Maajabu ya bongo movie..

Na kaa na dogo nalazimika tu kuziangalia lakini hamna wanachofanya...bora hata vichekesho
 
ukichunguza vizuri utagundua hao si wakristo. ni waoslam ambao kwa 'bahati mbaya' wamekumbana na hiyo scene na walawa reluctant kuigiza uhalisia. sijaiona ila ni mtazamo wangu
 

hahahaha nilicheka pale yule mama anatoa vipande vya kuku jikoni at moja kwa moja kaviweka kwenye hotpot hata hajaweka somewhere kwenye chombo cha kuchuja kwanza yale mafuta lol
 

Labda ndo lilikuwa kusudio ktk eneo hilo.
 

Low budget na mategemeo ya returns kubwa. Hapo mwendo ni "one take" only, no retakes!
 
Matatizo ya filamu za bongo ni mengi. Mojwapo ni kuwa, scripts zake haziko detailed, na hata wasanii hawajitumi kuinternalize scripts na mbaya zaidi directors hawazingatii kuhakikisha kuwa scripts zinazingatiwa. Kinachoshangaza kingine filamu ina kuwa imeshikilkiwa na mtu mmoja huyohuyo (director, script writer, actor, editor, producer etc). Na mbaya zaidi mradi mzima wa film hauna contuinuity director!!!
 
Ndiyo maana inaitwa "acting", hata kama haufungani na upande unaoigiza unatakiwa uuvae uhusika! Wenzetu wanaigiza madaktari, akiwa anaongea na mgonjwa (muigizaji mwingine) unasahau kama ni "movie". Mtu anaigiza Rais, hiyo "speech" anayotoa (ya kuigiza) hata Rais wa ukweli wa nchi fulanifulani hawezi toa. Kwetu mijitu inaamka tu na "kushoot", kumbe mnatakiwa muipitie "script" nzima na kufanya "consultation" kwa watu wenye taaluma halisi wawaelekeze,,,Oshh kutoa "movie" si rahisi hivi!

ukichunguza vizuri utagundua hao si wakristo. ni waoslam ambao kwa 'bahati mbaya' wamekumbana na hiyo scene na walawa reluctant kuigiza uhalisia. sijaiona ila ni mtazamo wangu
 
Kuna moja nilicheka miaka ya nyuma sana eti steringi alimfytulia mkuu wa maadui risasi na kioo kilikuwa kimewatenga mkuu wa maadui baada ya kufytulia risasi upande mwengine wa kioo akaanguka na kufa na damu kibao kuchuruzika lakin kioo hakikuvunjika kilikuwa vile vile.
 
Nyingine eti jini kuvuka barabara anaangalia kushoto kulia kushoto na kuhakikisha hamna magari anavuka
 
Kuna moja nilicheka miaka ya nyuma sana eti steringi alimfytulia mkuu wa maadui risasi na kioo kilikuwa kimewatenga mkuu wa maadui baada ya kufytulia risasi upande mwengine wa kioo akaanguka na kufa na damu kibao kuchuruzika lakin kioo hakikuvunjika.

Duuuuh bado sanaa bongo yetu afu tunawaza soko la kimataifa kweli
 
Mnakumbuka na zile za action et sterling na jambazi wanavyo pigana bac ni vituko tu akipiga teke mmoja nae nangoja mwenzie arudishe ndo anapiga tena na wlmwenzie anamngoje ivo ivo kweli bongo bwana
 
Nasikia the young billionaire ya kanumba the legindary (rip) waliekti masaa kumi na moja tu kwa anzia asubuhi had jion
 
Mnakumbuka na zile za action et sterling na jambazi wanavyo pigana bac ni vituko tu akipiga teke mmoja nae nangoja mwenzie arudishe ndo anapiga tena na wlmwenzie anamngoje ivo ivo kweli bongo bwana
inspekta seba nini?? Kwa upande flan alijitahid inspekta seba hasa ile last scene fight mkuu wa maadui alikuwa noma kweli nilimkubali alikuwa anaruka sarakas wewe anabwaka hapa na kuibukia upande wa pili anaweza pia kuzama hapa na kuchomoza kwengine. Ilimchukua muda mrefu sana inspekta seba kumzibit kwenye hule mjengo chakavu. Walijitahid sana kibongobongo kwenye hii movie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…