Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,232
- 6,479
Halo JF.
Waswahili walisema tembea uone. Katika tembea na pita zangu mkoani Singida hususan wilaya Iramba, natua KIOMBOI mjini yalipo makao makuu ya wilaya.
Nakutana na maajabu ya shule ya Msingi Kiomboi Bomani. Katika shule hii kuna walimu wengi na walio wengi zaidi ni wanawake. Penye wanawake au wabeijing kuna vitimbi na mikasa ya aina yake.
Walimu hawa kutokana na mashindano ya kuvaa, wamelazimishwa kuvaa sare zinazofanana. Uamuzi huu umefanywa na uongozi wa halmashauri ya wilaya ili kupunguza tambo na majungu miongoni mwa wanawake hawa. Lengo ni ili wote walingane.
Sasa nikaona haya pia ni maajabu, japo pia bado wanashindana katika kubadilisha mashati meupe. Leo mtu atavaa mtumba, kesho la dukani nk. Nikasema kweli binadamu humuwezi.