwa akisema mbele ya baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa uamuzi huo si wa kichama bali ni msimamo wa baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao wamepewa fedha na CHADEMA ili wawe na msimamo wa aina moja. Maalim Seif anasema kuwa wanaoratibu mpango huo ni Naibu Katibu Mkuu, Julius Mtatiro kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge wa chama hicho kutoka Zanzibar. Taarifa zinasema kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Ibrahim Lipumba inaelekea kuwa ameingia kucheza ngoma ambayo haijui na matokeo yake anaonekana kupoteza mwelekeo na kukosa msimamo. Hoja zilizoainishwa na Maalim Seif za kupinga makubaliano hayo ni hizi zifuatazo;

  1. Hakuna kikao chochote cha chombo chochote cha kiutendaji na kimaamuzi cha CUF kilichoketi iwe Zanzibar au Tanzania Bara kujadili jambo hilo na kuweka msimamo wa chama.
  2. Maoni yaliyotolewa na Kambi Rasmi ya Upinzani juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba hayakuwa maoni ya vyama vyote vya upinzani bali yalikuwa ni maoni ya CHADEMA pekee waliyoandaa kwa muktadha wa kujipatia umaarufu Zanzibar
  3. CUF ni moja ya vyama vinavyounda serikali ya umoja wa Kitaifa Zanzibar. Kutokana na ukweli kuwa Serikali hiyo imeshirikishwa na yeye (Maalim Seif) ameshiriki katika kuboresha Muswada huo anaamini kuwa chama hicho kupitia Serikali ya Umoja wa kitaifa ambayo imepewa baraka na Wazanzibari wote kimeshiriki kutoa maoni yake. Hivyo madai kuwa Wazanzibari hawajashirikishwa si ya kweli na ni upotoshwaji mkubwa
  4. Misimamo ya viongozi wa CHADEMA dhidi ya Zanzibar mara zote imekuwa hasi na kwa hali hiyo hali iliyojitokeza ya viongozi wa chama hicho kujipendekeza kwa Wazanzibari imetafsiriwa kuwa ni ulaghai wa kisiasa.
  5. Zanzibar ina viongozi ambao ndio waliopewa dhamana ya kuwasemea Wazanzibari na si mtu mwingine ambaye misimamo yake dhidi ya Wazanzibari inajulikana
  6. Kwa muda mrefu, CHADEMA wamekuwa wakitoa kauli za kuudhi dhidi ya CUF na viongozi wake hasa wale wanaotoka Zanzibar kama vile CUF ni CCM B, CUF ni chama cha Kiliberali ambacho kinasupport ndoa ya jinsia moja na CUF imeolewa na CCM. Kwa kauli hizo, hakika muungano unaosema hasa na CHADEMA si wa kweli bali ni wa maslahi ya upande mmoja.
  7. CHADEMA wanataka kuitumia CUF kama daraja ili kujipatia wafuasi Zanzibar. hii ni kutokana na CHADEMA kuendelea kupoteza mvuto visiwani humo hasa kutokana na viongozi wakuu wa chama hicho kuwa na chuki binafsi dhidi ya Zanzibar. Aibu aliyopata Katibu Mkuu wa CHADEMA alipofanya ziara visiwani humo imechochea viongozi wa chama hicho kuona haja ya kuungana na CUF

Kutokana na hali hiyo, Maalim Seif ametoa msimamo ufuatao ambao anategemea kuuwasilisha kwenye vikao halali vya kiutendaji vya CUF na ambao amesema unaungwa mkono na viongozi wengi wa chama hicho;

  1. Yeye kama katibu Mkuu na mtu anayekubalika na kutumainiwa na Wazanzibari wengi hatashiriki kikao chochote na CHADEMA kujadili jinsi ya kukwamisha mchakato wa Katiba
  2. Yeye kama Katibu Mkuu hatashiriki ziara iliyotangazwa na CHADEMA ya kuzunguka nchi nzima kwa kile kinachodaiwa kuishtaki serikali ya ccm kwa wananchi
  3. CHADEMA wameonywa kutojipendekeza kwa CUF na wamekumbushwa msimamo wao kuwa CHADEMA KITASIMAMA KWA MIGUU YAKE YOYOTE NA HAKIHITAJI MSHIRIKA YEYOTE KATIKA JAMBO LOLOTE

Nawasilisha

Tanzania hakuna upinzani bali kuna waganga njaa tuuuuuu huyo maalim nani sijui keshalewa viyoyozi na vijikuku vya ikulu sasa magamba wametishia kumfurusha. Hivi maoni ya wananchi yanatolewa na serikali na sio wabunge wao au wao wenyewe? njaa bhana
 
Chadema ndo chama kinachokua kwa kasi kubwa TZ na sikutegemea kumsikia seif akikubali hii kazi ya ukombozi inayotaka kufanywa na chadema+cuf ili hali yeye ni mpenda madaraka na anahofia kupoteza ajira yake.
NAPITA TU
 
Back
Top Bottom