Waathirika ajali ya Precision Air waanza kulipwa fidia kwa siri

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
Ikiwa zimepita siku saba tangu kutokea kwa ajali ya ndege ya Shirika la Precision Air na kusababisha vifo vya watu 19, shirika hilo limeanza mchakato wa malipo ya fidia kwa familia zilizoathiriwa na ajali hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Novemba 14, 2022, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Patrick Mwanri amesema mchakato huo utakaokuwa kati ya familia za waliothirika na shirika hilo utakuwa wa siri na utafanyika kwa umakini mkubwa.

Mkurugenzi huyo hakuweka wazi kiasi gani ambacho waathirika watalipwa, hata hivyo wiki iliyopita Mwenyekiti wa Chama cha Kampuni za Bima, Khamis Suleiman aliiambia Mwananchi kuwa inapotokea ajali ya ndege bima inatakiwa kumlipa mwathirika Sh300 milioni.

Akizungumza leo Mwanri amesema, “Shirika letu lina bima na ipo kulingana na taratibu za uendeshaji mashirika ya ndege. Hivi ninavyoongea taratibu zile zimeshaanza na wahusika tumeshaanza kuwasiliana nao ili waweze kupata taarifa rasmi ya nini kinahitajika.

“Mara nyingi suala hili hufanyika kwa faragha kati ya wahusika na sisi hatutalileta hadharani.Tuna mawasiliano ya karibu na majeruhi wote tangu wakiwa hospitali hata baada kutoka tukiwasaidia kwa namna mbalimbali kadiri ya uwezo wetu,”.

Pamoja na hilo Mwanri amesema shirika hilo lilichukua jukumu la kusafirisha miili yote kulingana na matakwa ya familia husika zilizopatwa na misiba.

Wakati wa shughuli ya kuaga miili hiyo mkoani Kagera, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema Serikali itasimamia gharama za mazishi na kuagiza wakuu wa Mikoa ambapo miili hiyo itapelekwa wasimamie zoezi hilo kikamilifu.

Ndege hiyo ilianguka katika Ziwa Victoria takribani mita 100 kutoka Uwanja wa Ndege wa Bukoba, mkoani Kagera ikiwa na watu 43 waliokuwa wakitoa jijini Dar es Salaam, kati yao 39 wakiwa abiria, marubani wawili na wahudumu wawili.

Baada ya ajali hiyo iliyotokea Novemba 6, mwaka huu saa 2:53 asubuhi, shughuli za uokoaji kwa sehemu kubwa zilifanywa na wavuvi wakiongozwa na kijana Jackson Majaliwa na wenzake waliowezesha watu 24 kuokolewa.

MWANANCHI
 
Kuna mtaalumu fulani alielezea kuhusu malipo hayo ya Bima, nilimsikiliza juzi hapa, hio milioni 300 sijui ni wangapi watafikia maana anasema ili ulipwe.

1. Itategemea uneathirikaje? Yaani kama ni kifo au kujeruhiwa au ulemavu,kama umejeruhiwa ni kwa kiasi gani huwezi kufanya kazi tena.

2. Kama ulikuwa msafiri ukafa,inategemea umeacha warithi wangapi waliokuwa wanakutegemea.

3. Kipato chako ulichokuwa unaingiza kabla ya ajali ndio kitaamua warithi wako walipwe kiasi gani?

Kwahio mambo ni mengi mno nadhani labda hio 300mil ni maximum lakini vigezo navyo ni vingi sana.
 
Huu utakuwa uzushi kwasababu uchunguzi bado.
...Uchunguzi Gani? Itakavyokuwa Vyovyote, Binadamu 19 wamefariki. Ndugu zao Wanastahili Malipo!.
Uchunguzi Itasaidia Nini Kwa Hao na wameishafariki??
 
kwa nini fidia ?

ni ajali ya makusudi ?
1668445596509.png
 
Mkurugenzi wa Precision Air mh Mwanri amesema kampuni yake imeanza mchakato wa kuwalipa Fidia Familia za walioathirika na Ajali

Mkurugenzi amesema mchakato utahusisha Taasisi mbalimbali za Kimataifa na kwamba mkataba baina ya kampuni na Waathirika utakuwa wa Siri

Source ITV habari
 
Back
Top Bottom