Maadhimisho ya miaka 35 ya CCM live Star tv

Maadhimisho ya miaka 35 ya CCM live Star tv

tuchague viongozi safi,waadilifu na wenye mvuto kwa jamii.wazalendo na wachapa kazi.
 
Hi picha ya sio ya leo! Pili umati huu huwa unafuata vitu viwili. Moja ni wasanii wanaoletwa na ccm ktk

mikutano na mikusanyiko yao. Pili wanafuata chakula/hela ambazo zinatolewa
ilihali wananchi wanakosa huduma za muhimu kama afya elimu etc. Mtalaaniwa wooote mnaohusika na upuuzi huu.


Ndiyo yale yale ya kura zimechakachuliwa.Picha hizi ni za leo katika matembezi toka Ofisi za Chama mpaka viwanja vya Furahisha.Kukataa picha hizi zinaonyesha baadhi ya watu kutokuamini kama magamba wameweza kupata ''nyomi''.Habari ndiyo hiyo, tazama Michuzi ama Mjengwa Blog.
 
tunao wanachama hawana mapenzi mema na chama hiki.leo utamsikia akisema hivi kesho vile lakini bado wanajiita wana ccm.si kweli.
 
Watu wameongeza kasi ya kutoka hasa mkuu wa nyumba alipo anza speech yake ya kusoma kama msoma risala ni balaa jamaa hawana mvuto nimeamini wamebaki na watu walotoka vijini na malori ambao wao mpaka mkutano uishe kabisa!
 
Ni wakati sasa wa kuachana na viongozi wabovu,wachochezi mnawajua,wazalendo mnawafahamu,wanaowagawa wananchi mnawafahamu hivyo tumieni fursa hiyo vizuri
 
Mwenyekiti wa chama mkoa ametoa tamko kuwa baada ya sherehe hizo kutakuwa na chakula kinachowatosha watu wote waliopo uwanjani...hii ni ajabu na kweli wakuu.

Teh teh teh teh teh....yani hicho ndicho walichowategea watu,na wamewapata kweli kweli,wewe mtu alikua hana uhakika wa mlo leo kwa nini hasijimwage kirumba....ila 2015 watabaki midomo wazi....yaani umati wote ule na ubwabwa wamekula lakini lo wanatutosa....ccm ni sawa na babu jinga.......
 
Hivi yule jamaa aliyeona mbali na kutaka kumtungua JK kutoka jukwaani wakati wa kampeni 2005 yupo wapi? Inanikumbusha mbali sana kwa sababu enzi hizo tulikuwa tunamwona JK ni lulu kwa kuwa watu wengi tulikuwa hatumfahamu vizuri.
 
wale watu wenye sifa chafu na wenye tuhuma tusiwachague.tusichague viongozi wanaotoa fedha.yaani elfu moja inakufanya uchague kiongozi mbovu.
 
hili la sifa katika chama chetu la wananchi kununuliwa limevunja heshima ya chama chetu sana
 
tunapochagua wagombea tuangalie changamoto zilizoko mbele yetu hususan 2014 kwenye serikali za mitaa na 2015 uchaguzi mkuu
 
Mimi ni CCM damu, ila siunge mkono wehu wengi walioko madarakani, wangekua poa tusingepoteza majob=mbo mengi, inaonyesha jinsi ubinafsi na uchovu uliopo. Nataka kusema nini, Uwanjani naona waliokimbilia kwenye Jukwaa la Wasanii ni nyekundunyekundu fulani hivi sioni Kijani kama nilivyotarajia, mavazo ya kawaida ni mengi. Maana yake nini, waliokuwa wanapita na wasio na shughuli mjini wamesikia habari ya pilau na mziki mkubwa unaongurumishwa Kirumba lazima ukimbilie kuona kulikoni.... si unatujua watanzania hata Bomu tunalikimbilia. Natumaini kuna Ambulance na Redcross wakutosha uwanjani, maana raia wengi wasiowahi kuona matamasha watakuwa wameingia

pumbavu kabisa! umezaliwa huko mpaka uwe ccm damu! mgando kabisa wewe...
 
ana shusha nondo za kufa mtu uwanja wote umezizima.......!!!

Duh! Kwa ambaye haangalii unaweza kumdanganya vizuri,kiukweli uwanja watu ni restless.movement here and there!njaa!sijui ngombe 50 wameenda wapi?
 
Back
Top Bottom