Mr Beast
Senior Member
- Nov 8, 2023
- 187
- 295
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna akiambatana na viongozi wengine wa Benki hiyo wamekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Ujenzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Bi. Zaipuna akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kukutana na viongozi waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuwapa mrejesho wa kiutendaji wa Benki ya NMB kwa mwaka 2023, kuwashukuru na kujadili maeneo ya kuendeleza ushirikiano kwa mustakabali wa Taifa la Tanzania na Watanzania.
Katika kikao hicho, Mhe. Bashungwa ameipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kupitia Wizara yake na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuleta tija zaidi.
Haya yote ni matokeo ya Uongozi uliotukuka wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ndio sababu Benki hii imetambuliwa pia kama Benki bora duniani katika tuzo za "The GlobalFinance Awards"