MAAJABU: Nyoka afa na mmiliki wake Songea

Kwa hiyo marehemu aliiunganisha nafsi au roho yake na nyoka? aisee huo ni utaalam wa gizani mshana jr hivi hii nayo tunaiita reincarnation?
Iko hivi haya madude/madudu kuna watu huwa wanaishi nayo lakini kwa masharti
Wengine ni ya urithi
Wengine waliyapata kwenye ishu za kutafuta kinga dawa utajiri na kadhalika
Sharti mojawapo ni kwamba siku ukiona huwezi kulilea tena unalirudisha ulipolitoa au unapewa maelekezo ya kwenda kulitupa
Ukikiuka masharti likafa nawe unakufa, hicho ndio kilichomtokea Komba
 
Alisema nyoka aliyeuawa na wananchi amechukuliwa na idara ya maliasili na uchunguzi zaidi ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa nyoka na kisha mmiliki wake naye kufa


Wanatumia kipimo gani kubaini hayo mahusiano ya nyoka na binadamu
 
Duh hii ni kuzidi kuonyesha, binadamu wote tunawaona wengine ni mashetani.

Mungu ni mwema.
 
Wamchunguze vizuri marehemu, yawezekana alibwia sumu kimyakimya pindi nyoka wake anaadhibiwa na wananchi, akaona afe mapema kabla mambo aliyodanganywa na mganga wake hayajawa dhahiri.

Waafrika sisi.
 
Serikali hawaamini UCHAWI.
Haya hapa chini yamesemwa na wataalam wa serikali

"Alisema nyoka aliyeuawa na wananchi amechukuliwa na idara ya maliasili na uchunguzi zaidi ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa nyoka na kisha mmiliki wake naye kufa. Kamanda Mwombeji alisema, kwa upande wa dereva wa pikipiki yeye anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma."
 
Huyo muendesha boda boda amenichekesha sana. Eti aliona kitu kinamtekenya, kugeuka hivi, salalee akakutana na bichwa la nyoka! Akaruka akatupa piki piki hukoo! Weee chezea na dawa ya sumu ya nyoka kuuzwa laki saba na nusu!
kuna jiwe la nyoka linanyonya sumu yooote ya Nyoka yapo sana Ugweno na kule kusini halizid 5000
nunua la akiba ubaki nalo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom