Maajabu Tanzania: Benki ya NMB kufadhili mikutano ya ALAT

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,030
22,704
ALAT ni Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa...Association of Local Authorities of Tanzania

Benki ya NMB imefanikiwa kuchangia kiasi cha Sh. 200 milioni kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya mkutano mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa (ALAT) unaotarajiwa kufanyika kwa siku tatu mkoani Arusha.

Mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 500 kutoka katika halmashauri 184 nchini. Katika miaka saba iliyopita, NMB yadai kutoa zaidi sh. 1.2 bilioni kufanikisha hii mikutano ya ALAT. Je hii ni misaada kwa serikali? Toa maoni yako!

alat-pic.jpg
 
Wanastahili kufanya hivyo kwakuwa ndio wanaowapa wateja.
wengi wao wametengenezewa mazingira ya kuwa katika benki hiyo.
Hivyo wanafanya hivyo kurudisha fadhira.
jaribu kufikiria serikali inawapa wateja zaidi ya 2,000,000 sasa kila mteja akiacha wastani wa shilingi 100,000 wanakuwa na uhakika wa shilingi 200,000,000,000 wakizitumia 80% kukopesha kwa ziada ya 20% wanapata 40,000,000,000.
sasa ukiwapa 200,000,000 shida iko wapi?
 
Ndiyo sababu hizi benki aziendi kwa wananchi wa kawaida...

Serikali ya mitaa ndiyo pesa zilipo, lazima watoe kidogo wanapata kwa wingi.

Waangaike na wewe kwenye kurudisha mkopo stress tupu
 
Serikali Ina hisa ndani ya NMB, Vile vile hata kama wangekuwa hawana hisa,hili li nchi,SI limejaa wezi watupu?kama waziri anaweza kuiba ekari 700!je Raisi ataiba ngapi.
 
Serikali Ina hisa ndani ya NMB,
Vile vile hata kama wangekuwa hawana hisa,hili li nchi,SI limejaa wezi watupu?kama waziri anaweza kuiba ekari 700!je Raisi ataiba ngapi
Nilidhani NMB hutoa gawio kwa serikali kama kawaida. Sasa hizi za kufanikisha mkutano wa hawa viongozi wa serikali imekaakaaje. Je hawa wajumbe serikali haiwalipi pia posho? Je kama NMB hawangetoa hizo hela, huu mkutano ungeshindwa kufanyika?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom