MAAJABU: Nyoka afa na mmiliki wake Songea

Kuna story moja huko kusini nasikia joka lilikuwa kila siku limfanyie mama wa mwenye duka vitendo vya udhalilishaji (siwezi kuandika hapa) ndipo baba anatakiwa nae apite. Kila siku wanauza kufuru.Hicho kibarua mama lazima akifanye kila siku ya MUNGU.
acha niwe maskini tu watu wana roho za ajabu na uoga hawana nyoka anakuingilia unamwangalia tu kisa utajiri hapana
 
Rafiki yangu mmoja alimaliza ualimu, alipangiwa shule huko kwenye mipaka ya Msumbiji, tena shule yenyewe kijijini, ukisharipoti kwa mwalimu mkuu unafahamishwa kwa mwekiti na katimu wa kijiji.

Basi alinipa story kuwa kijijini waliona nyoka mkubwa anatembea, yeye alistuka sana, ile anataka kupiga kelele watu walisema aahh si nyoka wa Fulani yule, basi ananiambia Sky, yani kama kawaida yani kama kusema kuku wa Fulani au mbwa wa Fulani, alichoka. Alipigana mpaka alipata uhamisho.
Mweeee...
 
Sijui kwa nini wengine hawaamini kama mungu yupo! Ikiwa haya yanawezekana na yanafanywa na wanadamu ambao hata siku ya kuumbwa au kuzaliwa kwako hawakuwepo! why don't we believe in his Holy existence?
 
Mkazi wa Mtaa wa Mateka, Manispaa ya Songea, Denis Komba (26) kufa baada ya nyoka wake aliyekuwa amembeba kwenye mfuko wa jaketi kuuawa na wananchi.
xWood-snake-Fake-snake-toy-Turn-the-snake.jpg.pagespeed.ic.kaiIdkr6VT.webp

Komba alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma (Homso) ambako alilazwa baada ya watu wenye hasira kumuua kwa mawe na fimbo nyoka wake huyo.

Mashuhuda wanaeleza kuwa kabla ya wananchi kumuua nyoka huyo, Komba aliwasihi wasifanye hivyo kwa kuwa wakimuua na yeye angekufa, lakini ombi lake hilo halikusikilizwa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, siku ya tukio Komba alikodi pikipiki ya Kassian Haule (24) ambaye ni mkazi wa Mpitimbi, yenye namba za usajili MC 724 AKB ili apelekwe nyumbani kwake mtaa wa Mateka.

Akisimulia tukio hilo, alisema alipofika katika eneo la Benki ya Posta ya zamani barabara kuu ya Sokoine, dereva wa pikipiki alihisi kuna kitu kinamtekenya na kumgonga gonga kwa nyuma, ndipo alipogeuka nyuma na kumwona abiria wake amebeba nyoka mkubwa huku amesimamisha kichwa.

Haule alisema, baada ya kumuona nyoka huyo aliruka kutoka kwenye pikipiki na kuanguka pembeni mwa barabara na abiria wake alimwachia yule nyoka ambaye alikimbilia kwenye kalavati la maji.

Aliongeza kuwa ndipo alipopiga kelele za kuomba msaada na kundi la vijana waendesha pikipiki wenzake walifika eneo hilo la tukio kwa lengo la kumsaidia mwenzao juu ya maswahiba yaliyompata hadi kumfanya apige kelele.

Alisema kabla ya vijana hao hawajafanya jambo lolote, Komba aliwaomba vijana hao na watu wengine waliofika katika eneo hilo wasimpige nyoka wake kwani iwapo watampiga na kufa yeye pia atapoteza maisha. Kutokana na maneno hayo, Haule alimtoa nyoka huyo ndani ya kalavati na kwa kushirikiana na vijana wenzake walianza kumpiga nyoka huyo hadi kufa.

Alisema wakati wanampiga nyoka huyo, Komba ambaye ndiye mmiliki wa nyoka huyo naye alianza kulegea kisha akaanguka chini huku akitokwa na mapovu mdomoni na puani.

Habari zinasema kuwa,baada ya Komba kuanguka alikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu; hata hivyo juhudi za madaktari na wauguzi wa hospitali za kuokoa maisha yake zilishindikana kwani Komba alifariki.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa Songea.

Alisema nyoka aliyeuawa na wananchi amechukuliwa na idara ya maliasili na uchunguzi zaidi ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa nyoka na kisha mmiliki wake naye kufa. Kamanda Mwombeji alisema, kwa upande wa dereva wa pikipiki yeye anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma.

Aidha Kamanda Mwombeji, ametoa rai kwa wananchi kuacha mara moja kumiliki nyara za serikali zinazoweza kuwaletea madhara kama vile majeraha au vifo

Msemo huu huwa ni mgumu kuuelewa:

Mshahara wa Dhambi ni Mauti.

Kijana aliambatana na nyoka.

Songea na wenyewe wamo. Kuna tukio moja tena la nyoka ambapo Mama aliposhindwa kushika mimba alienda kwa mganga wa kienyeji na kumpa dawa. baadaye alipata mtoto, lakini kadri mtoto alivyokuwa akikua alimg'ata wakati wa kunyonya na baadaye yule mama alipooza, Kumbe yule mtoto alikuwa Nyoka. Baadaya ya maombezi alipona na yule joka akatoweka.

Uchawi upo, lakini ni kujilisha upepo hauna faida zaidi ya madhara na kifo.
 
huyo aling'atwa sumu ikiwa inamuingia taratibu.
Mwili wake ukifanyiwa autopsy au post-mortem mtuletee majibu hapa.
Maelezo yanasema mwili haukuwa na jeraha na pia maelezo ya marehemu 'msimuue mkimuua nami nitakufa'...yapo sana haya mambo kuna wanaojiunganisha na Mamba(Ukerewe,Nyasa nk.),Paka,Bundi(Pwani) shetani yupo sana na ana mambo ukiambiwa hutakubali ila Maandiko huyachambua sana na kujikinga nayo...Mwanasayansi anafanya mambo kwa USHAHIDI na ma-formula,mchawi ni kificho.
 
Mkazi wa Mtaa wa Mateka, Manispaa ya Songea, Denis Komba (26) amefariki baada ya nyoka wake aliyekuwa amembeba kwenye mfuko wa jaketi kuuawa na wananchi.

Komba alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma (Homso) ambako alilazwa baada ya watu wenye hasira kumuua kwa mawe na fimbo nyoka wake huyo.

Mashuhuda wanaeleza kuwa kabla ya wananchi kumuua nyoka huyo, Komba aliwasihi wasifanye hivyo kwa kuwa wakimuua na yeye angekufa, lakini ombi lake hilo halikusikilizwa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, siku ya tukio Komba alikodi pikipiki ya Kassian Haule (24) ambaye ni mkazi wa Mpitimbi, yenye namba za usajili MC 724 AKB ili apelekwe nyumbani kwake mtaa wa Mateka.

Akisimulia tukio hilo, alisema alipofika katika eneo la Benki ya Posta ya zamani barabara kuu ya Sokoine, dereva wa pikipiki alihisi kuna kitu kinamtekenya na kumgonga gonga kwa nyuma, ndipo alipogeuka nyuma na kumwona abiria wake amebeba nyoka mkubwa huku amesimamisha kichwa.

Haule alisema, baada ya kumuona nyoka huyo aliruka kutoka kwenye pikipiki na kuanguka pembeni mwa barabara na abiria wake alimwachia yule nyoka ambaye alikimbilia kwenye kalavati la maji.

Aliongeza kuwa ndipo alipopiga kelele za kuomba msaada na kundi la vijana waendesha pikipiki wenzake walifika eneo hilo la tukio kwa lengo la kumsaidia mwenzao juu ya maswahiba yaliyompata hadi kumfanya apige kelele.

Alisema kabla ya vijana hao hawajafanya jambo lolote, Komba aliwaomba vijana hao na watu wengine waliofika katika eneo hilo wasimpige nyoka wake kwani iwapo watampiga na kufa yeye pia atapoteza maisha. Kutokana na maneno hayo, Haule alimtoa nyoka huyo ndani ya kalavati na kwa kushirikiana na vijana wenzake walianza kumpiga nyoka huyo hadi kufa.

Alisema wakati wanampiga nyoka huyo, Komba ambaye ndiye mmiliki wa nyoka huyo naye alianza kulegea kisha akaanguka chini huku akitokwa na mapovu mdomoni na puani.

Habari zinasema kuwa,baada ya Komba kuanguka alikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu; hata hivyo juhudi za madaktari na wauguzi wa hospitali za kuokoa maisha yake zilishindikana kwani Komba alifariki.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa Songea.

Alisema nyoka aliyeuawa na wananchi amechukuliwa na idara ya maliasili na uchunguzi zaidi ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa nyoka na kisha mmiliki wake naye kufa. Kamanda Mwombeji alisema, kwa upande wa dereva wa pikipiki yeye anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma.

Aidha Kamanda Mwombeji, ametoa rai kwa wananchi kuacha mara moja kumiliki nyara za serikali zinazoweza kuwaletea madhara kama vile majeraha au vifo.

Source: Nyoka wa maajabu afa na mmiliki wake mkoani Songea | Bongo5.com
Duuh,wangoni bana,wachawi vibaya.
 
ukisoma coment za watu humu unaweza ukawa unacheka kama zombi barabarani. HAHHAHAHAHAHHA

eti Komba naye alikuwa maliasili kwiiii kwiii kwiii kwiii>

PALE NI JOKA NA MWANAE
 
umenikumbusha yule wa makambako anamlisha na chakula na ana mal utitiri
 
Itakuwa wakati wa purukushani huyo nyoka alomgonga jamaa
So kafa kwa kuumwa na nyoka
 
Kamanda Mwombeji arekebishe kauli, huyo nyoka sio nyara za serikali bali ni nyara za shetani
 
Back
Top Bottom