MAAJABU: Nyoka afa na mmiliki wake Songea

MAAJABU: Nyoka afa na mmiliki wake Songea

We ulikuwa hapo wakati anasema hayo maneno ?
Na unajuaje hakung'atwa. ?
Habari inasema kuwa marehemu alisema kuwa "mkimuua nae atakufa"
Pia maelezo ya Afisa wa polisi yanasema Marehemu alipelekwa hospital na hakukutwa na jeraha lolote
 
Kuna watu unaweza kuona wanatembea ukadhani ni watu kumbe sio watu ni majoka!
Kweli mkuu ndio maana mm ht sipendi sana kushikana mikono na watu. Unaweza kuwa unampa mkono mtu kumbe ni bonge la kiumbe la ajabu.
 
IMG_1208.JPG
Habari inasema kuwa marehemu alisema kuwa "mkimuua nae atakufa"
Pia maelezo ya Afisa wa polisi yanasema Marehemu alipelekwa hospital na hakukutwa na jeraha lolote




Mkuu unaona hicho kisigino hapo ameng'atwa na nyoka. Sasa we fikiria hizi ngozi yetu ya rangi nyeusi hiyo itaonekana kirahisi?

Jeraha la nyoka wengine ni ndogo hata huwezi kuona kitu. Sasa nauliza tena Je walifanya autopsy huko hospitalini kama ndio majibu yako wapi? Kama Hapana sababu ya kifo hakijulikani mwisho wa hadithi.
 
Nasubiri wana Sayansi wa JF walitolee Maelezo ki sayansi hili swala!
 
We shindwa kabisa....
Ashindwe nini?? Mbona haya mambo hapa songea ni kawaida!! Vp hukubahatika kumwona yule chatu mtu wa kule Kipera(Ruvuma??) wenyewe tumezoea.Haupiti mwez tunaona mengine.Karibun songea kwa mafunzo ya ushirikina.
 
wakamatwe hao vijana na wafunguliwe kesi ya mauaji, kwa kosa la kumuua huyo kijana komba bila sababu wakati alishawaeleza wakimuua nyoka na yeye atakufa. hao vijana wana murder kesi, ndugu za marehemu watafute mawakili wazuri watashinda kesi
vijana wamejihami..mwenye border border angepoteza maisha mana hakikuwa kitu cha kawaida au alipaswa amueleze kabla hajampakiza kuwa amebeba nini.
 
Please n pls n pls sikushauri kabisa
Poa nilisoma kwenye mtandao mmoja mkuu mmoja analalamika maisha magumu, ana wajibu wa kuhudumia wazazi na kusomesha wadogo zake 4 yuko tayari kupata fedha za masharti, nikachoka maana unaweza kupata halafu masharti yawe hutakiwi kuwasomesha ndugu zako. Nimeelewa nitauza ubuyu niongeze kipato hizo za masharti hapana.
 
Hata mie nilipenda kujua da! wauza maduka wengi nasikia ndio vifaa vyao vya kuitia wateja.
Du! yawezekana hata unanunua bidhaa dukani kumbe anayekupatia ni mnyama sio yule mwanadamu unayemuona pale!
Haya mambo ya kimila na kiutamaduni mengine sio kabisa!
 
Jamaa uhai wake unashikiliwa na mr snake?dunia hii ina mambo kwa kweli
 
Dunia ina mengi,Laiti vijana wangemkamata bila kumuua labda Komba asingefariki na siri au miujiza ya nyoka yule labda ingeeleweka.Lakini sasa ni ngumu kupata undani wake,african science ina wenyewe muulize Profesa Maji marefu.
 
Du! yawezekana hata unanunua bidhaa dukani kumbe anayekupatia ni mnyama sio yule mwanadamu unayemuona pale!
Haya mambo ya kimila na kiutamaduni mengine sio kabisa!
Kuna story moja huko kusini nasikia joka lilikuwa kila siku limfanyie mama wa mwenye duka vitendo vya udhalilishaji (siwezi kuandika hapa) ndipo baba anatakiwa nae apite. Kila siku wanauza kufuru.Hicho kibarua mama lazima akifanye kila siku ya MUNGU.
 
Mkazi wa Mtaa wa Mateka, Manispaa ya Songea, Denis Komba (26) amefariki baada ya nyoka wake aliyekuwa amembeba kwenye mfuko wa jaketi kuuawa na wananchi.

Komba alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma (Homso) ambako alilazwa baada ya watu wenye hasira kumuua kwa mawe na fimbo nyoka wake huyo.

Mashuhuda wanaeleza kuwa kabla ya wananchi kumuua nyoka huyo, Komba aliwasihi wasifanye hivyo kwa kuwa wakimuua na yeye angekufa, lakini ombi lake hilo halikusikilizwa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, siku ya tukio Komba alikodi pikipiki ya Kassian Haule (24) ambaye ni mkazi wa Mpitimbi, yenye namba za usajili MC 724 AKB ili apelekwe nyumbani kwake mtaa wa Mateka.

Akisimulia tukio hilo, alisema alipofika katika eneo la Benki ya Posta ya zamani barabara kuu ya Sokoine, dereva wa pikipiki alihisi kuna kitu kinamtekenya na kumgonga gonga kwa nyuma, ndipo alipogeuka nyuma na kumwona abiria wake amebeba nyoka mkubwa huku amesimamisha kichwa.

Haule alisema, baada ya kumuona nyoka huyo aliruka kutoka kwenye pikipiki na kuanguka pembeni mwa barabara na abiria wake alimwachia yule nyoka ambaye alikimbilia kwenye kalavati la maji.

Aliongeza kuwa ndipo alipopiga kelele za kuomba msaada na kundi la vijana waendesha pikipiki wenzake walifika eneo hilo la tukio kwa lengo la kumsaidia mwenzao juu ya maswahiba yaliyompata hadi kumfanya apige kelele.

Alisema kabla ya vijana hao hawajafanya jambo lolote, Komba aliwaomba vijana hao na watu wengine waliofika katika eneo hilo wasimpige nyoka wake kwani iwapo watampiga na kufa yeye pia atapoteza maisha. Kutokana na maneno hayo, Haule alimtoa nyoka huyo ndani ya kalavati na kwa kushirikiana na vijana wenzake walianza kumpiga nyoka huyo hadi kufa.

Alisema wakati wanampiga nyoka huyo, Komba ambaye ndiye mmiliki wa nyoka huyo naye alianza kulegea kisha akaanguka chini huku akitokwa na mapovu mdomoni na puani.

Habari zinasema kuwa,baada ya Komba kuanguka alikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu; hata hivyo juhudi za madaktari na wauguzi wa hospitali za kuokoa maisha yake zilishindikana kwani Komba alifariki.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa Songea.

Alisema nyoka aliyeuawa na wananchi amechukuliwa na idara ya maliasili na uchunguzi zaidi ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa nyoka na kisha mmiliki wake naye kufa. Kamanda Mwombeji alisema, kwa upande wa dereva wa pikipiki yeye anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma.

Aidha Kamanda Mwombeji, ametoa rai kwa wananchi kuacha mara moja kumiliki nyara za serikali zinazoweza kuwaletea madhara kama vile majeraha au vifo.

Source: Nyoka wa maajabu afa na mmiliki wake mkoani Songea | Bongo5.com
Mshana junior, kuja pande hii tafadhali.
 
Back
Top Bottom