Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2024.
Jaji Mkuu Profesa Ibrahim ameyasema hayo leo tarehe 1/2/2024 kwenye maadhimisho ya siku ya sheria yaliyo fanyika Jijini Dodoma.
Jaji Mkuu amesema kufuatia kwa teknolojia ya kisasa kufungwa kwenye mahakama zote itasaidia kuandika na kutafasiri kwenye lugha mbalimbali hivyo kazi za Mahimu na Majaji itakuwa ni ndogo tu nayo ni kutoa maamuzi.
Hatua hii ya matumizi ya tehama itasaidia kuharakisha usikilizwaji wa kesi na kutolewa kwa hukumu kwa wakati.
Pongezi kwa mahakama kwa kupiga hatua kubwa, sasa wananchi wanacho subiri ni utekelezaji.