MAAJABU: Nyoka afa na mmiliki wake Songea

MAAJABU: Nyoka afa na mmiliki wake Songea

Mkazi wa Mtaa wa Mateka, Manispaa ya Songea, Denis Komba (26) amefariki baada ya nyoka wake aliyekuwa amembeba kwenye mfuko wa jaketi kuuawa na wananchi.

Komba alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma (Homso) ambako alilazwa baada ya watu wenye hasira kumuua kwa mawe na fimbo nyoka wake huyo.

Mashuhuda wanaeleza kuwa kabla ya wananchi kumuua nyoka huyo, Komba aliwasihi wasifanye hivyo kwa kuwa wakimuua na yeye angekufa, lakini ombi lake hilo halikusikilizwa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, siku ya tukio Komba alikodi pikipiki ya Kassian Haule (24) ambaye ni mkazi wa Mpitimbi, yenye namba za usajili MC 724 AKB ili apelekwe nyumbani kwake mtaa wa Mateka.

Akisimulia tukio hilo, alisema alipofika katika eneo la Benki ya Posta ya zamani barabara kuu ya Sokoine, dereva wa pikipiki alihisi kuna kitu kinamtekenya na kumgonga gonga kwa nyuma, ndipo alipogeuka nyuma na kumwona abiria wake amebeba nyoka mkubwa huku amesimamisha kichwa.

Haule alisema, baada ya kumuona nyoka huyo aliruka kutoka kwenye pikipiki na kuanguka pembeni mwa barabara na abiria wake alimwachia yule nyoka ambaye alikimbilia kwenye kalavati la maji.

Aliongeza kuwa ndipo alipopiga kelele za kuomba msaada na kundi la vijana waendesha pikipiki wenzake walifika eneo hilo la tukio kwa lengo la kumsaidia mwenzao juu ya maswahiba yaliyompata hadi kumfanya apige kelele.

Alisema kabla ya vijana hao hawajafanya jambo lolote, Komba aliwaomba vijana hao na watu wengine waliofika katika eneo hilo wasimpige nyoka wake kwani iwapo watampiga na kufa yeye pia atapoteza maisha. Kutokana na maneno hayo, Haule alimtoa nyoka huyo ndani ya kalavati na kwa kushirikiana na vijana wenzake walianza kumpiga nyoka huyo hadi kufa.

Alisema wakati wanampiga nyoka huyo, Komba ambaye ndiye mmiliki wa nyoka huyo naye alianza kulegea kisha akaanguka chini huku akitokwa na mapovu mdomoni na puani.

Habari zinasema kuwa,baada ya Komba kuanguka alikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu; hata hivyo juhudi za madaktari na wauguzi wa hospitali za kuokoa maisha yake zilishindikana kwani Komba alifariki.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa Songea.

Alisema nyoka aliyeuawa na wananchi amechukuliwa na idara ya maliasili na uchunguzi zaidi ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa nyoka na kisha mmiliki wake naye kufa. Kamanda Mwombeji alisema, kwa upande wa dereva wa pikipiki yeye anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma.

Aidha Kamanda Mwombeji, ametoa rai kwa wananchi kuacha mara moja kumiliki nyara za serikali zinazoweza kuwaletea madhara kama vile majeraha au vifo.

Source: Nyoka wa maajabu afa na mmiliki wake mkoani Songea | Bongo5.com

Tanzania kusikia mambo ya maendelea hapana Ila kwa uchawi du sayansi hiyi mpaka wazungu wanatuadabu
 
Kuna watu unaweza kuona wanatembea ukadhani ni watu kumbe sio watu ni majoka!
Sijui kwanani vijana tunakuta na tabia hizi, kule nyumbani kigoma nimeshuhudia kijana mdogo nae anamiliki joka kubwa tu. Mambo hizi zaman ilikuwa ni Kwa wazee tu
 
Rafiki yangu mmoja alimaliza ualimu, alipangiwa shule huko kwenye mipaka ya Msumbiji, tena shule yenyewe kijijini, ukisharipoti kwa mwalimu mkuu unafahamishwa kwa mwekiti na katibu wa kijiji.

Basi alinipa story kuwa kijijini waliona nyoka mkubwa anatembea, yeye alistuka sana, ile anataka kupiga kelele watu walisema aahh si nyoka wa Fulani yule, basi ananiambia Sky, yani kama kawaida yani kama kusema kuku wa Fulani au mbwa wa Fulani, alichoka. Alipigana mpaka alipata uhamisho.
 
Hao mapolisi wanaongea tu bila kufanya uchunguzi wowote. Hawana ujuzi wa kujua mtu ameuliwa na nini kabla ya kufanya uchunguzi wa marehemu.

Kwanza siamini kabisa kwamba hii story ya kweli.
Samahani Sana mkuu.

Bila samahani mkuu. Ila.mimi nimechagua kumuamini RPC kuliko afrodenzi, kwa sababu pia kazi ya uchunguzi huwa inafanywa na madaktari. You must have your reasons for not trusting them
 
Kuna story moja huko kusini nasikia joka lilikuwa kila siku limfanyie mama wa mwenye duka vitendo vya udhalilishaji (siwezi kuandika hapa) ndipo baba anatakiwa nae apite. Kila siku wanauza kufuru.Hicho kibarua mama lazima akifanye kila siku ya MUNGU.
Kwani nyoka ana "dudu" inayoweza kupenya kwa mwanamke?!!!!! looooh! bora nife maskini jamani, ushirikina hapana
 
Hii sayansi tungeitumia kwa shughuli za kimaendeleo tungekuwa mbali sana
 
Iko hivi haya madude/madudu kuna watu huwa wanaishi nayo lakini kwa masharti
Wengine ni ya urithi
Wengine waliyapata kwenye ishu za kutafuta kinga dawa utajiri na kadhalika
Sharti mojawapo ni kwamba siku ukiona huwezi kulilea tena unalirudisha ulipolitoa au unapewa maelekezo ya kwenda kulitupa
Ukikiuka masharti likafa nawe unakufa, hicho ndio kilichomtokea Komba
Wangekuwa na namba zako ungeweza kumuokoa marehemu mkuu.
 
Rafiki yangu mmoja alimaliza ualimu, alipangiwa shule huko kwenye mipaka ya Msumbiji, tena shule yenyewe kijijini, ukisharipoti kwa mwalimu mkuu unafahamishwa kwa mwekiti na katimu wa kijiji.

Basi alinipa story kuwa kijijini waliona nyoka mkubwa anatembea, yeye alistuka sana, ile anataka kupiga kelele watu walisema aahh si nyoka wa Fulani yule, basi ananiambia Sky, yani kama kawaida yani kama kusema kuku wa Fulani au mbwa wa Fulani, alichoka. Alipigana mpaka alipata uhamisho.
 
Huyu nyoka tumbatize tumpe jina JOKA KOMBA na ofisi ya waziri mkuu iagize JOKA KOMBA afanyiwe utafiti. Huu ni utajiri kwa nchi, ni utalii tosha.
 
Una simu kubwa sana hapo unayoweza itumia ku access ramani ya Tanzania au hukusoma Jiografia shule ya msingi?
unatumia akili kubwa kujibu vitu vidogo mwili kontena akili kisoda stupid
cc MNYAMAKAZI

Songwe ni mkoa now
Geita ni mkoa now
Manyara ni mkoa now
Simiyu pia ni mkoa now
kama ukielewa kwa nini nimendika hivi basi utaelewa swali langu pia
[HASHTAG]#useless[/HASHTAG]
[HASHTAG]#povu[/HASHTAG]
[HASHTAG]#nimepanic[/HASHTAG]
 
Huyo muendesha boda boda amenichekesha sana. Eti aliona kitu kinamtekenya, kugeuka hivi, salalee akakutana na bichwa la nyoka! Akaruka akatupa piki piki hukoo! Weee chezea na dawa ya sumu ya nyoka kuuzwa laki saba na nusu!
ha ha
 
Back
Top Bottom