Maalim Seif akana kuitwa msaliti kwa kukubali SUK asema sio kila jambo unasusia!

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,911
51,889
Msikilize mwenyewe

===
Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema uamuzi wa ACT-Wazalendo na yeye kuridhia kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitafa Zanzibar (SUK) usitafsiriwe kuwa ni usaliti kwa wananchi.

Unguja. Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema uamuzi wa ACT-Wazalendo na yeye kuridhia kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitafa Zanzibar (SUK) usitafsiriwe kuwa ni usaliti kwa wananchi.

“Eti wapo wanaosema mimi ni msaliti kwa kukubali kuingia katika Serikali. Kilichotokea si uamuzi yangu, bali ni uamuzi ya wananchi pamoja na kamati kuu. Mimi kama kiongozi mkuu wa chama kazi yangu ni kusimamia na nitaendelea kufanya hivyo kwa maslahi ya Wazanzibar,” alisema Maalim,

Desemba 8, 2020 Maalim Seif alikula kiapo cha kushika wadhifa huo mbele ya Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi baada ya kikao cha kamati kuu ya chama hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam kuja na uamuzi wa kuingia katika Serikali hiyo.

Hatua hiyo iliwagawa baadhi ya wapenzi, wafuasi na wanachama wa chama hicho, huku kwa nyakati tofauti Maalim Seif na Dk Mwinyi wakieleza mikakati ya Zanzibar mpya, wakisisitiza maslahi mapana ya nchi hiyo.

Awali, chama hicho kilipinga mwenendo na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, kikidai kuwepo kwa matukio ya wanachama wake kuuawa na kuteswa.

Jana, Maalim Seif ambaye ni mwenyekiti wa ACT-Wazalendo alizungumza katika mkutano uliofanyika makao makuu ya chama hicho Vuga Mjini Unguja na kukanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kwamba yeye ni msaliti wa Wazanzibar kwa kukubali kuingia katika Serikali hiyo.

“Nani nimemsaliti mimi?” alihoji Maalim Seif aliyesema kuwa suala hilo waliwahoji wananchi walipofanya ziara na wapo waliotaka wasiingie kwenye SUK, japo waliokubali walikuwa wengi.

Kuhusu watu aliodai kuwa wanajifanya kuwa wanachama wa ACT Wazalendo wakidai kukihama chama hicho kutokana na hatua hiyo, aliwataka waondoke. “Anayetaka kwenda CCM na aende, anayetaka kwenda Chadema na aende, anayetaka kwenda NCCR-Mageuzi na aende, wanaoumia na chama chao wapo na wapo tayari kukulinda ili kiendelee,” alisema.

Maalim Seif alisema kwa sasa hakuna mbadala,bali ni kukubali kufanya kazi na Dk Husein Mwinyi katika kuiletea maendeleo Zanzibar na kuondosha chuki baina ya wananchi wake.
 
Siasa za Zenji sizielewi, unaibiwa na unategemea kuibiwa na hawaachi kukuibia na wanahaidi kukuibia, we poa tu, na unakubali cheo cha ushauri, na bado mzee unang'ng'ania ukawakilishe!
 
Maalim siku zote focus yake ni Zanzibar tu na anavitumia vyama vya siasa vya bara kama vyombo vya kufikia lengo lake. Alikichukua chama cha wakina Aleck Che Mponda na kukigeuza kuwa chama ambacho priority yake kubwa ni masuala ya Pemba na Unguja. Ameingia sasa ACT-WAZALENDO na anarudia mchezo ule ule. Nasema hivi kwa sababu:

1. Anaposema wanachama wa ACT-WAZALENDO waliulizwa kuhusu hatua ya kuingia kwenye GNU sidhani kama anamaanisha wanachama walioko Kibondo au Newala. Kwake yeye mradi wanachama walioko Pemba na Unguja wameulizwa mchezo umekwisha.
2. ACT Wazalendo ni chama cha kitaifa na hivyo kabla ya uamuzi wowote kuchukuliwa walipaswa kuangalia athari au faida yake kwa Chama kwa ujumla na sio kwa upande mmoja wa Muungano. Mpaka sasa hivi tunachosikia ni faida tu kwa wanachama walioko Zanzibar lakini hatusikii lolote kuhusu faida ambazo mwanachama wa Kibondo atapata kutokana na hatua hii.

3. Lugha ya kuwa Zanzibar sio Tanzania Bara ni ya kuwakataza hata wanachama wenzake wasio wazanzibari kushiriki katika mjadala unaohusu uamuzi wao wa kujiunga katika SUK.

4. Kwa ACT-WAZALENDO ( Bara) uamuzi huu unaweza kuwaathiri sana maana wamejiweka wazi kwa tuhuma za kuwa wao sio sehemu ya upinzani makini bali ni sehemu ya utawala uliopo. Hali hii inaweza kukubalika Zanzibar lakini itawaathiri kwa wanachama wao waliokipigania chama chao kwenye mikoa kama Lindi na Mtwara.

5. Kwa matamshi yake tayari anajihesabu yeye ni sehemu ya utawala wa Zanzibar. Ameanza mpaka kutumia lugha za vitisho dhidi ya wale ambao hawakubaliani na uamuzi wake. Kwa kufanya hivi anaonyesha yeye by nature ni authoritarian na hataki watu watofautiane nae. Hii inasikitisha kwa sababu inaonyesha kuwa si muumini wa Demokrasia na kuna uwezekano mkubwa kama angekuwa na uwezo angefanya vitendo hivyo hivyo ambavyo alifanyiwa.

Hata hivyo pamoja na kusema hivi, ninawaombea heri ACT-WAZALENDO na viongozi wao katika safari yao ya kutuonyesha kuwa kuna njia mbadala. Mafanikio yao yatakuwa yetu sote. Na wakionyesha kuwa mawazo yangu ni potofu sitasita kurudi tena humu na kuwaomba msamaha.

Amandla.
 
Huyu Sefu msaliti alianza kuwasalito Wazenji wakati hayati Abood Jumbe alipotaka kuwakomboa toka kwa Kamba
 
Amandla...
Tatizo unarudia makosa Yale Yale ya kuichukulia Zanzibar kama koloni LA Tanganyika.

Ungejiridhisha hizo katiba za ACT na Hiyo ya licheck lLipumba. Utagundua composition zao zimezingatia nafasi ya Zanzibar kama partner wa muungano.

Unachekesha kusema kwa kuwa ACT imeamua kuiunga SUK Zanzibar na kusikiliza upande was wanachama Zanzibar pekee imewakosea watu was kibondo na mtwara lkn unasahau isingezingatia hivyo na kuamua jumla jumla tu kumbe ACT ingekuwa imewakosea wazanzibari vile vile.
Nataka ukubali kuwa hip sio hoja na bila kuwa na mtazamo huo in sawa na ukoloni ambao Mara zote ndugu zetu was Zanzibar wanapigia kelele.

Maalim Seif kaeleza vizuri. Si kila kitu kinasusiwa. By the way unataka kumfundisha mtaalamu wa kususia namna ya kususia wakati yeye mwenyewe ni mzoefu.

Hakuna hoja yoyote hapo yenye uhalali zaidi ya hasira kuficha chuki dhidi ya wazanzibari.

Tubadilike.
 
Mimi naona kajiumbua mwenyewe,
Uwezo wetu wa kuangalia Mambo kwa kuzingatia precedence ni mdogo sana.
Siasa wanazofanya leo CHADEMA, Maalim Seif amezifanya toka 1995, amewahi kuzuia Wabunge na wawakilishi wasishiriki, tena wakiwa na zaidi ya 45% ya sio nyie mna Mbunge mmoja tu Kati ya 264
Amewahi Kususia uchaguzi wa Jecha 2015. Amewahi kuandamanisha watu wakafa 30 na zaidi ya elfu wakaenda ukimbizini kambi ya Kakuma Kaskazini ya Kenya.
Wamewahi kupiga kura za Maruhani..
Amekuwa akizunguka Dunia nzima kuomba misaada na kutaka Zanzibar itengwe kwa miaka 25 bila mafanikio..
Leo hii eti Chadema ndio wanaanza kuwaona wahisani na mabeberu ndio kimbilio!!!
Maalim kafanya haya kwa miaka 35 bila mafanikio leo hii Chadema ndio wanaanza upya tena bila hata ramani..
Poleni sana,, angalieni Historia bhana
 
Maalim alipotoka C.U.F aliamia A.C.T,ilhali wakati wa mvutano wake na Lipumba Chadema walikua bega kwa bega na Maalim.
Kama ufipa wangekuwa na maono ya mbali wangejua mapema mchele na pumba ni zipi kabla ya kumsaport uchaguzi uliopita.
 
Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom