Mapato ya NMB yafikia Tsh. Trilioni 1.4 yavunja rekodi kuwa na wateja Milioni 7.1

Financial Intelligence

Senior Member
Sep 29, 2023
112
245
IMG-20240130-WA0074.jpg
Benki kuu ya biashara ya NMB Tanzania imetangaza matokeo yake ya kiutendaji ya FY2022|23.

Kwamara nyingine Matokeo yakionesha benki hii imevunja rekodi kwa mwaka mwingine tena baada ya kupata mafanikio ya kihistoria.

NMB Tanzania imefanikiwa kuongeza Jumla ya mapato ya Benki na kufikia Shilingi Trilioni 1.4 ikiwa ni ongezeko 18% ukilinganisha na FY2021|22

Jambo bora zaidi ni uwiano wa gharama za uendeshaji na mapato uliboreshwa zaidi hadi kufikia 39% hii ni sawa na kusema wanakusanya zaidi na wanatumia kiduchu.

Wakati huohuo uwiano wa mikopo chechefu umeshuka hadi kufikia 3.2.% Takwimu hizi zote ni chini ya ukomo wa kikanuni wa Benki Kuu wa 55% na 5% mtawalia.

Kutokana na ufanisi huu, Faida kabla ya Kodi imeongezeka kwa 26% hadi TZS 775BL huku Faida baada ya Kodi ikifikia TZS 542BL ikiwa ni ongezeko la 26%. kwa mwaka.

Mizania ya Benki imeendelea kukua na kufikia jumla ya mali ya Shilingi Trilioni 12.2 ikiwa ni ukuaji wa asilimia 19 kwa mwaka.

Tuliendeleza ajenda ya ujumuishaji wa kifedha kwa kufungua akaunti mpya za wateja zaidi ya milioni 1.2, na kufanya jumla ya akaunti za wateja wetu kufikia zaidi ya akaunti milioni 7.1. Hii ni idadi kubwa zaidi ya wateja kwa taasisi moja ya fedha nchini.

NMB iliwekeza zaidi ya TZS 6BL kwenye elimu, afya na mazingira, ikiwa sehemu ya dhamira yetu ya kujitolea kusaidia jamii inayotuzunguka.

Akiwasilisha Taarifa ya Fedha ya Mwaka 2023, Afisa mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ms Ruth Zaipuna amewashukuru wateja wote, wanahisa, wafanyakazi pamoja washirika wote wa Benki,

Zaidi sana ameishikuru Serikali kupitia Benki Kuu na Watanzania wote kwa mchango wao thabiti na imani waliyonayo kwa Benki ya NMB Tanzania.

Mtakumbuka katika mwaka wa 2023 jumla ya faida kwa mabenki yóte ilifikia shilingi Trilioni moja hivyo faida hii ya NMB inakuwa ni sawa na 78% ya faida yote katika robo ya tatu ya Mwaka uliokwisha.

Ningumu kuzungumzia mafanikio haya bila kumzingimzia Rais wa JMT Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkurugenzi mkuu wa NMB PLC Ms Ruth Zaipuna na Bodi nzima ya Benki hiyo chini ya Dkt Edwin Mhede.
 
Maoni yangu kwenye sekta hii ya fedha

1.Tangu Mzee Kimei aondoke pale CRDB hawa NMB wamekosa mshindani kabisa.

2. Huyu dada wa NMB amekuwa mbunifu sana kuliko Wakurugenzi wengine wa mabenki shindani.

3. Huyu dada akikaa katika nafasi hiyo kwa miaka 10 Kuna Benki baadhi zitafungwa hapa nchini.

4. NMB wameikamata Serikali kwelikweli ndio maana wanatoa zaidi tsh 6bilioni ili kujenga urafiki na Serikali.

5. Natamani huyu MD wa NMB ndio angekuwa Gavana wetu huenda tungeshuhudia mabadiliko makubwa kwa sekta ya kibenki hapa Tanzania

Nitaendelea hongera sana SA kwa kuwacharaza wabaya wetu wa Moroco
 
Ukiangalia NMB imejaa vijana local, wenye elimu local wanafanya mambo makubwa. Na wengi hawana elimu kubwa ya masters sijui ujinga gani.

Zamani ilizoeleka kwamba ni wazungu tu ndio wanaweza kufanya hivyo.

Crdb wanajisifu kua na mali nyingi(balance sheet kubwa) lakini ROA (Return on Assets) na AT(Assets Turnover) ratios zao ziko chini ukilinganisha na NMB.

Nmb wanazidi kua wabunifu, crdb inazidi kurudi chini. Soon NMB itakua ndio bank kubwa kuliko zote Tanzania.
 
Aise NMB inakimbia sana, Wateja mil7 sio mchezo, wanastahili pongezi
 
Nadhani NMB atakuja kukakilishwa tu na M-koba tujipe muda

Unless na yeye anguze mariba yake na ajiingize sana kwenye mitandao

Vinginevyo siku zake zinahesbika
 
Ukiangalia NMB imejaa vijana local, wenye elimu local wanafanya mambo makubwa. Na wengi hawana elimu kubwa ya masters sijui ujinga gani.

Zamani ilizoeleka kwamba ni wazungu tu ndio wanaweza kufanya hivyo.

Crdb wanajisifu kua na mali nyingi(balance sheet kubwa) lakini ROA (Return on Assets) na AT(Assets Turnover) ratios zao ziko chini ukilinganisha na NMB.

Nmb wanazidi kua wabunifu, crdb inazidi kurudi chini. Soon NMB itakua ndio bank kubwa kuliko zote Tanzania.
kwan saiv bank kubwa kuliko zote ni ipi?
 
Maoni yangu kwenye sekta hii ya fedha

1.Tangu Mzee Kimei aondoke pale CRDB hawa NMB wamekosa mshindani kabisa.

2. Huyu dada wa NMB amekuwa mbunifu sana kuliko Wakurugenzi wengine wa mabenki shindani.

3. Huyu dada akikaa katika nafasi hiyo kwa miaka 10 Kuna Benki baadhi zitafungwa hapa nchini.

4. NMB wameikamata Serikali kwelikweli ndio maana wanatoa zaidi tsh 6bilioni ili kujenga urafiki na Serikali.

5. Natamani huyu MD wa NMB ndio angekuwa Gavana wetu huenda tungeshuhudia mabadiliko makubwa kwa sekta ya kibenki hapa Tanzania

Nitaendelea hongera sana SA kwa kuwacharaza wabaya wetu wa Moroco
Kuna jamaa nilimwambia Morocco hachomoki akakataa
 
Back
Top Bottom