Maadhimisho ya miaka 35 ya CCM live Star tv

Pamoja na ukata mkali lakini bado kuna "nyomi" CCM .Hapa kweli Dr. Bana anasema magamba hawana mbadala.

download+(40).jpg




download+(41).jpg
Ukitaka kuamini mtaji wa magamba ni wajinga ona mitego wanayotumia kuuteka umati!
 
Maadhimisho ya CCM live Startv

Mwenyekiti wa chama mkoa ametoa tamko kuwa baada ya sherehe hizo kutakuwa na chakula kinachowatosha watu wote waliopo uwanjani...hii ni ajabu na kweli wakuu.
 
Ukizngatia fundi wake sheikh yaya ndio hayupo sasa cjui ule ulinzi usioonekana, nani atampatia?
 
Kwa haya matamshi ya watu akiyoana atajisikia je na atachukua uamuzi gani?
 
Maadhimisho ya CCM live Startv

Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa mwanza ametangaza kuwa baada ya maadhimisho watu wote wa uwanjani wasiondoke kwa kuwa watapewa chakula na kila mtu atakula.

Nimepata jibu kuwa kilichowavutia watu kwenda kwa wingi uwanjani ni chakula.Hivi CCM wanapata wapi pesa za kuwalisha watu wote hao?

Hivi CCM wana jeshi lao?
 
Duh watanzania njaa zitatuuwa pamoja na hali mbaya kiuchumi hospitali watu wanakufa kwa kukosa huduma lakini mijitu imejijaza uwanjani. Kweli hii laana
 
Aliyefikiri ujinga ni kutokujua kusoma na kuandika aliwadanganya watanzania. Maana ni ngumu sana kupambana na adui ujinga. Kwa hali hii itachukua muda sana watu kuondokana na adui huyo wa maendeleo.
 
Maadhimisho haya ya CCM yanaonyesha ambavyo umaskini wetu ni mtaji mkubwa sana kwa CCM..yaani ukiangalia asilimia 95 ya waohudhuria wanasubiri wali baada ya sherehe kwisha.Nadhani ndio sababu CCM haina mpango madhubuti ulio wazi na wenye utashi wa kisasa kuondoa umaskini wa watanzania.Kweli tumeshikwa kwa huu umaskini wetu ambao mimi nasema ni artificial.
 
sasa ndio najua tatizo letu watanzania ni CCM, ebu fanyeni hesabu, chama kilizaliwa 5/2/1977 leo tare 5/2/2012 ni miaka mingapi? mimi kwa kesabu zangu hii ni miaka 34! sasa wenzetuuu hiiii 35 yatoka wapi????
Kwani wewe hujui kuwa somo la hisabati ni mkwe wa watanzania?
 
Niko hapa mwanza ndani ya daladala kuelekea buswelu.Njiani ni msululu wa malori yamejaza watu.jua ni kali mno na inaonekana hawa watu wanatokea mawilayani.Hii hali ya kulundika watu kwenye malori mchana na jua kali ni udhalilishaji wa binadamu.mbaya zaidi waliobebwa wanaonekana wamechoka sana na hawana raha kabisa yaani kama wamelazimishwa vile
 
Mwenyekiti wa chama mkoa ametoa tamko kuwa baada ya sherehe hizo kutakuwa na chakula kinachowatosha watu wote waliopo uwanjani...hii ni ajabu na kweli wakuu.

Dah! si ajabu na nauli itatolewa kwa kila mmoja.
 
Back
Top Bottom