Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,964
- 6,908
Tatizo unarudia makosa Yale Yale ya kuichukulia Zanzibar kama koloni LA Tanganyika.
Ungejiridhisha hizo katiba za ACT na Hiyo ya licheck lLipumba. Utagundua composition zao zimezingatia nafasi ya Zanzibar kama partner wa muungano.
Unachekesha kusema kwa kuwa ACT imeamua kuiunga SUK Zanzibar na kusikiliza upande was wanachama Zanzibar pekee imewakosea watu was kibondo na mtwara lkn unasahau isingezingatia hivyo na kuamua jumla jumla tu kumbe ACT ingekuwa imewakosea wazanzibari vile vile.
Nataka ukubali kuwa hip sio hoja na bila kuwa na mtazamo huo in sawa na ukoloni ambao Mara zote ndugu zetu was Zanzibar wanapigia kelele.
Maalim Seif kaeleza vizuri. Si kila kitu kinasusiwa. By the way unataka kumfundisha mtaalamu wa kususia namna ya kususia wakati yeye mwenyewe ni mzoefu.
Hakuna hoja yoyote hapo yenye uhalali zaidi ya hasira kuficha chuki dhidi ya wazanzibari.
Tubadilike.
Ninavyojua mimi ni kuwa mpaka sasa hivi Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na chama cha ACT WAZALENDO ni chama cha kitanzania sio cha kizanzibari. Kama chama cha kitanzania kina wajibu wa kusikiliza maoni ya wanachama wa pande zote mbili za Muungano kuhusu hatua kubwa kama hii. Labda mtuambie kuwa kuna ACT Wazalendo ( Zanzibar) na ACT Wazalendo (Bara).
Kama Zanzibar wanaona kuwa watu wa Bara kuulizia masuala ya Zanzibar ni ukoloni basi waseme wazi kuwa hawautaki Muungano ili kila mmoja wetu aweze kujiamulia anavyotaka bila kujali mwenzake ataathirika vipi na uamuzi wake. Ilhali bado wako kwenye Muungano inawapasa kuwaheshimu wenzao ambao waliwakaribisha kwenye chama chao. Maoni ya mwanachama wa ACT Wazalendo Kilwa yanatakiwa yapewe uzito ule ule kama aoni ya mwanachama wa ACT wazalendo anayeishi Pemba.
Hivi huyo mwalimu wa kususia, amesusia mara ngapi kiasi cha kumfanya yeye mzoefu? Kwa bahati mbaya, kwetu sisi machogo, Maalim ni binadamu kama wengine. Anapokosea hatuchelei kumwambia. Yeye sio Mungu wetu.
Kwa mtazamo wenu huo haitachukua muda mtaigeuza ACT Wazalendo kuwa CUF nyingine. Hamjiulizi kwa nini wakina Zitto, Ado na wengine hawako mstali wa mbele kutetea uamuzi wa chama chao? Ado baada ya kusomea jamii maamuzi ya Kamati Kuu kapotea. Zitto kajikita katika masuala ya Ethiopia na alitokeza tu kama mgeni mualikwa. Bwana mdogo Nondo kajitahidi sana kutetea msimamo wenu Twitter lakini inaelekea na yeye kanyanyua mikono. Huu uamuzi ni mzuri sana kwa ACT Wazalendo (Zanzibar) lakini kwa Bara bado ina ukakasi. Na viongozi wenu machogo wanajua hilo.
Amandla...