Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,553
Vanessa Bryant atalipwa na Maafisa wa Polisi na Zimamoto wa Kaunti ya Los Angeles zaidi ya Bilioni 65 za Kitanzania kwa kusambaza Mtandaoni picha za Ajali Mbaya ya Helkopita iliyoua Mumewe na Binti yake Januari 26, 2020
Kwa kuzingatia Ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosisitiza Haki ya Faragha, Unazungumziaje hali halisi ya Utunzaji wa Faragha za watu iliyopo kwenye Mazingira yetu?
====
Vanessa Bryant ambaye ni Mke wa Staa wa mpira wa kikapu wa Marekani Marehemu Kobe Bryant, amekubali kulipwa fidia ya dola za kimarekani milioni 28.8 ($28,850,000) kutokana na makosa yaliyofanywa na Nchini Marekani ya kusambaza picha za ajali ya Helikopta iliyomuua Mumewe a Mtoto wao January 26 mwaka 2020.
Kwenye kesi hiyo iliyofunguliwa na Vanessa Bryant a Chris Chester ambaye naye alipoteza Mke a Mtoto kwenye ajali hiyo, waliwashitaki Maafisa hao kwa kitendo cha kuchukua picha za mabaki ya Binadamu waliofariki kwenye eneo la tukio kama "ukumbusho" na kuzisambaza, kitendo ambacho Vanessa alisema kilimfanva apitie changamoto za kihisia na kuweweseka usiku hivvo akaiburuza Taasisi hivo Mahakamani kwa uzembe na uvamizi wa haki za faragha.
Habari kutoka Los Angeles zinasema sasa Vanessa (40) amefikia makubaliano ya mwisho na Kaunti ya Los Angeles na kukubali kulipwa dola za kimarekani milioni 28.85 kutoka kwa Bodi va Wasimamizi wa Kaunti hivo ambapo makubaliano hayo yanajumuisha madai kutoka kwa Vanessa na yanahusu madai yoyote ya baadaye kutoka kwake na Watoto wa Kobe ambao ni Natalia (20), Bianka (6) na Capri (3).
Jimbo la California tangu wakati huo limepitisha sheria ya jimbo inayokataza Maafisa vya Vikosi vya Dharura na Uokoaji kupiga bila ruksa picha za Watu waliofariki katika eneo la ajali au uhalifu.
Chanzo: Millard Ayo