Maalim Seif Hamad apinga CUF kuungana na CHADEMA

Maalim Seif Hamad apinga CUF kuungana na CHADEMA

Kupanga kufunga ndoa kinyume na utaratibu ndiyo hivyotena kizungumkuti kimeanza.
 
kwani nani kawaambia CHADEMA iliwaomba CUF kuungana, hoja zenye ukweli ndizo zilizowafanya wabunge wa zanzibar wenye nia nzuri na nchi yao kuunga mkono msimamo wa CDM>>> na mlitegemea nini kutoka kwa Maalum Seif wakati yeye ni makamu wa Rais na serikali ndiyo iliyowasilisha msuada huo?

wakati machadema mnafunga ndoa ya mkeka na cuf hamkujua kuwa cuf ipo madarakani? Na maalim seif ni makam wa rais?
 
Acha mipasho na taarabu zako hiz, we subiria majibu ya hiz harakati za CDM na CUF ndo mtatafuta pa kutokea.
Milango ya kutokea haitabadilika chadema na cuf ta wakafunga ndoa kanisani bado watapotezana tu na ccm kuendelea kuwatumikia watanzania.
 
kuna thread imefutwa haraka niliweka challenge ya CUF ktk hili na umuhimu wa CDM kwa CUF...Nilijua maalimu hatakubali, ila desperately bila CDM kusema neno roho ya CUF haitopona.

CUF wanahitaji heshima, na heshima wataipata kwa kuipa nafasi nafsi CDM..ila itakuja with cost..kwa kukubali faida zote CDM watakazozipata....na CUF hawawezi pata vyote..yaani heshima bila CDM, na wakiikosa heshima ni wazi wataingia shimoni na CCM.

CUF wanahitaji kufuata Njia za CDM kwa kuwa karibuna na CDM ili wapate heshima ya kusimamia misingi ya chama,kuanzia mahakamani hadi uraiani.

Maalimu anayyo shida kukubalina na hiyo hali...nilijua atakumbushia udugu na CCM kuliko aone CDM wakipaa...anajua watakapoingia pemba na CDM km rafiki basi muda si mrefu watakuwa wkaigombania no mbili.
 
Tunaweza kuwa tunajadili umbeya maana habari yenyewe inatajwa kuwa 'habari za kuaminika kutoka vyanzo vinavyoaminika', vyanzo hivyo ni vipi, haviwezi kutajwa ili tujue kama ni vya kuaminika au hapana? Upuuzi mtupu.

Mh katika hilo, nadhani Julius Mtatiro ndiye mwenye siri nzito na mtu anayestahili kujibu swali hilo
 
Huyu nae hamnazo kabisa.,yeye anaenjoy chopa ya serikali anabebea mkaa analeta siasa uchwara hapa....yeye ashapozwa na uongozi atulie tu.hana nguvu tena kwenye mordern politics,pact walizo sigh na sisi zinamfunga kufunya siasa za upinzani.
 
CDM walitaka mteremko sasa chama makini kimeshtukia janja ya wanakaskazini!hongera katibu mkuu
 
Wadau,

Taarifa za kuaminika nilizopata kutoka chanzo cha kuaminika huko
Zanzibar zinasema kuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad
amepinga kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama hicho kuingia
makubaliano na CHADEMA ili kupinga muswada wa katiba mpya. Maalim Seif
amenukuliwa akisema mbele ya baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar kuwa uamuzi huo si wa kichama bali ni msimamo wa baadhi ya
viongozi wa chama hicho ambao wamepewa fedha na CHADEMA ili wawe na
msimamo wa aina moja. Maalim Seif anasema kuwa wanaoratibu mpango huo ni
Naibu Katibu Mkuu, Julius Mtatiro kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge
wa chama hicho kutoka Zanzibar. Taarifa zinasema kuwa Mwenyekiti wa
chama hicho, Ibrahim Lipumba inaelekea kuwa ameingia kucheza ngoma
ambayo haijui na matokeo yake anaonekana kupoteza mwelekeo na kukosa
msimamo. Hoja zilizoainishwa na Maalim Seif za kupinga makubaliano hayo
ni hizi zifuatazo;

  1. Hakuna kikao chochote cha chombo chochote cha
    kiutendaji na kimaamuzi cha CUF kilichoketi iwe Zanzibar au Tanzania
    Bara kujadili jambo hilo na kuweka msimamo wa chama.
  2. Maoni yaliyotolewa na Kambi Rasmi ya Upinzani
    juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba hayakuwa maoni ya
    vyama vyote vya upinzani bali yalikuwa ni maoni ya CHADEMA pekee
    waliyoandaa kwa muktadha wa kujipatia umaarufu Zanzibar
  3. CUF ni moja ya vyama vinavyounda serikali ya
    umoja wa Kitaifa Zanzibar. Kutokana na ukweli kuwa Serikali hiyo
    imeshirikishwa na yeye (Maalim Seif) ameshiriki katika kuboresha Muswada
    huo anaamini kuwa chama hicho kupitia Serikali ya Umoja wa kitaifa
    ambayo imepewa baraka na Wazanzibari wote kimeshiriki kutoa maoni yake.
    Hivyo madai kuwa Wazanzibari hawajashirikishwa si ya kweli na ni
    upotoshwaji mkubwa
  4. Misimamo ya viongozi wa CHADEMA dhidi ya
    Zanzibar mara zote imekuwa hasi na kwa hali hiyo hali iliyojitokeza ya
    viongozi wa chama hicho kujipendekeza kwa Wazanzibari imetafsiriwa kuwa
    ni ulaghai wa kisiasa.
  5. Zanzibar ina viongozi ambao ndio waliopewa
    dhamana ya kuwasemea Wazanzibari na si mtu mwingine ambaye misimamo yake
    dhidi ya Wazanzibari inajulikana
  6. Kwa muda mrefu, CHADEMA wamekuwa wakitoa kauli
    za kuudhi dhidi ya CUF na viongozi wake hasa wale wanaotoka Zanzibar
    kama vile CUF ni CCM B, CUF ni chama cha Kiliberali ambacho kinasupport
    ndoa ya jinsia moja na CUF imeolewa na CCM. Kwa kauli hizo, hakika
    muungano unaosema hasa na CHADEMA si wa kweli bali ni wa maslahi ya
    upande mmoja.
  7. CHADEMA wanataka kuitumia CUF kama daraja ili
    kujipatia wafuasi Zanzibar. hii ni kutokana na CHADEMA kuendelea
    kupoteza mvuto visiwani humo hasa kutokana na viongozi wakuu wa chama
    hicho kuwa na chuki binafsi dhidi ya Zanzibar. Aibu aliyopata Katibu
    Mkuu wa CHADEMA alipofanya ziara visiwani humo imechochea viongozi wa
    chama hicho kuona haja ya kuungana na CUF

Kutokana na hali hiyo, Maalim Seif ametoa msimamo ufuatao ambao
anategemea kuuwasilisha kwenye vikao halali vya kiutendaji vya CUF na
ambao amesema unaungwa mkono na viongozi wengi wa chama
hicho;

  1. Yeye kama katibu Mkuu na mtu anayekubalika na
    kutumainiwa na Wazanzibari wengi hatashiriki kikao chochote na CHADEMA
    kujadili jinsi ya kukwamisha mchakato wa Katiba
  2. Yeye kama Katibu Mkuu hatashiriki ziara
    iliyotangazwa na CHADEMA ya kuzunguka nchi nzima kwa kile kinachodaiwa
    kuishtaki serikali ya ccm kwa wananchi
  3. CHADEMA wameonywa kutojipendekeza kwa CUF na
    wamekumbushwa msimamo wao kuwa CHADEMA KITASIMAMA KWA MIGUU YAKE YOYOTE
    NA HAKIHITAJI MSHIRIKA YEYOTE KATIKA JAMBO LOLOTE

Nawasilisha
Wakati anawaeleza hayo wewe ulikuwa wapi hadi ukapata fursa ya kupangilia vizuri mawazo yake?
 
hatutachangia hii thread maana aliyeileta, anayechangia ni mtu mmoja kwa id kibao ,anachokifanya ni kuhama hama komputa na kufikiria sasa atukane tusi lipi...hakika hakuna wenye akili timamu wataleta mwawazo mbadala ila watasoma na kuuliza maswali na mengineyo...kumbuka sijachangia thread hii,,,na wanajf wenye akili timilifu hatutachangia maneno yenu ya kwenye kanga bali tutauliza maswali mengi tuuu.
upo sahihi kabisa.....halafu anaonekana katumwa
 
Njaa na Uchu wa madaraka ni vitu vibaya sana. CUF is Maalim's way, any other way is wrong way. Siku zake za kulia silver spoon zinahesabika
 
Sasa ngoma imeingia patamu. Sijui CHADEMA watakuja na lipi la kutueleza

Ngoma bado mbichi huyo ndiyo maalim nadhani wazanzibar wamemsuta kuungana na makfir chadema ingekuwa ni kuitukana zanzibar.

Ndoa sasa itakuwa ndoano sikujua kama chadema ndiyo alikuwa mke na cuf ndiyo mume au vinginevyo.

Mkuu, sawa kabisa. Si hilo tu bali ametudhihirishia kuwa CHADEMA ni waongo na ni walaghai

Chadema kinafaa kuungana na jamaa yao shetani tu wala siyo chama cha siasa.

Mh katika hilo, nadhani Julius Mtatiro ndiye mwenye siri nzito na mtu anayestahili kujibu swali hilo

Ndoa ya mkeka imebuma

Mkuu, hakika njia ya mnafiki ni fupi. CHADEMA wamesahau kuwa walijigamba kuwa wao watasimama kwa miguu yao tu na si kutegemea mbeleko ya vyama vingine

Maalim seif mjanja, inaitwa ngastukaa, hakuna kumtumia mwanaume mwenzio km ile mipira

Mkuu, sidhani kama kulikuwa na ndoa hapo ila nilichobaini ni kuwa CHADEMA (mwanamke) alikuwa anamtamani CUF (mwanaume) ila alikuwa anashindwa kumtongoza kwa kuogopa kuchomolewa na kuitwa malaya. uvumilivu ulipomshinda mwanamke akajitosa kumtongoza mwanaume na sasa amechomolewa

Ila kiukweli nimependa sana msimamo wa huyu mtu. ningeshangaa kama angekubali kuungana na CHADEMA maana kwa kufanya hivyo kungehatarisha serikali ya umoja wa kitaifa ambayo kwa sasa imekuwa imara sana

I support you Mkuu. Ila nadhani uroho wa madaraka ni kasumba ya wanasiasa wengi wa kiafrika. Mwone hata mwenyekiti wake alivyong'ang'ania nafasi ya mwenyekiti

Maalim Seif sasa ameiva kisiasa.

Haani ukitaka kuona upuuzi wa vijana wa Lumumba ni kama huu yaani wanachangia kwa fujo huku hawajui hata wanachokichangia hii ni sawa na WANAJITEKENYA NA KUCHEKA WENYEWE
 
Sijaona afya ya huu muungano suala linakuja kwenye kugombea vyeo
 
Jamani hii habari ni moja ya picha kali sana sawa na za kihindi tu, na ipo kama ifuatavyo;
Kwanza crew nzima inaonesha ni ya Tangayika ambapo

SCRIPT WRITTER: Atakuwa ni yule kijana anayeropoka hovyo
EDITOR: Hii kazi alishika mzee wa mabomu licha ya kuwa atakuwa ameshiriki kazi nyingine nyingi ili kuwezesha filamu hii kali.
GRAPHICs DESIGNER: Hii nafasi mzee wa tembo atakuwa amemudu vizuri sana. Nafasi kubwa kabisa za mwisho ni kama hivi;
DIRECTOR: Hii kazi imefanywa vizuri sana na CCM.
PRODUCER: LUMUMBA PRODUCTION 2013.
Haki zimehifadhiwa ila zimevuja.

Lengo la picha ni kuchonganisha na kuvuruga muungano wa wapinzani kwa sababu unaonekana kuwa HATARI zaidi kwa CCM juu ya katiba mpya.
 
wadau,

taarifa za kuaminika nilizopata kutoka chanzo cha kuaminika huko zanzibar zinasema kuwa katibu mkuu wa cuf, maalim seif sharif hamad amepinga kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama hicho kuingia makubaliano na chadema ili kupinga muswada wa katiba mpya. Maalim seif amenukuliwa akisema mbele ya baadhi ya viongozi wa serikali ya mapinduzi zanzibar kuwa uamuzi huo si wa kichama bali ni msimamo wa baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao wamepewa fedha na chadema ili wawe na msimamo wa aina moja. Maalim seif anasema kuwa wanaoratibu mpango huo ni naibu katibu mkuu, julius mtatiro kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge wa chama hicho kutoka zanzibar. Taarifa zinasema kuwa mwenyekiti wa chama hicho, ibrahim lipumba inaelekea kuwa ameingia kucheza ngoma ambayo haijui na matokeo yake anaonekana kupoteza mwelekeo na kukosa msimamo. Hoja zilizoainishwa na maalim seif za kupinga makubaliano hayo ni hizi zifuatazo;

  1. hakuna kikao chochote cha chombo chochote cha kiutendaji na kimaamuzi cha cuf kilichoketi iwe zanzibar au tanzania bara kujadili jambo hilo na kuweka msimamo wa chama.
  2. maoni yaliyotolewa na kambi rasmi ya upinzani juu ya muswada wa sheria ya marekebisho ya katiba hayakuwa maoni ya vyama vyote vya upinzani bali yalikuwa ni maoni ya chadema pekee waliyoandaa kwa muktadha wa kujipatia umaarufu zanzibar
  3. cuf ni moja ya vyama vinavyounda serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar. Kutokana na ukweli kuwa serikali hiyo imeshirikishwa na yeye (maalim seif) ameshiriki katika kuboresha muswada huo anaamini kuwa chama hicho kupitia serikali ya umoja wa kitaifa ambayo imepewa baraka na wazanzibari wote kimeshiriki kutoa maoni yake. Hivyo madai kuwa wazanzibari hawajashirikishwa si ya kweli na ni upotoshwaji mkubwa
  4. misimamo ya viongozi wa chadema dhidi ya zanzibar mara zote imekuwa hasi na kwa hali hiyo hali iliyojitokeza ya viongozi wa chama hicho kujipendekeza kwa wazanzibari imetafsiriwa kuwa ni ulaghai wa kisiasa.
  5. zanzibar ina viongozi ambao ndio waliopewa dhamana ya kuwasemea wazanzibari na si mtu mwingine ambaye misimamo yake dhidi ya wazanzibari inajulikana
  6. kwa muda mrefu, chadema wamekuwa wakitoa kauli za kuudhi dhidi ya cuf na viongozi wake hasa wale wanaotoka zanzibar kama vile cuf ni ccm b, cuf ni chama cha kiliberali ambacho kinasupport ndoa ya jinsia moja na cuf imeolewa na ccm. Kwa kauli hizo, hakika muungano unaosema hasa na chadema si wa kweli bali ni wa maslahi ya upande mmoja.
  7. chadema wanataka kuitumia cuf kama daraja ili kujipatia wafuasi zanzibar. Hii ni kutokana na chadema kuendelea kupoteza mvuto visiwani humo hasa kutokana na viongozi wakuu wa chama hicho kuwa na chuki binafsi dhidi ya zanzibar. Aibu aliyopata katibu mkuu wa chadema alipofanya ziara visiwani humo imechochea viongozi wa chama hicho kuona haja ya kuungana na cuf

kutokana na hali hiyo, maalim seif ametoa msimamo ufuatao ambao anategemea kuuwasilisha kwenye vikao halali vya kiutendaji vya cuf na ambao amesema unaungwa mkono na viongozi wengi wa chama hicho;

  1. yeye kama katibu mkuu na mtu anayekubalika na kutumainiwa na wazanzibari wengi hatashiriki kikao chochote na chadema kujadili jinsi ya kukwamisha mchakato wa katiba
  2. yeye kama katibu mkuu hatashiriki ziara iliyotangazwa na chadema ya kuzunguka nchi nzima kwa kile kinachodaiwa kuishtaki serikali ya ccm kwa wananchi
  3. chadema wameonywa kutojipendekeza kwa cuf na wamekumbushwa msimamo wao kuwa chadema kitasimama kwa miguu yake yoyote na hakihitaji mshirika yeyote katika jambo lolote

nawasilisha

wacha uongo wewe!!!
Maalim hata hayupo nchini wiki ya pili hii!!!
Nyie maccm vp??
 
Tunaweza kuwa tunajadili
umbeya maana habari yenyewe inatajwa kuwa 'habari za kuaminika kutoka
vyanzo vinavyoaminika', vyanzo hivyo ni vipi, haviwezi kutajwa ili tujue
kama ni vya kuaminika au hapana? Upuuzi mtupu.

mkuu, hata dr slaa mara nyingi anasema kuwa ana taarifa za kuaminika kutoka vyanzo vya kuaminika na tunamwamini. hapa suala si chanzo cha taarifa bali taarifa yenyewe
 
Wakati anawaeleza hayo wewe ulikuwa wapi hadi ukapata fursa ya kupangilia vizuri mawazo yake?

mkuu, kwa jinsi huyu Lusewa alivyoiweka hii habari, sina mashaka nayo kabisaaaaa. halafu huyu atakuwa mtu wa karibu na Maalim Seif au amepata hii taarifa kutoka kwa mtu ambaye yupo karibu naye
 
Back
Top Bottom