Maadili ya viongozi wa umma ni nguzo muhimu kwa ustawi wa taifa hili, viongozi wetu lazima wajitafakari na hili

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
232
260
Maadili ni nyenzo muhimu na nguzo kwa viongozi wa Umma katika kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi zao kwa manufaa
ya wananchi na kwa taifa kwa ujumla.
Hakuna maendeleo yoyote katika nchi ambayo yanaweza kupatikana iwapo viongozi ambao ndio watendaji wa kazi watashindwa kufuata maadili ya kazi zao katika kutekeleza majukumu yao. Hivyo ni jukumu letu sote kama wananchi na viongozi wetu kukumbushana Maadili ya kazi zetu ili kuleta Amani, Usawa na Haki ya kidemokrasia nchini.
Ni vema Viongozi wa Umma wakafuata maadili katika utendaji wao wa kazi ili kuwawezesha wananchi kuwa na imani nao, na pia kuwawezesha kufanya kazi zao vizuri na kwa ufanisi mzuri kwa maslahi ya Taifa na pia kwa wanachi wanaowaongoza.Si wanasiasa na wale walioko Katina Nyumba za ibada
Msingi wa kudhibiti maadili ya Viongozi wa Umma unatokana na ibara ya 132 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa Ibara hiyo, Bunge limetakiwa kutunga Sheria ya Maadili kwa kuanisha misingi ifuatayo:-
  • Kufafanua nafasi za madaraka ambazo watu wenye kushika nafasi hizo watahusika nayo.
  • Kuwataka watu wanaoshika nafasi fulani za madaraka kutoa mara kwa mara maelezo rasmi ya mapato, rasilimali na madeni yao.
  • Kupiga marufuku mienendo na tabia zinazopelekea kiongozi aonekane hana uaminifu, anapendelea au si muadilifu au anaelekea kukuza au kuchochea rushwa katika shughuli za umma au anahatarisha maslahi au ustawi wa jamii.
  • Kufafanua adhabu zinazoweza kutolewa kwa kuvunja misingi ya maadili.
  • Kuelekeza taratibu, madaraka na desturi zitakazofuatwa ili kuhakikisha utekelezaji wa maadili.
  • Kuweka masharti mengine yoyote yanayofaa au ambayo ni ya muhimu kwa madhumuni ya kukuza na kudumisha uaminifu, uwazi, kutopendelea na uadilifu katika shughuli za umma na kwa ajili ya kulinda fedha na mali nyinginezo za umma.
    Kwa kuzingatia msingi wa kudhibiti maadili ya viongozi wa umma, jukumu mojawapo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni:- Kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi yoyote wa umma.Tujipime kama Taifa na haya tunayoyaona viongozi wetu mkisemana ovyo,mkilumbana ovyo ovyo,baadhi yenu mkiongea hadharani uongo,fitna chuki baina yenu mnaliweka Taifa Katika ombwe la Kukosa uadilifu kwa Vijana wengi...Watanzania wengi wanaona wanaelewa na Manajua kwa Ndani baadhi ya matendo ya wenzetu tuliowapa nafasi za kutuongoza na kututumikia wakikiuka wazi wazi makubaliano yetu kikatiba..wawe waadilifu,Tunahitaji ushauri wa Pamoja nini kifanyike Huko tuendako ,Nawakilisha
 
Tujipime kama Taifa na haya tunayoyaona viongozi wetu mkisemana ovyo,mkilumbana ovyo ovyo,baadhi yenu mkiongea hadharani uongo,fitna chuki baina yenu mnaliweka Taifa Katika ombwe la Kukosa uadilifu kwa Vijana wengi...Watanzania wengi wanaona wanaelewa na Manajua kwa Ndani baadhi ya matendo ya wenzetu tuliowapa nafasi za kutuongoza na kututumikia wakikiuka wazi wazi makubaliano yetu kikatiba..wawe waadilifu,Tunahitaji ushauri wa Pamoja nini kifanyike Huko tuendako ,Nawakilisha
Naunga mkono hoja.
P
 
Wanasiasa 'Mercenary' ni hatari sana kwa mustakabali wa Taifa letu.
 
Back
Top Bottom