Wafalme 18
Senior Member
- Sep 17, 2023
- 120
- 126
Benki ya NMB imeshinda tuzo tatu kutoka Taasisi ya Chartered Institute of Customer Management zikiitambua Benki kama kinara katika utoaji huduma bora na wezeshi nchini.
NMB imepata heshima hiyo kupitia tuzo za ‘Mwaka za Umahiri wa Huduma kwa Wateja 2024 (Annual Tanzania Service Excellence Awards 2024) ambapo benki ya Nmb iliibuka mshindi wa jumla wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kwa kampuni zinazofanya kazi nchini.
Mbali na tuzo hiyo, NMB ilitangazwa mshindi wa pili katika Sekta ya Kibenki kwa utoaji huduma bora na mshindi wa pili katika kipengele cha mpango maalum na jumuishi wa huduma kwa wateja.
Tuzo za Umahiri wa Huduma kwa Wateja zilianzishwa mwaka 2010 na zimekuwa zikifanyika katika nchi mbalimbali Barani Afrika lakini zimefanyika jana kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam nchini Tanzania mwaka huu.
Tuzo hizi zimetolewa na Balozi John Ulanga, Mkurugenzi wa Biashara ya Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kupokelewa na Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja NMB - Abella Tarimo, alieambatana na Meneja wa Nmb Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper.